UCHAGUZI 2015: Matokeo ya uchaguzi ngazi ya Rais yataanza kutangazwa kwa awamu ya kwanza saa tatu asubuhi, saa sita mchana, saa tisa na saa 12 jioni.
UCHAGUZI 2015: Wagombea urais wa vyama vya CCM na Chadema wanachuana vikali kwa mujibu wa matokeo ya awali yanayotangazwa kwenye vituo mbalimbali nchini
MATOKEO URAIS Z’BAR: Kwa mujibu wa NEC, Dk Shein (CCM) ameongoza katika jimbo la Kiembesamaki kwa kura 4,413 dhidi ya 2,986 za Maalim Seif (CUF)
MATOKEO URAIS Z’BAR: Hadi sasa ZEC imetangaza matokeo ya urais katika majimbo ya Fuoni na Kiembesamaki na Shein (CCM) anaongoza dhidi ya Maalim Seif (CUF)
MATOKEO URAIS Z’BAR: ZEC yatangaza kuwa Jimbo la Fuoni; Dk Shein (CCM) amepata kura 889 wakati Maalim Seif (CUF) akiwa na kura 429. Waliojiandikisha kupiga kura jimbo katika jimbo hilo ni 1,822, waliopiga kura ni 1,397.
CHADEMA: Imethibitika kuwa tulichokibashiri kimetokea. Hivyo tuna haki ya kulinda kura zetu.
CHADEMA: Dosari za uchaguzi Katavi, Kimara na Pemba zinadhihirisha kuwa uchaguzi huu si huru na haki
ARUMERU: Msimamizi mkuu wa kituo cha Arumeru Magharibi, Fidelis Lumato amesema kuwa wanashukuru wamemaliza uchaguzi salama bila vurugu hivyo wanaomba wananchi waendelee hivyo hadi kesho asubuhi atakapotangaza matokeo ya jumla.
MUSOMA: Polisi watumia mabomu ya machozi kutawanya wananchi wanaovunja kituo cha kuhesabia kura cha Kigera, Musoma Mjini wakipinga matokeo yanayotangazwa
IFAKARA: Polisi wapiga mabomu ya machozi baada ya vijana kufanya fujo kwa kurusha mawe juu ya majengo ya shule ya msingi Mhola.
MVOMERO: Wasimamizi katika kituo cha shule ya msingi Wami Sokoine wakitumia simu za tochi na karabai kwa ajili ya uhesabuji kura. KJusoma zaidi bofya
TUNDUMA: Mawakala Jimbo la Tunduma wanyang’anywa simu na wasimamizi baada ya kubainika wakirusha matokeo kwa wenzao nje. Na kutokana na hali hiyo wananchi wameanza kukusanyika kwa wingi jirani na vituo vya kuhesabia kura huku wakiimba nyimbo za vyama vyao.
ARUMERU: Kata ya Maivo kituo cha sokoni Jimbo la Arumeru watu bado wako kwenye foleni wanapiga kura na hii ni baada ya majina zaidi ya 200 kukosekana kwenye orodha ya wapiga kura.
Msimamizi wa kituo cha skuli ya Mtambile, jimbo la Mtambile, mkoa wa Kusini Pemba, Hafidhi Said Ali akionyesha tochi itakayotumika usiku wa kuhesabu kura kituoni hapo.
AWE: Zoezi la kuhesabu kura bado linaendelea katika vituo mbalimbali vya Jimbo la Kawe.Katika kituo cha Bunju A, zoezi la kuhesabu kura za urais lilirudiwa baada ya wakala wa CCM kutoridhishwa na matokeo ya mgombea wake.
Zoezi la kuhesabu kura linaendelea kituo cha Uwanja wa soko Mageuzi Jimbo la Shinyanga mjini.
KIGOMA: Kigoma Kusini hali ni shwari, watu wapo wajumbani wanasubiri matokeo, hata baa hazina watu mji umetulia.
KARATU: Karatu waanza kuhesabu kura katika madarasa ya shule hakuna umeme wanatumia tochi.
SERENGETI: Zoezi la kuhesabu kura Jimbo la Serengeti linaendelea, shamrashamra baadhi ya mitaa ikianza licha ya mvua kubwa inayonyesha.
LINDI: Mkazi wa kijiji cha Kiangara wilaaya ya Liwale mkoani Lindi Abreheman Mkopora anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kutaka kujiandikisha mara mbili.
NYAMAGANA: Kituo cha shule ya msingi Mbugani Jimbo la Nyamagana kuna vijana wanalinda kura
Baadhi ya wakazi wa Kinyerezi wakimhoji askari Magereza katika kituo cha shule ya msingi Mount Pleasant baada ya kuona gari ndogo mabayo imeelezwa kuwa ni ya mlinzi inaingizwa ndani ya kituo hicho wakati kura zinahesabiwa ndani. Waliingia ndani na kupekua gari hilo.
TEMBONI: Kituo cha shule ya msingi Temboni hadi sasa watu zaidi ya 400 hawajapiga kura majina yao hayaonekani kwenye daftari, zoezi limesitishwa watu wameambiwa watawanyike wamegoma.
TUNDUMA: Wananchi Jimbo la Tunduma wamenza kusimama kando kando mwa vituo vya kuhesabia kura na kila gari linalopita jirani na vituo wanazuia na kulirudisha lilikotoka. Wanasema hawamuamini mtu yeyote anayekatiza eneo hilo.
Wananchi wa kata ya Uwanjani wakiwa kwenye uwanja wa Moira wa shule ya msingi Tunduma wakisubiria matokeo, polisi wamewaambia wakusanyike hapo baada ya kuona wanasogea na kujikusanya jirani na vituo vya kupigia kura.
MOSHI: Gari la mmoja wa makampeni meneja wa mgombea ubunge Jimbo la Moshi vijijini (CCM), Dk Cyrill Chami, limeshambuliwa na kuharibiwa vibaya na wananchi wakilishuku kuwa na kura bandia.
MWANZA: Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Tito Mahinya anasema kuanzia saa 6:00 usiku wataanza kutoa matokeo ya jumla ya udiwani Jimbo la Nyamagana.
MWANZA: Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Tito Mahinya anasema kuanzia saa 6:00 usiku wataanza kutoa matokeo ya jumla ya udiwani Jimbo la Nyamagana.
LULINDI: Jimbo la Lulindi wananchi wameshindwa kupiga kura ya nafasi ya ubunge hivyo uchaguzi wa nafasi hiyo umeahirishwa, ni baada ya kukosewa majina ya mgombea wa CUF katika wa CUF katika karatasi ya kupigia kura.
0 comments:
Post a Comment