Thursday, 4 July 2019

WACHIMBAJI WAWILI WAFARIKI KWA KUFUKIWA NA KIFUSI CHA MGODI WA MWEMBE

...

Picha haihusiani na habari

Wachimbaji wawili wa Dhahabu katika kijiji cha Izumbi, Sangamba Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo katika Mgodi wa Mwembe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema, tukio hilo limetokea siku ya Julai 2, 2019 majira ya saa 10 jioni, ambapo wachimbaji hao walifariki baada ya kuangukiwa na kifusi kilichochanganyika na mawe hali iliyopelekea kukosa hewa.

''Wakati wanafanya shughuli hizo basi waliangukiwa na kifusi cha udongo mchanganyiko na mawe na kusababisha kifo chao baada ya kukosa hewa. Mwamba huo unamilikiwa na mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Mwembe Msemakweli, na sisi kama jeshi la polisi baada ya kupata taarifa hizo, tulifika eneo la tukio na kuthibitisha na marehemu walifariki wakati wanakimbizwa Zahanati'', amesema Kamanda Matei.

Aidha Kamanda Matei ametoa rai kwa wale wanaofanya shughuli za uchimbaji, akiwataka kuwa makini wakati wa kufanya shughuli zao, na kwamba shughuli ya kupanga mbao za kuzuia vifusi waifanye kabla hawajaingia ndani ya shimo badala ya kupanga wakiwa ndani ya shimo.

kamanda Matei amewataja waliofariki kuwa, ni Zakayo Muyunga na Ayoub Mpimbi wote wakazi wa Izumbi.
Chanzo - EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger