Mratibu wa mradi wa ‘ Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii’ kutoka Shirika la Under The Same Sun, Grace Wabanhu akitambulisha mradi huo kwa wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino katika mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Under The Same Sun limetambulisha rasmi mradi wa ‘ Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)’ wenye lengo la kuwajengea uwezo wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino katika mkoa wa Shinyanga kuhusu ualbino ili wawe na uelewa wa kutosha na kupata ujasiri wa kuielimisha jamii juu ya hali ya ualbino.
Mradi huo umetambulishwa leo Jumatatu Novemba 18,2019 katika ukumbi wa Shinyanga Fairies Hotel Mjini Shinyanga wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu kuhusu elimu ya ualbino kwa na wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino 30 kutoka wilaya za mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa mradi wa ‘ Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii’ kutoka Shirika la Under The Same Sun, Grace Wabanhu alisema mradi huo wa miezi minne unaotekelezwa katika mkoa wa Shinyanga na Mwanza utafikia tamati mwezi Januari,2020.
“Lengo la mradi unaofadhiliwa na watu wa Canada ni kutoa elimu ya ualbino kwa wanawake hawa,tumechukua wanawake 30 kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga,Mwanza hivyo hivyo wanawake 30. Wanawake hawa watapata mafunzo ya uelewa juu ya ualbino na wao ndiyo watakuwa wakufunzi kuielimisha jamii”,alisema.
“Tunatarajia kwamba wanawake watakaojengewa uwezo watakuwa na uelewa wa kutosha juu ya hali ya ualbino na watakuwa na ujasiri wa kuielimisha jamii inayowazunguka kwa lengo la kuondoa unyanyapaa na ukatili dhidi yao na watoto wenye ualbino ili kuleta usawa kati ya watu wenye ualbino na wasio na ualbino”,aliongeza Wabanhu.
Alisema wameamua kuchagua kundi la wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino kutokana na kwamba kundi hilo limesahaulika lakini kwa kuzingatia kuwa akina mama hao ndiyo wanalea watoto na ni waathirika wakubwa wa vitendo vya unyanyapaa na ukatili na wamekuwa wakikimbiwa na waume zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye ualbino mkoa wa Shinyanga (TAS),Eunice Zabron alisema njia pekee ya kukomesha vitendo vya unyanyapaa na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino ni kutoa elimu ya kutosha kwa jamii.
Zabron ambaye pia Mwenyekiti wa Idara na Wanawake na Watoto katika Chama cha Watu wenye ualbino mkoa wa Shinyanga aliipongeza serikali kwa kuendelea kuwa bega kwa bega na watu wenye ualbino huku akibainisha kuwa vitendo vya unyanyapaa vimeendea kupungua kutokana na elimu inayotolewa na vyombo vya habari na wadau mbalimbali kuhusu ualbino.
Kwa upande wake,Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Lilian Kiyenze kwa niaba ya Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga aliwataka wanawake hao kutumia vizuri elimu watakayopatiwa kuhusu Ualbino ili wakawe chachu ya mabadiliko katika jamii.
ANGALIA PICHA
Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Lilian Kiyenze akizungumza kwa niaba ya Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga wakati Shirika la Under The Same Sun likitambulisha mradi wa ‘ Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)’ leo Jumatatu Novemba 18,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Lilian Kiyenze akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)’.
Mratibu wa mradi wa ‘ Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii’ kutoka Shirika la Under The Same Sun, Grace Wabanhu akitambulisha mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)’kwa wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino katika mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa mradi wa ‘ Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii’ Grace Wabanhu akielezea kuhusu mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI).
Grace Wabanhu akizungumza wakati akitambulisha mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)’
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye ualbino mkoa wa Shinyanga (TAS),Eunice Zabron akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI).
Wanawake wenye watoto wenye ualbino wakiwa ukumbini wakati mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI) ukitambulishwa.
Akina mama wakiteta jambo ukumbini.
Wanawake wenye ualbino wakiwa ukumbini wakati mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI) ukitambulishwa rasmi mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini wakati mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI) ukitambulishwa.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
0 comments:
Post a Comment