Saturday, 4 July 2015

MAAJABU AJALI YA BASI KUGONGA TRENI

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOYMAAJABU AJALI YA BASI KUGONGA TRENI
NI maajabu ya Mungu! Nyuma ya tukio la ajali ya
basi kugona treni iliyotokea hivi karibuni, yamebainika maajabu ya aina yake baada ya mtoto Alhaji Mdoe aliyekuwa amepakatwa na mama yake kukutwa akiwa hai wakati mama yake akiwa amefariki dunia.

Ajali hiyo ilitokea Jumatano asubuhi eneo la Kibaoni Wilaya ya Kilosa mkoani hapa, ambapo mama aliyekuwa amempakata mtoto huyo alikuwa miongoni mwa watu watano waliofariki dunia katika ajali hiyo huku ndugu zake wengine wakijeruhiwa vibaya.

Akizungumzia tukio hilo, baba wa mtoto huyo, Mdoe Ally, mkazi wa Kijiji cha Tingiga, Kilosa, alisema kwenye basi hilo alikuwa yeye na familia yake akimpeleka mkewe Amina Mohamed kwa mganga Mlandizi Mkoa wa Pwani aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya miguu na mikono.

“Nilikuwa safarini kwenda Mlandizi kumpeleka mke wangu kwa mganga kwa bahati mbaya wote tumejeruhiwa isipokuwa mtoto wangu mdogo Alhaji ambaye alibebwa na mama yake (mkewe), Husna na Salehe (wanaye) wamevunjika miguu na mama yao ameumia kichwani,” alisema Mdoe ambaye kwa wakati huo (juzi), alifichwa kama mkewe alifariki kwenye ajali hiyo.

Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Wilaya Kilosa, Dk. Dikson Masale amethibitisha kupokea maiti 5 na majeruhi 31.

“Ni kweli tumepokea majeruhi 31 kati yao wanaume 10, wanawake 15 na watoto 6 na maiti 5 ambazo zimetambuliwa kwa majina ya Saleh Gomba, Amina Mohamed, Mwajili Mzange, Surati Mwajili na dereva wa basi hilo, Masoud Cholo,” alisema Dk. Masale.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Mussa Malambo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha gari lenye namba za usajili TB37 CMT Isuzu Coaster lililogonga treni.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger