Monday, 8 July 2019

TFF Yasitisha Mkataba na Kocha Amunike Taifa Stars

...
Aliyekuwa kocha mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike, amefutwa kazi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ikiwa ni siku chache zimepita baada ya timu hiyo kutolewa hatua ya makundi kwenye fainali za AFCON.

Taarifa iliyotolewa ya TFF leo, imeeleza kuwa pande mbili zimefikia makubaliano ya kusitisha mkataba huo.

''Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” Emmanuel Amunike tumefikia makubaliano ya pamoja kusitisha mkataba baina yetu''.

Aidha TFF imeweka wazi kuwa itatangaza kocha wa muda atakaekiongoza Kikosi cha timu ya Taifa kwa mechi za CHAN.

Pia wamefafanua zaidi kuwa makocha wa muda watatangazwa baada ya Kamati ya Dharura ya Kamati ya Utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019.

Kwasasa shirikisho limebainisha kuwa mchakato wa kutafuta Kocha mpya umeanza mara moja.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger