
Kuhusu Gamboshi/Gambosi
- Inasemekana Makao makuu ya uchawi Tanzania ni Kijiji Cha Gambushi,
- Kijiji cha Gambushi kipo wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu mpakani kabisa na wilaya ya Magu mkoani Mwanza,
- Umbali kutoka kijiji hiki kwenda Bariadi mjini ni Kilometa 60.
- Kijiji hiki kinavuma kwa uchawi kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla na ndipo jina la Ambushi lilipozaliwa kutokana na jina kamili la Gambushi,
- Kijiji hiki kuna imani kwamba usiku hung'aa na kuonekana kama Jiji la New York wakati hakuna hata nguzo moja ya Umeme,
- Tangu upatikane uhuru kijiji hiki hakija wahi kutembelewa na Kiongozi yeyote,
- Watu wa kijiji hiki wote huamini uchawi ndo kila kitu kwao,
- Huwezi kuingia kijiji hiki bila kuonana na wenyeji kwanza,
- Wachawi wote Tanzania huenda kuzuru hapo kama vile wakristo wanavyoenda Roma au waislamu wanavyoenda Makka,
- Ukifika wilaya ya Bariadi ukauliza nataka kwenda kijiji cha Gambushi lazima watakuuliza hili swali " Unakijua lakini kijiji hicho",
- Kijiji hiki kina miujiza mingi sana ni kawaida kabisa kukuta watu wa ajabu,paka anaongea kama binadamu na vibweka vya kila aina,
- Tangu kupata uhuru Mwenge haujawahi kufika huko.
0 comments:
Post a Comment