Sunday, 16 June 2019

Picha : KIWOHEDE, AGAPE WAUNGANA NA SERIKALI, KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO AFRIKA DUNIANI MKOA WA SHINYANGA

...


Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Kahama.

Mashirika yasiyo ya kiserikali KIWOHEDE na AGAPE ACP, ambayo yanatekeleza miradi ya kupinga matukio ya ukatili dhidi ya watoto wadogo pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga, yameungana na Serikali ya mkoa wa Shinyanga kuadhimisha kilele cha siku ya mtoto wa Afrika Duniani.

Maadhimisho ya kilele ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani yamefanyika leo Juni 16, 2019 kimkoa wilayani Kahama, kwenye uwanja wa michezo wa Taifa ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Kahama,Mhe. Anamringi Macha, akimwakilisha mkuu wa mkoa,Mhe. Zainab Telack.



Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha,aliitaka jamii kuachana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ambapo aliwasisitiza wazazi kuacha tabia ya kuwafanyia vitendo vya kikatili watoto wao pamoja na kuwabagua kuwapatia elimu na kufikia hatua ya kuwaozesha ndoa za utotoni wanafunzi wa kike.

Alisema serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote atakayekamatwa akiwafanyia ukatili watoto.

Mhe. Macha alitumia fursa hiyo kuyapongeza mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani humo likiwamo KIWOHEDE na AGAPE, kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya ya kushirikiana na serikali kutatua changamoto mbalimbali ndani ya jamii.

Naye Mratibu wa mradi wa afya ya uzazi, ujinsia na haki za vijana wa Shirika la KIWOHEDE,Amos Juma  aliitaka jamii kuachana na vitendo vya kunyanyasa watoto wao pamoja na kuacha tabia ya kuendekeza mila na desturi kandamizi kwa kuwaozesha watoto na hatimaye kuzima ndoto zao.

Amesema katika mradi wao wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia na kutetea haki za vijana, ambao wanautekeleza kwenye kata ya Zongomela, wamekuwa wakikumbana na changamoto ya jamii kupenda kuendekeza mila na desturi zilizopitwa na wakati, na hivyo kuwapatia changamoto kubwa ya kumaliza kabisa ukatili kwa watoto licha ya kuupunguza kwa asilimia kubwa.

KIWOHDE kama wadau wakubwa wa kutetea haki za watoto, tunapenda kutumia fursa hii kwenye maadhimisho haya ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani, kuwataka wazazi waachane na mila kandamizi pamoja na kuwafanyia vitendo vya ukatili watoto wao, bali wawatekelezee mahitaji hayo pamoja na kuwapatia elimu bila ya kuwabagua ili wapate kutimiza ndoto zao,”alisema Amosi.

“Mradi huu tulianza kuutekeleza mwaka 2017 na unatarajiwa kuisha mwaka huu 2019, ambapo kipindi tunauanza kuutekeleza kwenye Kata ya Zongomela, kulikuwa na matukio mengi ya ukatili dhidi ya watoto zikiwamo na mimba za wanafunzi, lakini kwa sasa matukio hayo yamepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na awali,”aliongeza.

Naye Afisa mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto kutoka Shirika la AGAPE mkoani Shinyanga Felix Ngaiza, ambao wana utekeleza wilayani Kishapu katika kata za Itilima, Kishapu na Bunambiu, aliitaka jamii kuachana na vitendo vya kikatili pamoja na kuwaozesha wanafunzi ndoa za utotoni.

Ngaiza alisema AGAPE itaendelea kushirikiana na serikali na jamii ili kuhakikisha haki za watoto na wanawake zinalindwa katika jamii.

Aidha kauli mbiu ya mwaka 2019 ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani, inasema “ Mtoto ni Msingi wa Taifa Endelevu, Tumtunze, Tumlinde na Kumwendeleza.”


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Kaham,Mhe. Anamringi Macha akipinga vikali vitendo vya wazazi kuwafanyia ukatili watoto pamoja na kuwaozesha ndoa za utotoni ikiwemo na wanaume kuwa patia mimba za utotoni, na kutangaza atakayekamatwa serikali itamchukulia hatua kali za kisheria. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mkuu wa wilaya ya Kahama,Mhe. Anamringi Macha, akiwataka wanafunzi wilayani humo kuwa wanatoa taarifa juu ya matukio ya kikatili ambayo wanafanyiwa, pamoja na kuacha mapenzi katika umri mdogo ili wapate kutimiza ndoto zao, sanjari na kuwakumbusha wazazi wao kuwa tekelezea haki zao.


Awali vijana kutoka Shirika la KIWOHEDE wakiongoza maandamano ya wanafunzi kutoka katika halmashauri ya Kahama Mji kuelekea kwenye uwanja wa taifa wilayani Kahama kwa ajili ya kuadhimisha kilele siku ya mtoto wa Afrika Duniani kimkoa wilayani Kahama.

Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Kahama Mji Mary Chima, akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani kimkoa wilayani humo.

Wanafunzi wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani kimkoa wilayani Kahama, wakisikiliza nasaha kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama,Mhe. Anamringi Macha namna ya kudai haki kutoka kwa wazazi wao ili wapate kutimiza ndoto zao.

Wanafunzi wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani kimkoa wilayani Kahama.

Maadhimisho ya kilele cha siku ya mtoto wa Afrika Dunia mkoani Shinyanga yakiendelea wilayani Kahama.

Wanafunzi wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani kimkoa wilayani Kahama.

Wanafunzi wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani kimkoa wilayani Kahama.

Awali mkuu huyo wa wilaya ya Kahama Kabla ya kutoa hotuba yake kwenye maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani, alianza kutembelea mabanda ya wadau wa maendeleo.Pichani ni Mhe. Macha akiwa kwenye banda la Shirika la KIWOHEDE akisikiliza kazi ambazo wanazifanya za kutetea haki za watoto pamoja na kuwapatia vijana mafunzo ya ujasiriamali.

Mkuu wa wilaya ya Kahama,Mhe. Anamringi Macha, akiangalia nguo za Batiki ambazo hutengenezwa na vijana wa kike kutoka Shirika la KIWOHEDE wilayani Kahama.

Katibu wa Klabu ya Tuseme kutoka shule ya Sekondari Isunuka wilayani Kahama Neema Steven akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama,Mhe. Anamringi Macha namna Shirika la KIWOHEDE lilivyowasaidia kuwapatia elimu ya afya ya uzazi na ujinsia na hatimaye kujitambua na kupunguza tatizo la mimba za wanafunzi shuleni hapo.

Mratibu wa elimu ya afya ya uzazi,ujinsia na haki za vijana kutoka Shirika la KIWOHEDE Amosi Juma akimwelezea mkuu wa wilaya ya Kahama,Mhe. Anamringi Macha namna wanavyofanya kazi wilayani humo ya kutatua changamoto mbalimbali ndani ya jamii ikiwamo kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.

Mratibu wa elimu ya afya ya uzazi,ujinsia na haki za vijana kutoka Shirika la KIWOHEDE wilayani Kahama Amosi Juma, akieleza namnashirika hilo linavyowasaidia vijana wa kike kwa kuwajengea uwezo wa kufanya shughuli za ujasiriamali ikiwamo kutengeneza batiki, na kushona nguo.

Mkuu wa wilaya ya Kahama,Mhe. Anamringi Macha akiwa kwenye banda la Shirika la AGAPE, akisikiliza kazi ambazo wanazifanya za kutetea haki za wanawake, watoto kwa kupinga matukio ya ukatili pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.

Afisa mradi wa Sauti ya mwanamke na mtoto kutoka Shirika la AGAPE Felix Ngaiza, akimwelezea mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Anamringi Macha namna mradi huo unavyofanya kazi, ambao umelenga kutokomeza matukio ya ukatili pamoja na mimba na ndoa za utotoni na kubaki kuwa historia, ambapo mradi huo unatekelezwa wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akiwa kwenye Banda la Shirika la TVMC, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa miradi Adriana Leonard namna shirika hilo linavyofanya kazi.

Vijana kutoka Shirika la KIWOHEDE wilayani Kahama wakitoa burudani kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto Afrika Duniani kikoa wilayani Kahama.

Wanafunzi kutoka Compassion wilayani Kahama nao wakitoa burudani kwenye kilele cha maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani kimkoa wilayani Kahama.

Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Mwendakulima wilayani Kahama nao wakitoa burudani kwenye kilele cha maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani kimkoa wilayani Kahama.

Afisa Maendeleo ya jamii mkoani Shinyanga Glory Mbia (kulia) akiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani kimkoa mkoani Shinyanga, ambapo nchini Tanzania yalianza kuadhimishwa mwaka 1991, kutokana na vifo vya watoto vilivyotokea huko nchini Afrika kusini mwaka 1976 wakati wakidai haki zao.

Burudani zikiendelea kutolewa kwenye kilele cha maadhimisho hayo ya mtoto wa Afrika Duniani kimkoa wilayani Kahama, ambapo mbali na nyimbo pia kulikuwa na maagizo yenye jumbe mbalimbali za kutoa mafundisho namna ya malezi bora kwa watoto.

Vijana kutoka Shirika la KIWOHEDE wilayani Kahama wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kuadhimisha kilele cha siku ya mtoto wa Afrika Duniani kimkoa wilayani Kahama.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger