Friday, 5 July 2019

Iran yamuita balozi wa Uingereza kuhusiana na kuakamatwa meli yake

...
Iran imemuita balozi wa Uingereza mjini Tehran kuhusiana na kile ilichosema ni kukamatwa leo kinyume cha sheria meli ya mafuta ya Iran katika kisiwa cha Gibraltar. 

Televisheni ya serikali ya Iran imemnukuu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni Abbas Mousavi akithibitisha habari hizo. 

Jeshi la wanamaji wa Uingereza lilikamata meli hiyo ya mafuta ikituhumiwa kwa kupeleka mafuta nchini Syria ikiwa ni hatua ya kukiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya. 

Kitendo hicho kinazusha hofu ya kuongeza mgogoro kati ya nchi za Magharibi na Iran. 

Waziri Kiongozi wa Gibraltar Fabian Picardo alisema katika taarifa kuwa wanaizuilia meli hiyo na shehena yake. 

Meli hiyo inasafiri kwa bendera ya Panama na inaaminika kuwa imebeba mafuta ya Iran.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger