Waganga wa tiba asili wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa na ushirikiano katika kuwafichua waganga matapeli wanaotumia taaluma hiyo vibaya na kuwapeleka katika vyombo vya dola ili ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Kauli hiyo imetolewa na katibu taifa wa Umoja wa Waganga na wakunga wa tiba asili Tanzania(UWAWATA) Lucas Mlipu katika ziara yake wilayani humo kwa lengo la kutoa elimu kwa waganga dhidi ya kuendesha shughuli zao kwa udanganyifu.
Kwa upande wake, mkuu wa polisi wilayani Kahama Lutusyo Mwakyusa amesema waganga wa tiba asili wametakiwa kushirikiana na jeshi la polisi kwa kuwafichua waganga matapeli na kuwataka kuwa waaminifu wanapotibu wagonjwa na kuacha tamaa.
Nao waganga wa tiba asili wilayani humo wakizungumza na kahama fm kwa nyakati tofauti wameshukuru kupatiwa elimu hiyo ili kuwapa na wenzao ambao wapo huko vijijini ili kuepukana na waganga matapeli wanotumia taaluma hiyo kwa kuwadanganya wagonjwa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na wakunga wa tiba asili Tanzania(UWAWATA) wilayani kahama, Kulwa Said amesema lengo la kikao hicho ni kuzindua kampeni ya kuwapatia elimu elekezi wanganga wilayani humo ili kusaidia jamii kuwatambua baadhi ya waganga matapeli.
0 comments:
Post a Comment