Tuesday, 5 November 2019

Prof. Mussa Assad Aahidi Kumpa Ushirikiano CAG Mpya.....Ataja Kazi Yake Mpya Atakayoifanya Kwa Sasa

...
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake, Prof. Mussa Assad ameahidi kumpa ushiarikiano wowote atakaouhitaji CAG mpya, Charles Kichere kwani wao wanafahamiana kwa kipindi kirefu tangu akiwa anafundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Novemba 5, alipokuwa akimkabidhi Kichere ofisi ambapo amesema kuwa akihitaji kitu kutoka kwake au kutokana na ujuzi wake binafsi atakuwa tayari kumsaidia.

“Kichere nimefahamiana naye kwa muda mrefu sana sio mtu mgeni kwangu hivyo ninachoahidi ni kwamba akihitaji chochote kile kutoka kwangu binafsi au kutokana na ujuzi wangu wa miaka mitano nitampa, siku yoyote akipiga simu nitakuwepo kwaajili yake.

“Kichwani kwangu mimi ni mtu ambaye ninapenda nipande bamia nilisimamie liote liingie jikoni nile kwahiyo kwasababu hiyo katika miezi miwili iliyopita nilianza kuwekeza katika kilimo hivyo ni nachokifikiria sasa hivi nikae shambani kwangu na kupumzika kule lakini wakinihitaji watu wa mjini watanipigia simu nitakuja kufanya kazi zangu,” amesema Prof. Assad.

Katika hatua nyingine, Profesa Assad  amemshauri  CAG Kichere kuwa ni vyema akawajengea uwezo watumishi waliopo kuliko kuwafanyia mabadiliko kwa haraka kwa sababu hatua hiyo inaweza kuharibu utendaji wa taasisi.

“Taasisi haitakiwi kufanyiwa mabadiliko ya haraka muhimu ni kuwajengea uwezo waliopo, kinyume na hapo unaweza kuharibu taswira.

“Huwa naamini changes  zinaweza kutokea ila zitokee katika namna ambayo zimepangwa vizuri, si mwaminifu katika mfumo wa kutoa watu wote na kuweka new team usually lazima kutakuwa na mkanganyiko and can be very expensive kwa institutions kama hizi ambazo mtu anajifunza kwa miaka mingi.

“Kufikia level ya DAG lazima amefanya kazi na amekaa kwenye ofisi miaka 10 hadi 15, kwa hiyo experience yake ni muhimu kuihamishia kwa mtu mwingine, ukifanya immediate changes unaweza kupoteza ile instution memory,” amesema Profesa Assad


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger