Saturday, 9 March 2019

AZANIA BANK YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUUNGANA NA WANAWAKE KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD

...

Wafanyakazi wanawake wa Azania Bank watoa zawadi na misaada mbalimbali kwa wanawake wenzao wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kama sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Meneja Mwandamizi wa Uendeshaji wa Azania Bank, Jane Chinamo akizungumza na wanahabari baada ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo kutoa zawadi na misaada mbalimbali kwa wanawake wenzao wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kama sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

***

Dar es Salaam, 9 Machi 2019 : Wafanyakazi wanawake wa Azania Bank leo wameungana na wanawake wenzao wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kama sehemu ya kuonyesha upendo na mshikamano katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2019.

 Ziara ya Wanawake wa Azania Bank katika wodi za wanawake wanaopatiwa matibabu katikaa taasisi hii imelenga kuwapa moyo wagonjwa na kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya kujikimu
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger