Monday, 16 September 2019

Picha : TGNP MTANDAO YAENDESHA WARSHA KWA WAANDISHI WA HABARI JUU YA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UONGOZI

...
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi 

Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi amefungua warsha ya Waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa wanawake katika uongozi ili kuwajengea na kuwaongezea uelewa na uwezo waandishi hao wa habari kuripoti masuala ya kijinsia hasa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi.

Warsha hiyo ya siku tatu iliyofunguliwa leo Jumatatu Septemba 16,2019 inafanyika katika ukumbi wa TGNP Mtandao uliopo Mabibo Jijini Dar es salaam ikikutanisha waandishi wa habari 43 kutoka mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Tabora na Mara.

Akifungua warsha hiyo,Liundi amesema katika warsha hiyo inalenga kuweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti masuala ya kijinsia katika vyombo vya habari katika kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki wa wanawake na vijana katika uongozi.

"Waandishi wa habari mna nafasi kubwa sana ya kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi ikiwemo siasa,naamini kupitia warsha hii ya siku tatu mtakuwa chachu ya mabadiliko katika kuhamasisha wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi lakini pia katika utoaji maamuzi",amesema.
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akifungua warsha ya Waandishi wa habari 43 kutoka mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Tabora na Mara kuhusu ushiriki wa wanawake katika uongozi leo katika ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es salaam. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akifungua warsha ya Waandishi wa habari  kuhusu ushiriki wa wanawake katika uongozi leo katika ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akifungua warsha ya Waandishi wa habari  kuhusu ushiriki wa wanawake katika uongozi.
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akifungua warsha ya Waandishi wa habari  kuhusu ushiriki wa wanawake katika uongozi.
Afisa Habari wa TGNP Mtandao,Monica John akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Mwezeshaji Beatrice Ezekiel akitoa mada kuhusu dhana mbalimbali za Jinsia ikiwemo 'Fikra Mgando'.
Waandishi wa habari,Frank Mshana kutoka Shinyanga  na Happiness Severine kutoka Simiyu wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Warsha inaendelea.
Warsha inaendelea.
Washiriki wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger