Sunday, 3 March 2019

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI

...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Machi, 2019 amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua Balozi Dkt. Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mahiga alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kabla ya uteuzi huo Prof. Kabudi alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger