Halmashauri Kuu Taifa ya Chama cha United People's Democratic Party (UPDP) imemvua uenyekiti Fahmi Dovutwa baada ya kubainika kufanya kosa la kukisemea chama hicho kinyume na katiba.
Uamuzi huo ulitangazwa jana Jumapili Desemba 2, 2019 Mjini Unguja, Zanzibar na Kaimu Mwenyekiti wa UPDP Taifa, Abdalla Mohammed Khamis akisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao hicho kujadili kwa kina makosa alioyafanya Dovutwa.
Alisema kosa kuu lililopelekea kuvuliwa kwa wadhifa wake ni kukisema chama hicho kuwa hakitoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Novemba 24, 2019, kitendo ambacho alikifanya bila kuagizwa wala kupata ridhaa ya uongozi wa chama hicho.
Alisema suala la chama hicho kutoingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa imekiathiri kwani utekelezaji wa agizo alilotoa Dovutwa limesababisha chama kukosa wenyeviti wa serikali hizo ambao wataweza kuwakilisha chama.
Khamis alisema Dovutwa anaweza kukata rufaa endapo atahisi amevunjiwa haki yake kisheria na kikatiba na kwa sasa atabaki kuwa mwanachama wa kawaida.
0 comments:
Post a Comment