Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman amejiunga na Mabingwa wa nchi ya Tanzania kwa mkataba wa mwaka mmoja, leo.
Simba imeamua kujiimarisha zaidi katika sehemu ya kiungo cha ukabaji kwa kuvuka mipaka hadi nchini Sudan ambako imemsajili kiungo Bora mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu ya Sudan.
Huyo ni mchezaji wa timu ya taifa ya Sudan tangu akiwa na miaka 17 akitokea kwa mabingwa mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu ya Sudan klabu ya Al Hilal.
0 comments:
Post a Comment