Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema mbunge anayekataa bajeti ya Serikali bungeni ni mpuuzi.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo wakati akiahirisha Bunge la sita la Vijana la mwaka 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma.
"Kuna mambo matatu katika bajeti, kusema ndio, hapana au kukaa kimya ambako ni ishara ya kuwa hujakataa au kukubali lakini unasema hapana kwa sauti kubwa hivi unamwelewa mtu huyo kweli," amesema Ndugai.
Spika amesema bajeti zinazokataliwa na wapinzani huwa zimebeba mishahara yao na watumishi wengine, fedha za miradi ya maendeleo na kwamba kusema hapana ni sawa na kutaka kila kitu kisipelekwe.
0 comments:
Post a Comment