Monday, 18 March 2019

ZITTO ATINGA OFISI ZA CUF, AJIFUNGIA NA MAALIM SEIF

...
Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo leo tarehe 18 Machi 2019 amefika katika Ofisi ya Wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) Magomeni jijini Dar es Salaam kuzungumza na Maalim Seif Shariff Hamad.

Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo alifika ofisini hapo muda mfupi baada ya Maalim Seif, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF kutangaza kujiunga na ACT-Wazalendo.

Kufika kwa Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini kulipokewa kwa shangwe na baadhia ya viongozi waliokuwa wa CUF na wanaomuunga mkono Maalim Seif.

“ACT-Wazalendoooo, ACT-Wazalendoo” ndio maneno yaliyokuwa yakitamkwa na viongozi hao wakati wakimpokea Zitto ambaye baada ya kufika, alipelekwa moja kwa moja chumba alichokuwemo Maalim Seif.

Humo ndani Zitto na Maalim Seif walitete kwa dakika kadhaa na kisha Zitto kutoka na kupanda gari lake kisha kutokomea. Haijaelezwa Zitto na Maalim Seif walizungumza nini.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger