Jeshi la polisi wilayani
kahama mkoani Shinyanga limekamata mashine moja ya BVR ikitumika
kuandikisha wapiga kura saa tatu usiku nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa
wa Nyakato wilayani humo Mayunga Alphonce kupitia CHEDEMA, huku wakiwalipa shilingi 5,000 kila mmoja.
Akizungumza leo na
waandishi wa Habari mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya amesema tukio
hilo limetokea jana majira ya saa 3 usiku katika mtaa wa nyakato ambapo
mashine hiyo ilikutwa ikiwa inafanya kazi ya kuandikisha wapiga kura.
Mpesya amesema kuwa
vyombo vya usalama wilayani humo vilipata taarifa kutoka kwa raia wema
ambazo zimewezesha kukamatwa kwa mashine hiyo pamoja na vitambulisho
vitano ambavyo tayari vilikuwa vimeshakamilika kuandikishwa.
Ameongeza katika
harakati za kukamata mashine hiyo pia wameweza kumkamata mhamiaji haramu
mmoja raia wa Burundi ambaye tayari alikuwa ameshaandikishwa na mashine
hiyo akiwa ndani ya nyumba ya mwenyekiti huyo wa mtaa.
Mpesya amesema jeshi la
Polisi wilayani humo linamshikilia kaimu afisa mtendaji wa kata ya
Nyasubi Lugina Misango ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia mashine
hizo kwa kosa la kuruhusu mashine hiyo kutumika nyumbani kwa myekiti wa
mtaa.
Katika hatua nyingine
Mpesya amewataka waandishi wa habari wanaotumiwa kukanusha taarifa hiyo,
kutambua kuwa ofisi yake ni mamlaka kamili ya serikali na kwamba
wasubiri hatua za kisheria kwani ushahidi wa kukamatwa kwa mashine hiyo
upo kituo cha polisi.
0 comments:
Post a Comment