Saturday, 30 March 2019

Picha : SHIRIKA LA AGPAHI LATOA MAFUNZO YA SAIKOLOJIA KWA WATUMISHI WA AFYA MWANZA

...

Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kutoka Vituo vya Afya mkoani Mwanza, yanayolenga kuwajengea
uwezo katika kutoa msaada na huduma za kisaikolojia kwa watoto na vijana wanaoishi na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Mafunzo hayo ya siku tano yalianza jumatatu Machi 25, 2019 hadi Ijumaa Machi 30, 2019 katika ukumbi wa “Isamilo Lodge” Jijini Mwanza ambapo yamewashirikisha wataalam wa afya zaidi ya 60 kutoka Halmashauri mbalimbali mkoani Mwanza ikiwemo Nyamagana, Ilemela, Misungwi, Magu, Ukerewe na Buchosa.

Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona amesema mafunzo hayo yatawasaidia watoa huduma za afya katika vituo vya tiba na matunzo kutambua namna bora ya kuwahudumia wateja wao hususani watoto na vijana.

Amesema mafunzo hayo yatawasaidia pia kuwatambua watoto na vijana wenye changamoto kisaiklojia na namna ya kuwasaidia huku wakizingatia upatikanaji wa huduma bora na rafiki kwa wateja kupitia mbinu mbalimbali ikiwemo michezo.

“Tunatarajia pia wataenda kuanzisha vikundi vya akina mama wanaoishi na maambukizi ya VVU ambao wako kwenye kitengo cha kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ili nao waweze kujifunza kupitia uzoefu wao huku vikundi vilivyopo
vikiimarishwa zaidi”,amesema Yona.

Baadhi yawashiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo walikuwa wakikumbana na changamoto ya kutambua mazingira halisi yanayowakabili watoto na vijana kupitia klabu zao.

Shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia taasisi ya Centres for Disease Control (CDC), linashirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutekeleza afua mbalimbali za kupambana na
maambukizi ya VVU pamoja na kuwahudumia watu wanaoishi na maambukizi hayo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mmoja wa Wawezeshaji, Margaret Safe kutoka Kibaha mkoani Pwani akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji, Margaret Safe akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakimsikiliza Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona.
Mwezeshaji, Dkt. Nikodemas Kikoti akiendelea kutoa mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakimsikiliza Mwezeshaji, Dkt. Nikodemas Kikoti kutoka mkoani Iringa.
Wataalam wa afya walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia mada kwa umakini.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
Timu ya wakufunzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo pia walipewa mtihani na hapa wakiwa kwenye chumba cha mtihani ili kupima uelewa wa kile walichofundishwa.
Washiriki wakijibu mtihani kuhusu walichofundishwa.
Baada ya mafunzo ya nadharia darasani yaliyofanyika Isamilo Lodge, washiriki walielekea Lesa Garden kukutana na baadhi ya watoto na vijana kutoka klabu za elimu na makuzi kwa ajili ya kucheza na kufurahi pamoja ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwasili Lesa Garden iliyopo Luchelele Jijini Mwanza.
Mafunzo kwa vitendo kupitia michezo.
Inaelezwa vijana hujifunza na kuelewa vyema kupitia michezo na hapa michezo imepamba moto.
Michezo mbalimbali ikiendela.
Mafunzo kwa vitendo kupitia michezo.
Washiriki wa mafunzo wakifurahi pamoja na vijana.
Michezo ikiendelea Lesa Garden.

Watoa huduma za afya wamehimizwa kutumia michezo kufikisha elimu kwa watoto na vijana.
Inaelezwa michezo husaidia watoto na vijana kuelewa vyema yale wanayofundishwa hivyo watoa huduma za afya wamehimizwa kutumia michezo pia kuwaelimisha vijana na watoto.
Washiriki wakifurahia pamoja na vijana.
Pia kulikuwa na burudani ya muziki ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo ambapo husaidia watoto na vijana kuwa huru kwa watoa huduma za afya.
Burudani ya muziki.
Washiriki wa mafunzo wakifurahia muziki pamoja na watoto/ vijana.
Michezo na burudani ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger