Monday, 18 November 2019

Marekani, Korea Kusini kusitisha Mazoezi Ya Kijeshi

...
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper amesema kwamba wamesitisha kwa muda usiojulikana mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Korea Kusini katika kile alichokitaja nia njema kuelekea Korea Kaskazini. 

Hatua hiyo inakuja hata baada ya Waziri wa Ulinzi wa Japan Taro Kono ambaye nchi yake imekuwa ikitishwa na majaribio ya mara kwa mara ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini kumuelezea Esper kwamba hakuna ambaye ana matumaini kuhusu kubadilisha hatua za Korea Kaskazini.

Matamshi hayo ya Kono yanaashiria kuzorota kwa mahusiano kati ya Marekani na washirika wake wa kimataifa, katika wakati wanapojaribu kuirejesha Korea Kaskazini kwenye mazungumzo ya kuachana na mipango yake nyuklia na makombora.

Ingawa katika tawala zilizopita Marekani iliyaita mazoezi  hayo kuwa ni muhimu lakini Rais Donald Trump ameyaita kuwa ni upotevu wa fedha na uchokozi dhidi ya Korea Kaskazini.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger