Wednesday, 4 December 2019

Kauli Ya Humphrey Polepole Baada Ya Sumaye Kung'oka CHADEMA

...
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amemwambia Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye kuwa alimueleza asingeweza kupata kazi ya kushauri chama chochote cha siasa kama angekuwa nje ya Chama Cha Mapinduzi.

Polepole ametoa kauli hiyo saa chache baada ya Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye kutangaza kujiondoa ndani ya CHADEMA kwa kile alichokidai kuwa hakuna demokrasia ya kweli.

Polepole ameandika; Mzee nilikwambia, kazi ya ushauri hutaipata ukiwa nje ya CCM wenzako wanaotushauri na tunazingatia ushauri wao kwasababu tunawaheshimu, ni wana CCM na kiitikadi tuko pamoja. Sasa umebaki bila Itikadi. Ile ni mali ya Mtu ni yake, nilikwambia mwache, ona sasa unahama mara ya pili
🙆🏽‍♂️



Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger