Tuesday, 24 September 2019

Aliyekuwa Afisa Usalama Wa Shirika La Posta Atiwa mbaroni Kwa Tuhuma Za Kujihusisha Na Madawa Ya Kulevya

...
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya kwa kushirikiana na jeshi la polisi linamshikilia aliyekuwa Afisa Usalama wa Shirika la Posta Tanzania Bw.George Arsein Mwamgambe kwa tuhuma za kusafirisha madawa ya kulevya kwa njia ya Posta.

Taarifa hiyo imetolewa jana Septemba 23 na Kaimu kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji, ambapo amesema kuwa mwanaume huyo walimkamata kwa kushirikiana na jeshi la polisi na kwamba hapo awali aliwahi kutoweka kufuatia mahojiano yaliyokuwa yakiendelea dhidi yake.

''Mamlaka imemkamata George Mwangabe pamoja na wenzake sita wanaohusishwa na dawa za kulevya aina ya Heroin ambapo hadi sasa uchunguzi umekamilika na washtakiwa watafikishwa mahakamani'', amesema Kaimu Kamishina Kaji.

Kwa upande mwingine katika kipindi cha mwezi Septemba, Mamlaka hiyo imefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya Heroin zaidi ya kilo moja katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza pamoja na zaidi ya kilo 214 za vifurushi vya dawa za kulevya aina ya mirungi, zilizokuwa zikisafirishwa kwa njia ya Posta kutoka Arusha kwenda nchini Uingereza.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger