Monday, 4 November 2019

Rais Magufuli Ampa Maagizo Mazito CAG Mpya....." Usijifanye Muhimili, Kaliheshimu Bunge"

...
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere, leo Novemba 4 Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumpa maagizo katika kazi yake mpya.

Moja ya maagizo aliyompa ni kuhakikisha anasuka upya uongozi ndani ya taasisi hiyo ili kuhakikisha kuwa inafanya kazi kulingana na sheria na maagizo  ya mihimili inayoongoza nchi.

Maagizo mengine aliyopewa ni, "CAG nenda kafanye kazi huko, usije ukajifanya na wewe ni muhimili mwingine, mihimili ni mitatu na umeshaiona hapa. Nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa Serikali, kafanye kazi zako vizuri bila ya kuonea watu.


 “Unapopewa kazi na mihimili mingine kama Bunge au Mahakama kaitekeleze usibishane nao wewe ni mtumishi. Kasimamie hiyo ofisi kuna baadhi ya watendaji wako wanapokwenda kukagua kwenye balozi wanaomba fedha, sasa nenda kawachambue.” Amesema Rais Magufuli.

Aidha, amesema Rais ana mamlaka ya kumtoa CAG kulingana na Katiba na Sheria akieleza kuwa upo uwezekano wa mtumishi wa nafasi hiyo kutolewa muda wowote hata chini ya miaka mitano.

"Unaweza kumaliza miaka yako mitano au ukaishia mmoja. katika maisha ya duniani huwezi ukapewa mamlaka ya kuteua halafu usiwe na mamlaka ya kutengua, sikutishi lakini wewe nenda kafanye kazi zako"

Kuhusu suala la rushwa, Rais Magufuli amesema, "lakini pia kasimamie hiyo ofisi kuna baadhi ya watendaji wako wanapotumwa kwenda kukagua kwenye balozi wanalipwa pesa hapa na wakifika huko nako wanaomba pesa, ofisi ya CAG sio safi kama mnavyofikiri".


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger