Saturday, 4 July 2015

SLIM AELEZA UGUMU WA MWEZI MTUKUFU

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

 SlimOmary 
Staa wa filamu Bongo, Slim Omary.

Gladness mallya
STAA wa filamu Bongo, Slim Omary ameeleza ugumu anaokutana nao kutokana na kutokuwa na mke wa kumpikia futari kama alivyozoea.
Akistorisha na gazeti hili, Slim ambaye hivi karibuni ameachana na mkewe Asia Morgana kwa kupeana talaka mahakamani, alisema mwezi huu mtukufu ni changamoto kubwa kwake hasa kwenye suala la futari kwani alikuwa amezoea kuandaliwa na mkewe lakini ndiyo hivyo wameachana inabidi ale kwa mama lishe kwani si hodari wa kukaa jikoni mwenyewe.
“Napata changamoto kubwa sana lakini namshukuru Mungu kwa kuwa aliwaweka mama lishe kwani ndiyo wanaonisaidia mimi kupata futari kwani nilizoea kupikiwa nyumbani lakini kwa sasa hakuna wa kuandaa hivyo kwa kila jambo namshukuru Mungu tu,” alisema Slim huku akiongeza kuwa anamuomba Mungu ampatie mke mwema.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger