Jana mchana askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima amekamatwa Airport wakati akitua toka Nje ya nchi alikoenda kwa matibabu.
Duru za habari zinanyetisha kuwa Askofu Gwajima alishuka na
ndege ya Kenya Airways iliyokuwa inatoka Nairobi kuja Dar ambapo baada
ya kushuka alitaka kuunganisha na chopa yake kuingia mjini kupitia Sea
Cliff.
Mpaka sasa Askofu yupo chini ya ulinzi na wafuasi wake na
wasaidizi wake wamethibitisha kuwa walikuwa na taarifa za kuja kwa
Askofu wao leo na ndege ya Kenya Airways lakini hawajamuona,na habari
walizozipata ni kuwa mara baada ya kushuka vyomba vya Usalama
vilimkamata sbb walikuwa wakimtafuta kwa muda mrefu.
Waumini wake na wasaidizi wake wanaendelea kufuatilia
kujuwa kiongozi wao anashikiliwa katika kituo kipi cha polisi.Hizi
habari zimezua "taharuki" kanisani kwake na waumini wapo katika
makundimakundi kujadili hatima ya Askofu wao
0 comments:
Post a Comment