Saturday, 22 June 2019

ASKARI WA JWTZ AGONGA KINGO YA BARABARA NA KUSABABISHA KIFO CHA BINTI USIKU SHINYANGA MJINI

...

Picha haihusiani na habari hapa chini

Binti aitwaye Nadia Rajab (18) mkazi wa Kambarage Mjini Shinyanga amefariki dunia baada ya pikipiki aliyokuwa amepanda ikiendeshwa na Othuman Hassan (30) askari wa JWTZ, mkazi wa Old Shinyanga kuacha njia na kugonga kingo ya barabara. 

Kwa Mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP,Richard Abwao ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Juni 22,2019 majira ya saa tisa na dakika 40 alfajiri katika barabara ya Uhuru, maeneo ya Total Petrol Station kata ya Shinyanga Mjini, Manispaa na Mkoa wa Shinyanga. 

“Pikipiki yenye namba za usajili MC. 402 BYN aina ya SANLG iliyokuwa ikiendeshwa na Hassan ambaye ni askari wa JWTZ, mkazi wa Old Shinyanga iliacha njia na kugonga kingo ya barabara na kusababisha kifo kwa abiria wake aliyekuwa amembeba kwenye pikipiki hiyo aitwaye Nadia Rajab”,amesema Kamanda Abwao. 

Kamanda Abwao amekitaja chanzo cha tukio hilo ni uzembe wa dereva kuendesha pikipiki akiwa amelewa na tayari dereva amekamatwa na pikipiki husika ipo kituoni. 

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger