Waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa, ametangaza kurejea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM). Lowassa aliondoka CCM katikati ya mwaka 2015, kufuatia chama hicho “kumtosa katika kinyang’anyiro cha urais.”
Taarifa zinasema, kurejea kwa mwanasiasa huyo kwenye chama tawala, akitoka Chadema 'Akileft' kunatokana na shinikizo kutoka ndani ya familia yake na kile kinachoitwa, “kufungwa kwa njia yake ya kutaka kuwa mgombea tena wa urais kupitia Chadema.”
Ingawa upinzani haujataja mgombea wake, lakini anayepewa nafasi kubwa ya kugombea nafasi hiyo, ni Tundu Lissu, mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni.
Kinachotajwa kuwa shinikizo la familia, taarifa zinasema, linatokana na kesi ya jinai inayomkabili mmoja wa watoto wake, Sioi Solomon.
Sioi mbaye aliyekuwa mwanasheria wa benki ya Stanbic, tawi la Tanzania na wenzake wengine watatu, wanashitakiwa kwa makosa kadhaa, ikiwamo kula njama na kujipatia kwa udanganyifu, kughushi, utakatishaji wa fedha haramu.
Washitakiwa wengine, ni aliyepata kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na mwenyekiti wa kampuni ya Enterprise Growth Market Advisors Ltd (EGMA), Harry Kitilya; aliyekuwa mkuu wa idara ya ushirikiano na uwekezaji wa benki hiyo, Shose Mori Sinare na mwanasheria wa benki, Sioi Graham Solomon.
Washitakiwa wote wako gerezani tokea 1 Aprili 2016. Lowassa ameripotiwa akisema, alikutana na rais Magufuli na kumuomba kumsaidia kumtoa Sioi, ombi ambalo halikuwa limetekelezwa hadi anapotangaza kuondoka upinzani.
Lowassa ambaye alikuwa mpinzani mkuu wa Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu uliyopita, aliondoka CCM na kujiunga na Chadema, kupitia mkutano wake na waandishi wa habari wa tarehe 28 Julai 2015, katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Via Mwanahalisi Online
0 comments:
Post a Comment