Wednesday, 20 March 2019

BALOZI WA ZAMBIA NCHINI KENYA AFARIKI DUNIA

...


Balozi wa Zambia nchini Kenya Brenda Muntemba-Sichilembe, amefariki dunia jijini Nairobi baada ya kupata ajali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Macharia Kamau, amesema leo Jumatano Machi 20, 2019 kwamba balozi huyo alipoteza maisha baada ya kupata ajali ya gari barabara ya Machakos.

Amesema Mutemba (49), alipoteza maisha akipatiwa matibabu Hospitali ya Nairobi baada ya ajali iliyotokea wiki tatu zilizopita.

Kamau amesema balozi huyo alipata ajali Februari 26, 2019 eneo la Lukenya barabara ya Mombasa baada ya gari lake kugongana na gari kubwa la mizigo.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger