Friday, 8 November 2019

Kauli ya Waziri Jafo Baada Ya CHADEMA Kutangaza Kujitoa Uchaguzi Serikali za Mitaa

...
Baada  ya Chadema kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo amesema uamuzi huo unawanyima fursa wagombea wa chama hicho waliopitishwa, waliokata rufaa kupinga kuenguliwa.

Jana  jioni Alhamisi Novemba 7, 2019 mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema chama hicho kimejitoa na hakitashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwa ni kuhalalisha ubatili, akibainisha kuwa takribani asilimia 85 ya wagombea wao nchi nzima wameenguliwa.

Katika maelezo yake Jafo amesema; “Nimesikia kuwa Chama kimojawapo kimejitoa kwenye Uchaguzi, ninachoweza kusema ni kuwa hawajawatendea haki Wananchi wa chini kwa sababu baadhi yao walishateuliwa na wengine wameshawasilisha malalamiko yao kwenye Kamati za Rufaa na tayari baadhi ya Kamati za Rufaa zimeshaanza kutoa maamuzi juu ya rufaa hizo. 

"Mtazamo wangu maamuzi hayo yatawanyima haki na kuwadhulumu wananchi wa chini haki yao ya kugombea na kuongoza Serikali za Mitaa ambao baadhi yao wameshateuliwa na wengine wanasubrii rufaa zao”


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger