Wakati wachezaji wakiendelea na mazoezi, nje ya uwanja hali ni tofauti baada ya viongozi walioambatana na Simba kushindwa kuvumilia hali ya mashabiki wa Stand United jinsi wanavyoshangilia.
Mvutano baina ya wapinzani hao umechukua takribani dakika sita huku viongozi wa Simba wakiwafuata jukwaani mashabiki wa Stand United wakiwataka watoke uwanjani, jambo lililozua vurugu na baadaye Simba kutulia.
Mashabiki wa Stand United wameonekana kukomaa, huku wakidai kuwa hapa ni nyumbani kwao hivyo si rahisi kutokana uwanjani hapo na kuanza kupiga ngoma wakiimba kuwa wanaroga mechi.
Hadi sasa tayari Simba imeshafanya mazoezi mawili tofauti, ikiwa kukimbia kwa kuzunguka uwanja, kupigiana vichwa na kufunga na sasa wanasikiliza maelekezo ya Kocha wao, Patrick Aussems kujua programu inayofuata.
Na Saddam Sadick - Mwanaspoti
0 comments:
Post a Comment