Monday, 17 June 2019

Mahakama Yaamuru Wema Sepetu Aende Gerezani Siku 7

...
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemuamuru Msanii Wema Sepetu kwenda gerezani siku saba mpaka Juni 24  akisubiria uamuzi wa mahakama wa kumfutia dhamana. 

Nyota huyo wa filamu anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono mitandaoni kupitia simu yake ya kiganjani.

Uamuzi huo wa Mahakama umefikiwa leo Juni 17,  mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wakati mshtakiwa huyo alipofikishwa mbele yake.

Wakili wa Serikali Glory Mwenda amedai mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa hapo baada ya mahakama wiki iliyopita kutoa hati  ya kumkamata Wema kwa kosa la kuruka dhamana.

Hakimu Kasonde alimtaka Wema kujieleza kwanini asifutiwe dhamana kwa kushindwa kufika mahakamani kwa tarehe mbili tofauti.

Akijieleza Wema alidai Mei 14 mwaka huu hakufika sababu alikuwa safarini mkoani  Morogoro na Juni 11 mwaka huu aliumwa akashindwa kupandisha mahakamani.

Mshtakiwa aliomba msamaha na Wakili wa Serikali, Mwenda aliomba Mahakama impe onyo mshtakiwa ili asirudie kufanya kitendo hicho chenye usumbufu.

Hakimu Maira alisema kasikia hoja zilizowasilishwa na atapitia kiapo cha mshtakiwa kisha atatoa uamuzi Juni 24 mwaka huu na akaamuru katika kipindi cha kusubiri uamuzi mshtakiwa akae rumande.

Wema anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa hazina maudhui.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger