Monday, 2 December 2019

Hage Geingob Achaguliwa Tena Kuwa Rais wa Namibia.....Umoja wa Afrika Watoa Neno, Rais Magufuli Ampongeza

...
Rais wa sasa wa Namibia Hage Geingob ameshinda kwa muhula wa pili licha ya kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya wapiga kura wanaomuunga mkono. Rais Geingob amepata  ushindi wa asilimia 56.3  ikilinganishwa na asilimia 86.7 ya mwaka 2014.

Tume ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Umoja wa Afrika (AUEOM) imesema uchaguzi huo umefanyika kwa kufuata sheria za ndani na kukidhi vigezo vya kimataifa.

Taarifa iliyotolewa  na tume hiyo imepongeza serikali na watu wa Namibia kwa kufanya uchaguzi mkuu kwa amani, na kusema uchaguzi huo uliofanyika Novemba 27 umewapatia watu wa Namibia fursa ya kuwa na uhuru wa kueleza maoni yao.

Tume hiyo pia imeipongeza serikali ya Namibia kwa kuidhinisha Katiba ya Afrika kuhusu Demokrasia, Chaguzi na Utawala iliyopendekezwa na Umoja wa Afrika kufuatia uchaguzi mkuu wa mwaka 2014. 


Rais wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli ni miongoni mwa Marais waliotuma salamu za Pongezi kwa   Hage Geingob kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais ya Namibia kwa Muhula wa Pili.

"Hongera sana Mhe. Rais Hage Geingob. Your re-election is clear testimony of the trust and confidence that Namibians have bestowed on you. I wish to assure you of our continued support to further strengthen the historical ties between our two brotherly countries."Ameandika Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger