Mwandishi Wetu
MIKOSI mikosi! Hakuna neno
lingine sahihi zaidi ya hilo kufuatia watoto wawili wa aliyewahi kuwa
waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi katika serikali ya awamu
ya tatu, Tatu Ntimizi, Mussa na nduguye, Said Ntimizi kwa nyakati
zinazokaribiana kukumbwa na madai ya uhalifu yaliyowasababishia
kufikishwa polisi na mahakamani.
Mussa ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Uyui, Tabora, Juni 1, mwaka huu alipandishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora kwa madai ya kumlawiti kijana
mmoja muuza chipsi (jina linahifadhiwa), mkazi wa manispaa hiyo.
Mussa alifikishwa mbele ya Hakimu
Jocktan Rushwera na kusomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Juma
Masanja ambaye alidai, mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo nyumbani kwake
eneo la Bachu, Tabora.
Wakili Masanja aliieleza mahakama kuwa,
Mussa alimrubuni kijana huyo kwa kumnunulia bia mbili kwenye baa moja ya
mjini hapo na baada ya kulewa na kupoteza fahamu, alimpeleka nyumbani
kwake eneo la Bachu na kumfanyia kitendo hicho.
Hata hivyo, mshtakiwa alikana kutenda
kosa hilo na kesi yake ikapigwa kalenda hadi Juni 30, mwaka huu ambapo
ilitarajiwa kusikilizwa tena.
Wakati kesi ya kaka mtu, yaani Mussa
ilitarajiwa kusikilizwa Juni 30, Said (34) yeye, Juni hiyohiyo
alishikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni jijini Dar kufuatia
kifo cha aliyekuwa mmiliki wa Shule ya Awali na Msingi ya Mtakatifu Zion
iliyopo Bahari Beach, Dar, Annah Mizighi Mwambili (47) ambaye Desemba,
mwaka jana aliuawa na mwili wake kutupwa ndani ya shule yake hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar, Jumatatu iliyopita, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Kamishina Suleiman Kova, alisema Said anashikiliwa na wenzake
wawili, Daniel Mkilindi (25) na Erick Mziray (40) kwa madai ya kuhusika
na mauaji hayo.
Habari ya Said, ukiacha vyombo vingine vya habari, pia iliandikwa kwenye gazeti ndugu na hili, Uwazi toleo la Jumanne iliyopita.
Baada ya habari hiyo kutoka, baadhi ya
wasomaji wa Gazeti la Uwazi walipiga simu kwenye chumba cha habari na
kusema ni dhahiri familia ya waziri Ntimizi imekumbwa na mikosi.
“Jamani, nimeisoma kwenye Gazeti la
Uwazi hii habari ya mtoto wa Tatu Ntimizi, Said. Mimi ninavyojua huyu
Said na Mussa aliyefikishwa Mahakama ya Tabora hivi karibuni akidaiwa
kumlawiti muuza chipsi ni ndugu. Tena najua huyu Said alikuwa kwenye
mkakati wa kugombea ubunge Jimbo la Igalula, Tabora.
“Hii ni mikosi jamani! Hata kama
mahakama itawakuta hawana hatia lakini ni mikosi kwa familia ya waziri.
Kaka anapata janga hili, mdogo mtu anapata janga lile. Tena kwa kipindi
kifupi. Kama si mikosi ni nini sasa?” alihoji msomaji mmoja.
0 comments:
Post a Comment