Sunday, 1 December 2019

ESTHER MATIKO AULA UENYEKITI CHADEMA KANDA YA SERENGETI.... KUONGOZA SHINYANGA,MARA NA SIMIYU

...




Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog 
Mbunge wa jimbo la Tarime mjini Esther Matiko, ameibuka kidedea kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti, mara baada ya kuwashinda wagombea wenzake watatu waliokuwa wakiwania nafasi hiyo, akiwamo John Heche Mbunge wa Tarime vijijini ambaye alikuwa akitetea kiti chake.


Uchaguzi huo umefanyika leo Desemba mosi 2019  kwenye ukumbi wa mikutano Karena hoteli Shinyanga mjini,  ambao umehudhuriwa na wajumbe kutoka mkoani ya Simiyu, Mara pamoja na Shinyanga, mikoa ambayo inaunganisha Kanda hiyo ya Serengeti.

Aidha uchaguzi huo  ulihusu nafasi ya mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti, Makamu Mwenyekiti, pamoja na Mweka hazina na umesimamiwa na mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema Taifa Boniface Jacob, ambaye pia ni mstahiki Meya wa Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi huyo wa uchaguzi Boniface Jacob, amemtangaza Esther Matiko kuwa mshindi wa nafasi ya uenyekiti Chadema Kanda ya Serengeti kwa kupata kura 44, akifuatiwa na John Heche kura 38, nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mshemas Yakobo aliyepata kura tatu (3), pamoja na Alex Malima ambaye hakupata kura.

Nafasi ya Makamu mwenyekiti ametangazwa Gimbi Masaba ambaye amepata kura 45, akifuatiwa na King Tarai kura 38, pamoja na Jackson Luyobya kura 12, pia nafasi ya mwekahazina ametangazwa Maendeleo Makoye kura 42, akifuatiwa na Catherine Ruge kura 32, huku jumla ya kura zote zilizopigwa ni 85.

Akizungumza mara baada ya kupata ushindi wa nafasi hiyo ya Uenyekiti Chadema Kanda ya Serengeti Mbunge Matiko, amewataka wajumbe hao kuondoa makundi yaliyokuwepo wakati wa kupiga kampeni, na kuungana kuwa kitu kimoja ili wafanye kazi kwa ushirikiano na kukijenga chama.

“Nashukuru sana wajumbe kwa kunipigia kura na kunichagua kuwa mwenyekiti wenu wa Chadema Kanda ya Serengeti, ila naomba kwenu kitu kimoja muondoe makundi yaliyokuwepo wakati wa kupiga kampeni ya kupata viongozi, bali tunapaswa kuwa kitu kimoja,”amesema Matiko.

Naye msimamizi wa uchaguzi huo ,Jacob, amewapongeza wajumbe hao kwa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia bila ya kuwepo na vurugu zozote, huku akitoa wito kwa wana- Chadema wote kuwa siku ya uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti wa Chadema Taifa, wafanye uchaguzi wa haki na kuzingatia demokrasia.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Msimamizi wa uchaguzi Chadema Kanda ya Serengeti, Boniface Jacob akitangaza matokeo ya nafasi ya uenyekiti, makamu mwenyekiti na mwekahazina. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko, akizungumza mara baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya mwenyekiti Kanda ya Serengeti, inayo unganisha mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara.

Washindi wa uchaguzi Chadema Kanda ya Serengeti, wa kwanza mkono wa kulia ni mwenyekiti Esther Matiko, katikati makamu Mwenyekiti Gimbi Masaba, akifuatiwa na Mweka hazina Maendeleo Makoye.

Wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.

Wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.

Wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.

Wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.

Wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.

Wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.

Baadhi ya wagombea wakiwa na hofu ya matokeo kabla hayajatangazwa.

Makamu mwenyekiti Chadema Kanda ya Serengeti Gimbi Masaba akishangilia ushindi.

Mwenyekiti Chadema Kanda ya Serengeti Esther Matiko, akishangilia ushindi.

Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger