Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imefanikiwa kumrejesha nyumbani aliyewahi kuwa mchezaji wake Ibrahim Ajibu Migomba ambaye ametambulishwa hii leo na klabu hiyo kupitia ukurasa wa Instagram.
Simba imejiwekea utaratibu wa kila siku jumatatu mpaka ijumaa saa saba kamili mchana kutambulisha wachezaji ambao imewasajili kwaajili ya msimu ujao.
Taarifa ya Simba ambayo imechapishwa katika ukurasa huo wa Instagram inasema kuwa
Ibrahim Ajib akisaini mkataba.
“Safari ya mtoto kuishi mbali na nyumbani imefikia ukingoni. Ibrahim Ajibu ameamua kufanya maamuzi sahihi ya kurudi nyumbani Msimbazi, ndio amerudi na amesaini mkataba wa miaka miwili kucheza na kuwapa furaha Wanasimba. Karibu nyumbani Ajibu”imesema taarifa hiyo.
0 comments:
Post a Comment