Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Liberatus Sabas
Na woinde shizza,arusha.
Jeshi la
Polisi Mkoani hapa linatarajia kuwafanyia usaili vijana wa Mkoa huu
waliomaliza kidato cha nne mwaka 2014 ambao wamechaguliwa kupitia tovuti
ya Tamisemi ambayo ni www.pmoralg.go.tz. Wanaotarajia kujiunga na
mafunzo ya Jeshi la Polisi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Liberatus Sabasaliyasema
hayo ofisini kwake leo asubuhi ambapo alisema zoezi hilo litafanyika kwa
muda wa siku mbili mfululizo yaani kuanzia tarehe 06.07.2015 na tarehe
07.07.2015 katika ofisi za Makao Makuu ya Polisi za Mkoa huu.
Aidha
alisema zoezi hilo litaanza kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 10:00
Jioni huku tayari majina ya vijana waliochaguliwa na maelezo yake
yameshabandikwa katika ofisi za Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Arusha, Mkuu wa wilaya ya Arusha na Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa
wilaya ya Arusha Mjini huku wilaya za Longido, Arumeru, Monduli, Karatu
na Ngorongoro majina yao yatabandikwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na
Halmashauri husika za wilaya hizo.
Waombaji
watatakiwa wawe na vyeti vyote vya masomo (Academic
Certificate(s)/Result Slip(s) & Leaving Certificate(s) na nakala
halisi ya cheti cha kuzaliwa (original Birth Certificate) huku Hati ya
Kiapo cha kuzaliwa haitakubaliwa pia atatakiwa kuwa na namba za simu
ambayo itasaidia kumjulisha endapo atachaguliwa.
Aidha
Kamanda Sabas alisema kwamba kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili
atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la
usaili huku atatakiwa kuwa na kalamu ya wino kwa ajili ya usaili wa
kuandika bila kusahau kuzingatia tarehe na muda kuanza usaili.
Kamanda
alimalizia kwa kusema kwamba, Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye
kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye ili mradi awe
amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili
0 comments:
Post a Comment