Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema nchi ya Ujerumani imetangaza rasmi kufadhili Tafiti za Kisayansi nchini Tanzania ili kuongeza chachu ya maendeleo ya kisayansi na kufanya tafiti kukua zaidi.
Ndalichako aliyasema hayo jana usiku wakati akifungua Mkutano wa Baraza la sayansi,teknolojia na ubunifu uliofanyika hotel ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
Proffesa Ndalichako alisema Ufadhili huo utasaidia kwa kuibua na kukuza tafiti mpya ambazo zitazaa matunda katika jamii hasa katika soko la ajira nchini.
“Tunapokea kwa mikono miwili ufadhili huu toka Ujerumani najua utasaidia kuibua tafiti mpya ambazo zinaenda sambamba na soko la Ajira nchini”,alisema Ndalichako.
Aliongeza kuwa Tanzania ipo tayari kuunga mkono tafiti za kisayansi pamoja na teknolojia mbalimbali ili kufanya upatikanaji wa masoko mapya yenye rasilimali watu wa kujitosheleza.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kupokea Mapendekezo ya tafiti kutoka kwenu ambayo mtayatoa katika Mkutano huu kwa nia ya kufanya tafiti katika nchi zetu za Afrika zinaleta tija na chachu ya Maendeleo”,alisema Ndalichako.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi nchini (COSTECH) Dr. Amos Nungu alisema kuwa kwenye Mkutano huo watajadili Namna ya kukuza ushirikiano kati ya Taasisi ambazo zinafadhili katika nchi za Afrika,kubadilishana uzoefu wa kisayansi katika tafiti na namna watakavyoweza kufanya ushirikiano wa kufanya kufanya miradi mipya ya kitafiti.
0 comments:
Post a Comment