Brighton Masalu
MWANAMAMA na ‘mtoto wa mjini’, Lungi Maulanga ameibiwa baadhi ya vitu vya ndani wakati akiwa katika matembezi ya usiku.
Akizungumza na gazeti hili, Jumatano
wiki hii, mmoja wa marafiki ‘changu ni chako’ wa msanii huyo ambaye
hakutaka jina lake ‘lichorwe’ gazetini, alisema tukio hilo la hasara
lilitokea usiku wa Jumanne nyumbani kwa Lungi Magomeni jijini Dar wakati
akiwa kwenye ‘kujirusha’.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi
wetu alimtafuta Lungi ambaye alikuwa na haya ya kusema “Ni kweli
nimeibiwa vitu kadhaa ikiwemo tv na deki, ukweli nimechoka sasa sababu
hii siyo mara ya kwanza kuibiwa hapa ndani, najiandaa kuhama.”
0 comments:
Post a Comment