Sunday, 7 July 2019

SHIRIKA LA RELI TANZANIA TRC KUFUNGA NJIA ZA RELI KWA SAA 72 ILI KUKARABATI RELI YA KATI

...

Na Grace Semfuko,MAELEZO
Shirika la Reli Tanzania TRC limeanza kukarabati njia ya Reli ya kati ya kutoka Dar Es Salaam mpaka Isaka iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga takribani kilomita 970 ili kuimarisha reli hiyo yenye kiwango cha Mitagauge zoezi ambalo lilianza Juni mwaka huu na kutarajia kukamilika mwaka 2020.

Katika Utakabati huo Shirika hilo linatarajia kufunga njia za reli hiyo kwa saa 72 kwa wiki ikiwa ni sawa na siku tatu kwa Wiki kwa muda wa miezi mitano kuanzia Julai hadi Novemba 2019, zoezi zoezi ambalo  kukamilika kwake kutaingiza faida mara dufu ya usafiri huo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Masanja Kadogosa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam na kubainisha kuwa kukamilika kwa Reli hiyo kutaongeza mapato ya usafirishaji wa Reli kwa asilimia mia moja.

“Waandishi wa Habari na Watanzania kwa ujumla, TRC sasa tunakuja kuimarisha miundombinu yenu ya Reli, tunafanya hivi kwa kuwa tunafahamu mnahitaji huduma hizi, tunaomba mtuvumilie kwa siku ambazo tutafunga njia hizi”alisema Kadogosa.

Alisema kwa treni za kawaida za mjini (Cummuter Train) za kutoka Kamata kwenda Ubungo na Pugu zitafanya kazi siku za jumatatu hadi Ijumaa huku Treni za kawaida (Ordinary Train) za kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma, Mwanza na Mpanda zitafanya kazi siku za Jumatatu na Jumatano saa tisa alasiri tu na treni za Deluxe ya kutoka Dar kwenda Kigoma zitakuwepo siku ya Jumanne pekee.

Alibainisha kuwa ukarabati mwingine wa njia ya Reli kutoka Tanga kwenda  Arusha ulianza mapema mwaka huu ambapo njia hiyo itaanza kutumika mwezi Desemba mwaka huu.

“Ndugu zangu wa mikoa ya Kaskazini mtaanza kunufaika na usafiri wa treni ya Abiria kuanzia Desemba mwaka huu, yaani Sikukuu zaKrismas na Mwaka mpya mtaenda nyumbani na Treni ya Abiria ya TRCälisema Kadogosa.

Akizungumzia ujenzi wa Reli ya Standard Gauge inayoendelea kujengwa Nchini Kadogosa alisema kwa awamu ya kwanza kutoka Dar Es Salaam kwenda Morogoro ujenzi huo umefikia asilimia 56.
 


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger