Wednesday 28 September 2022

NDEJEMBI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUJITOA KIKAMILIFU KATIKA KUWAHUDUMIA WANANCHI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili.

Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao, wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili.


Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Meatu, Bw. Msoleni Dakawa, akitoa taarifa ya utelezaji wa majukumu ya halmashauri yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Wakwanza kulia), wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi katika halmashauri hiyo.


Mkuu wa Shule ya Kimali, Bw. Marco Ng’wendamunkono wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa halmashauri hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi (Wakwanza kushoto) akijibu hoja iliyokuwa imewasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo. Kulia Kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Fauzia Ngatumbura na kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Oscar Maduhu.


Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Thomas Shishwa akitoa neno la shukurani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

***************************

Na. Veronica E. Mwafisi-Meatu

Tarehe 28 Septemba, 2022

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa umma nchini kujituma na kujitoa kikamilifu katika kuwahudumia wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Serikali kupitia taasisi zake.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa watumishi wa umma, wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu akiwa katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamozo zinazowakabili watumishi wa umma katika Wilaya hiyo.

Mhe. Ndejembi amesema, watumishi wa umma ni mabalozi wa serikali hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, weledi, kujituma na kujitoa kwa ajili ya serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Mtumishi wa umma ni mwakilishi wa serikali mahali anapofanya kazi, hivyo hana budi kutambua kuwa serikali imemuajiri ili kuwatumikia wananchi kwa kuwapatia huduma bora kama ambavyo serikali imekusudia,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Meatu, Bw. Msoleni Dakawa amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ajira mpya 104 katika Halmashauri hiyo zikiwemo kada za elimu na afya ili kuwahudumia wananchi wilayani humo.

Aidha, Bw. Msoleni ameishukuru ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kutoa kipaumbele cha kuwapatia stahiki watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

Naye, Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Thomas Shishwa kwa niaba ya watumishi wengine, amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kutenga muda wake kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi papo kwa hapo, ikiwa ni pamoja na kuwapatia ufafanuzi wa hoja za masuala ya kiutumishi walizoziwasilisha.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi anaendelea na ziara ya kikazi Mkoani Simiyu yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.

Share:

NAIBU WAZIRI MASANJA AFUNGUA WARSHA YA WADAU WA UHIFADHI MFUMO WA IKOLOJIA WA HEWA YA UKAA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akifungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) akifungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul (kushoto) wakikata utepe kama ishara ya kufungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul akizungumza katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii,Deusdedit Bwoyo akitoa maneno ya utangulizi katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akizungumzia namna taasisi yake inavyoshiriki katika utunzaji wa misitu ya mikoko katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati)katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

…………………………………………….

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amefungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini.

Warsha hiyo imefunguliwa Septemba 27,2022 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ufunguzi huo, Mhe. Masanja amesema misitu ya mikoko na majani ya baharini inatarajiwa kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa bluu kwa kuhifadhi hewa ya ukaa mara tano zaidi ya misitu ya kawaida.

Ameelekeza washiriki wa warsha hiyo kuibua masuala muhimu yatakayoisaidia Serikali kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya biashara ya hewa ya ukaa.

Ametaja faida nyingine za misitu ya mikoko kuwa ni kusaidia kukabiliana na athari za kimazingira kama mabadiliko ya tabia ya nchi, mmomonyoko wa udongo na vimbunga baharini, kusaidia uwepo wa mazalia ya samaki, chanzo cha kuni, mbao na milunda ya kujengea.

Aidha, amesema uwepo wa shughuli za kibinadamu katika misitu ya mikoko, hupelekea kupotea kwa mikoko na kuathiri ukuaji wa uchumi wa bluu.

Mhe. Masanja amefafanua kuwa ili kukabiliana na changamoto za upotevu wa misitu ya mikoko Serikali itatoa elimu kwa wananchi namna bora ya kutunza mikoko hiyo na kushiriki moja kwa moja katika uhifadhi wa mikoko kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Naye, Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu za Misitu Tanzania, Prof Dos Santos Silayo amesema wananchi wanatakiwa wawe na mifumo endelevu ya kupata kipato itakayowawezesha kukidhi mahitaji yao bila kukata mikoko.

“Mifumo hii itawawezesha wananchi kuvuna hewa ya ukaa na kujipatia fedha bila kuathiri mikoko kwa mfano kufanya shughuli za ufugaji nyuki na utalii” amefafanua Prof. Silayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uvuvi, Wizara ya Uchumi wa Bluu Zanzibar, Dkt. Salumu Hemedi amesema kuna uhusiano mkubwa wa uchumi wa bluu na biashara ya hewa ya ukaa.

Amesema biashara ya hewa ya ukaa inafanyika sana katika mataifa mengi duniani ambayo yana viwanda yanatumia hewa ya ukaa katika nchi ambazo zina misitu ambazo zinalipwa ili kutunza misitu.

Warsha hiyo imehudhuriwa wa Maafisa kutoka Serikali ya Tanzania na Kenya, Wawakilishi wa Sekta Binafsi, Wadau wa Uhifadhiwa Mifumo Ikolojia ya Bluu pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania.
Share:

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YATEMBELEA EPZA NA DAMPO LA PUGU


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mhe.David Kihenzile wakitazama namna ya uhifadhi maji taka katika kiwanda cha kutengeneza nguo EPZA mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea mamlaka hiyo leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam.

Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile akiongozana na kamati yake kutembelea dampo la uchafu lililopo Pugu leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile akiongozana na kamati yake kutembelea dampo la uchafu lililopo Pugu leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam.Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira akionesha jambo mara baada ya kamati hiyo kufanya ziara ya kutembelea dampo la kuhifadhi uchafu lililopo Pugu Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Mhandisi Amani Mafuru mara baada ya kamati hiyo kufanya ziara ya kutembelea dampo la kuhifadhi uchafu lililopo Pugu Jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mhe.David Kihenzile wakitazama namna ya uhifadhi maji taka katika kiwanda cha kutengeneza nguo EPZA mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea mamlaka hiyo leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile (mwenye kaunda ya bluu) akimsikiliza Meneja Utawala wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu ya Uwekezaji(EPZA) Bw.Rigobert Massawe mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza nguo kilichopo EPZA leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile akiongoza na kamati yake kutembelea kiwanda cha kutengeneza nguo kilichopo EPZA mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea EPZA leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile (mwenye kaunda ya bluu) akimsikiliza Meneja Utawala wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu ya Uwekezaji(EPZA) Bw.Rigobert Massawe mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza nguo kilichopo EPZA leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam.Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mhe.David Kihenzile wakitazama namna ya uhifadhi maji taka katika kiwanda cha kutengeneza nguo EPZA mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea mamlaka hiyo leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira wakiwa katika kikao mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea dampo la uchafu Pugu pamoja na Mamlaka ya Ukanda Maalumu ya Uwekezaji(EPZA) leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile akizungumza katika kikao na kamati yake mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea dampo la uchafu Pugu pamoja na Mamlaka ya Ukanda Maalumu ya Uwekezaji(EPZA) leo Septemba 28,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

************************

KAMATI ya Bunge Viwanda Biashara na Mazingira imeishauri Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kuhakikisha uchafu ulipo katika dampo kuufanya fursa na kuibua miradi mbalimbali itokanayo na uchafu ili kupunguza mlundikano wa uchafu katika eneo hilo.

Pia imeutaka uongozi wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji(EPZA) kuboresha miundombinu ya kimazingira katika eneo hilo ili kuweza kuwavutia na kuwashawishi wawekezaji.

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyotembelea Dampo hilo na baadae Mamlaka ya Ukanda Maalumu ya Uwekezaji(EPZA) Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda Biashara na Mazingira David Kihenzile kimsingi alisema hatua hizo zote ni muhimu na zaidi zimelenga kuhakikisha afya wananchi zinalindwa.

Akiwa na Kamati hiyo katika dampo la Pugu Kinyamwezi, Kihenzile alisomewa ripoti ya utendaji kazi wa Dampo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Amani Mafuru aliyebainisha kuzidiwa kwa dampo hilo kutokana na uwingi wa taka zinazozalishwa katika Jiji la Dar es Salaam.

"Tumejionea changamoto lukuki ambazo zinalikabili dampo hili, kimsingi sisi kama kamati tumeona kuna kila sababu ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kuweka mkono wake mahali hapa na kulisaidia Jiji la Dar es Salaam ambalo linaoekana wazi kuwa limezidiwa nguvu" alisema Kihenzile

Alisema kwa kufanya hivyo pamoja na mambo mengine kwa kiasi kikubwa kutasadia kuokoa maisha ya wananchi waliopo jirani na dampo hilo kutokana na athari zitokanazo na dampo ikiwemo hewa chafu.

Kuhusu EPZA Kihenzile mbali na kutaka Viwanda vingine nchini kuiga njia bora ya utunzaji wa mazingira katika eneo hilo, aliutaka Uongozi unaousimamia ukanda huo wa uwekezaji kuhakikisha miundombinu yake ya kimazingira hasa mfumo wa majitaka ya viwanda yanakuwa bora zaidi ili kuendelea kuwavutia wawekezaji.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo akiwemo Hawa Mchafu na Deo Mwanyika, mbali na kuunga mkono hoja ya Ofisi ya Makamu Raise Muungano na Mazingira kuungana na Jiji la Dar es Salaam katika kutafuta suluhu ya dampo hilo,walisema kuna haja eneo linalolizunguka dampo kujengewa ukuta

Pamoja na ukuta, pia walishauri kuona namna gani afya za wananchi waliopo karibu na dampo hilo zinatazamwa lakini pia wafanyakazi wanaotoa huduma katika dampo hilo .
Share:

HUAWEI,UDSM WAZINDUA KITUO CHA MAFUNZO YA TEHAMA KWA VITENDO


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew (Katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa vitendo katika Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kituo hicho kilichojengwa kwa msaada wa kampuni ya Huawei Tanzania kilizinduliwa wakati wa kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na miaka 10 ya CoICT yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wengine ni pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye (wa pili kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bw. Shang Xiaofeng (wa pili Kushoto) na Rasi wa Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano, Prof. Joel Mtebe (kushoto).


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew (kushoto) akichangia mawazo wakati akizindua kituo cha mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa vitendo katika Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kituo hicho kilichojengwa kwa msaada wa kampuni ya Huawei Tanzania kilizinduliwa wakati wa kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na miaka 10 ya CoICT yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.


Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bw. Shang Xiaofeng akitoa hotuba yake wakati wa kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na miaka 10 ya CoICT yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye ( wa tatu kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bw. Shang Xiaofeng ( wa pili kushoto), Rasi wa Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano, Prof. Joel Mtebe ( wa pili kulia) na viongozi wengine waandamizi kutoka taasisi hizo mara baada ya uzinduzi wa kituo cha mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa vitendo katika Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

..................................................

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

Kampuni ya Mawasiliano ya Huawei Tanzania na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamezindua kituo cha mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa vitendo katika Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) iliyopo eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mradi huo unaolenga kutoa uzoefu wa kivitendo kwa wanafunzi na wataalamu wa Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ulizinduliwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew wakati wa kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na miaka 10 ya CoICT yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Akizungumzia hatua ya Huawei, Mhandisi Kundo, aliipongeza kampuni hiyo ya China kwa jitihada zake za kuendeleza na kukuza sekta ya Habari na Mawasiliano nchini huku akibainisha kuwa serikali imefurahishwa sana na mchango wa kampuni hiyo katika kuchochea ukuaji wa sekta hiyo muhimu.

“Ni mwaka mmoja tu umepita tangu nilipozindua maabara ya TEHAMA ya Huawei katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na leo tena nimezindua kituo cha mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa vitendo hapa CoICT ambacho pia kinatokana na ufadhili wa kampuni ya Huawei. Hili ni jambo kubwa na tuna kila sababu ya kuwashukuru na kuwapongeza Huawei kwa juhudi zao,'' alisema.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bw. Shang Xiaofeng alisema kuwa kituo hicho kinalenga kutoa mafunzo kwa wahandisi zaidi ya 200 kila mwaka wakiwemo wanafunzi na wahitimu ili kukuza mfumo wa ikolojia wa vipaji nchini katika miaka ijayo.

"Kujenga uhusiano wa muda mrefu, kutafuta njia nzuri za kuzitumia rasilimali tulizonazo, juhudi za kuleta za maendeleo, na manufaa kwa pande zote ni jukumu letu sote. Ninaamini kabisa kituo hiki pamoja na kituo cha Mafunzo cha Huawei cha Chuo Kikuu ch Dodoma vitakuwa msingi katika kufikia mafanikio haya ya pamoja" alisema Bw. Shang

Kulingana na Bw. Shang, kampuni hiyo kwa sasa inatekeleza miradi mingi inayowanufaisha maelfu ya wanafunzi na watendaji wa sekta hiyo kwa nia ya kujengea uwezo kwenye nyanja ya TEHAMA na kuboresha maendeleo ya nyaja hii nchini.

“Miradi hii ni pamoja na programu ya mafunzo ya TEHAMA ya Huawei, Shindano la TEHAMA la Huawei pamoja na mradi wa Seeds for the Future,’’ aliitaja na kuongeza kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa ajili ya kutimiza Dira ya Taifa ya 2025 kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza.

Alibainisha zaidi kuwa Huawei itaendelea kujitolea katika uvumbuzi wa miundombinu ya kidijitali, ili kujenga thamani kwa wateja na washirika.

‘’Huawei tunasisitiza kuwekeza zaidi ya 10% ya mapato yetu ya mauzo katika Utafiti na Maendeleo kila mwaka, na tunapanga kuendelea kuongeza uwekezaji huu. Mnamo mwaka 2021, tulitumia Dola za Marekani bilioni 2.4 katika utafiti na maendeleo, ikilinganishwa na jumla ya Dola za Marekani bilioni 120 katika muongo mmoja uliopita.’’

“Tumeanzisha maabara 86 za kimsingi duniani kote, na kuwekeza zaidi ya dola bilioni 3 katika utafiti wa kimsingi kila mwaka’’ alibainisha

Katika hotuba yake wakati wa hafla hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye alipongeza uhusiano uliopo kati ya chuo hicho na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo kampuni ya Huawei.
Share:

UZAZI WA MPANGO CHANZO CHA UCHUMI IMARA


Muuguzi akionesha mojawapo ya njia salama za uzazi wa mpango ambayo ni kitanzi. 

****************** 

Na Irene Mark 

WAKATI Dunia ikiadhimisha siku ya uzazi wa mpango kila Septemba 26 ya mwaka, suala la utoaji mimba kwa njia zisizo salama linachangia ongezeko la vifo vitokanavyo na uzazi. 

Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), inaeleza kuwa vifo vya uzazi nchini Tanzania viliongezeka hadi vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2015 kutoka vifo 454 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2010. 

Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi, Elias Kweyamba, anasema asilimia kati ya 16 hadi 19 ya vifo vya uzazi vinatokana na utoaji wa mimba usio salama. 

Kwa sababu hiyo ipo haja ya Dunia husasani kwa nchi zinazoendelea kupata elimu sahihi ya njia za uzazi salama ili kuepuka mimba zisizotarajiwa ambazo mara nyingi hutolewa kwa njia hatarishi. 

Wakizungumza na *HabariMseto Blog* kwa nyakati tofauti baadhi ya wanawake waliofika kwenye Zahanati ya Mpunguzi jijini Dodoma kupata huduma za kliniki pamoja na watoto wao wamesema elimu zaidi inahitajika hasa kwenye matumizi ya njia za uzazi wa mpango. 

Wameeleza namna wanavyokosa elimu ya kupambana na maudhi madogomdogo baada ya kutumia njia za kupanga uzazi hali inayowalazimu kusitisha matumizi ya njia hizo na kuwasababishia kupata watoto wasiowatarajia ama kutoa mimba kwa njia hatarishi. 

Wanawake hao pia hawana taarifa za uwepo wa siku ya kupanga uzazi duniani ambayo kimsingi inawahusu katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi lakini pia kuwa na afya njema huku wakishiriki kazi za kiuchumi kwa maslahi ya familia zao na taifa. 

Katika kuadhimisha siku hiyo kila mwaka serikali, mashirika kibinafsi, vyombo vya habari na watu mbalimbali hukusanyika na kujadili masuala muhimu ya upatikanaji wa huduma bora za uzazi wa mpango. 

Monica Agustino (22) kutoka Kijiji cha Mpunguzi ni mama wa watoto wanne, mkubwa ana miaka sita na mdogo ana miezi mitatu. 

Anasema hivi sasa hata afya yake si nzuri kutokana na kupata watoto mfululizo huku akibainisha kwamba malezi ya watoto kwa kufanya vibarua kwenye mashamba ya watu ni magumu. 

“Niliwahi kuzaa baada ya kukatisha masomo nikiwa kidato cha pili kijana niliyezaa naye ndio baba wa watoto wote hawa tunafurahi kuona watoto ila tunakabiliana na wakati mgumu katika malezi hasa wakiumwa. 

“Nimesikia kuhusu njia za uzazi wa mpango nikiwa na mtoto wa pili nilitumia njia ya kijiti lakini nilishindwa kwa sababu waliniambia damu yangu haijaendana. 

“Baada ya kuweka kijiti nikawa napata kizunguzungu, nakosa hamu ya kula, napata hedhi mfululizo na kuchoka sana ikabidi nikitoe sikumaliza muda mrefu nikabeba mimba ya mtoto wa tatu,” amesisitiza Monica. 

Huku akitabasamu Monica anasema anatamani kupata njia ya uzazi wa mpango itakayomsaidia bila kupata maudhi yanayomuumiza mwili. 

Anasema hakupata kwa wakati elimu ya uzazi wa mpango ndio maana amekuwa na familia kubwa inayomshinda kwenye malezi hivyo anakuwa tegemezi kwa ndugu na majirani. 

“Kuna wakati tunakosa chakula na mimi ninanyonyesha basi napambana kuomba nikipata kidogo nawapa watoto mimi na baba yao tunavumilia. 

Theresia Masanja (28) mwanakijiji kutoka Mpunguzi aliyekuwepo kwenye zahanati hiyo anasema mimba za mfululizo zilimfanya apoteze watoto wake wawili na kwamba baada ya kupata ushauri wa kitaalam wa njia za kisasa na bora za uzazi wa mpango amezifuata na sasa anaishi kwa furaha. 

“Nilipata mimba nikiwa na mtoto wa siku 40 kwa huku kijijini kwatu ni aibu nikatafuta mbinu za kienyeji za kutoa mimba. 

“Mtoto alikuwa na nyonya nikaelekezwa dawa nikanywa mimba ilishafikia miezi mitatu kumbe dawa ile niliyokunywa ni sumu kiumbe cha tumboni kilikufa na mimi hali yangu ikawa mbaya nilisafishwa kizazi huku nyumbani mwanangu mdogo aliugua na kwa kuwa hakunyonya hali ilikuwa mbaya akaletwa hospitali lakini haikuwa habati, mwanangu akafariki akiwa na miezi mitano. 

“Nilipata elimu na vipimo nikakubaliana na watoa huduma na sasa natumia njia ya kitanzi. Nimebaki na watoto wawili mkubwa ana miaka 12 na mdogo ni huyu wa mwaka mmoja na nusu,” anasema Masanja huku akitabasamu. 

Anazitaja njia nyingine za uzazi wa mpango anazozifahamu kuwa ni kondom, sindano, dawa, kijiti na kufunga uzazi. 

Masanja alishauri elimu ya uzazi wa mpango iwafikie pia wanaume ili nao washiriki katika kutunza afya za wake zao na watoto. 

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Mussa Mfaume amesema ofisi yake imefungua milango kwa mashirika binafsi kupeleka elimu ya uzazi wa mpango kwa wanaume ambao ni wadau muhimu kwa mustakabali ya afya ya mwanamke na watoto. 

“Licha ya kutoa kipaumbele kwa wanaume wanaokuja kliniki na wake zao kuoata huduma kwa haraka bado elimu zaidi inahitajika ili suala la afya ya uzazi liwe jambo la kifamilia,” amesisitiza Dk.Mfaume 

Mtoa huduma wa afya ya uzazi na uzazi salama, Ozia Dominic, amesema wanawake wengi wanajitokeza kupata elimu kuliko wanaume hivyo wanawahamasisha kuwapeleka waume zao. 

Hata hivyo tafiti mbalimbali za wataalam wa afya chini ya UNFPA zinaonesha kwamba zaidiee ya wanawake na wasichana bilioni 1.8 wako katika kundi la umri wa uzazi lakini wengi wao wanakabiliwa na vikwazo ambavyo ni ukosefu wa taarifa sahihi na huduma bora za kupanga uzazi kutoka kwa watumishi wenye utaalam. 

Nchini Tanzania asilimia 32 tu ya wanawake walio katika umri wa uzazi wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango huku asilimia 22 wakiwa na mahitaji ambayo hayajafikiwa. 

Kwa kuzingatia kanuni zilizopo zinazowaweka wasichana kwenye ngono na ndoa za utotoni, asilimia 27 ya wasichana wenye umri kati ya miaka 19 na 15 ni wajawazito au wameanza kuzaa. 

Matokeo yake, wanakabiliwa na hatari kubwa za kuharibika kwa mimba, utoaji mimba usio salama, aina nyingine za magonjwa ya uzazi ikiwemo saratani na vifo kutokana na matatizo ya ujauzito na uzazi. 

Mbali na hayo, wanawake na wasichana wanashindwa kutimiza ndoto zao za maendeleo na kukabiliwa na kutengwa katika kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na vyombo vya maamuzi kwa sababu ya kushindwa kusimamia uzazi wao. 

Huduma za kupanga uzazi ni moja ya afua mtambuka zinazopewa kipaumbele hasa katika huduma za kinga za afya. 

Huduma hizo za ni muhimu katika kufikia malengo makuu ya afya hasa katika afya ya uzazi na mtoto. Inachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya uzazi kwa takriban asilimia 44 kupunguza vifo vya watoto. 

Huduma hizo ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa kaya na taifa, kuondoa umaskini na kupunguza njaa. 

Pia zinasaidia kupambana na maradhi ya Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI), kukuza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake, kuhakikisha uendelevu wa mazingira na kukuza uchumi wa mmoja mmoja na kaya kwa ujumla.
Share:

Tuesday 27 September 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 28,2022

Magazetini leo Jumatano September 28 2022










Share:

BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA KWA AJILI YA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI MAMA SAMIA KAHAMA


Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akimkabidhi meza Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Mama Samia iliyopo katika Manispaa ya Kahama. Meza hiyo ni sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2021. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Benki ya CRDB imekabidhi viti 62 na meza 62 kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mama Samia iliyopo katika mtaa wa Sokola kata ya Majengo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.


Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika leo Jumanne Septemba 27,2022 katika shule hiyo ambapo Mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga.


Akizungumza wakati wa kukabidhi viti na meza hizo, Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana amesema benki hiyo ni mdau mkubwa wa elimu na imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika shule ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.

"Leo tunakabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mama Samia ikiwa ni sehemu ya utamaduni wa benki ya CRDB kushirikiana na serikali kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya elimu. Tutaendelea kushirikiana na serikali kutatua changamoto zilizopo", amesema Wagana.


"Sisi Benki ya CRDB kama Benki inayoongoza nchini Tanzania tunaamini suala la elimu ni la kila mtu, tunaomba wadau mbalimbali wajitokeze kusaidia mahitaji yaliyopo katika shule zetu kwani serikali pekee haiwezi kumaliza changamoto zote", ameongeza.

Katika hatua nyingine Wagana ametumia futsa hiyo kuwaomba wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB ikiwemo mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima na watumishi pamoja na kufungua akaunti zikiwemo akaunti kwa ajili ya watoto 'Junior Jumbo Account' na Malkia Account kwa ajili ya wanawake.


"Sisi CRDB tunajitahidi kuwezesha watoto wasome katika mazingira bora na tutaendelea kuboresha sera zetu. Benki ya CRDB ni mahali salama, tuna akaunti za kila aina, karibuni mtuunge mkono kwenye benki hii ya Watanzania", ameeleza Wagana.

Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kahama, Evodi Kareti na Meneja Rasilimaliwatu Benki ya CRDB, Benjamini Ngaiwa wamewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuepuka vishawishi vinavyoweza kusababisha washindwe kumaliza masomo hivyo kutotimiza ndoto zao na kwamba Benki ya CRDB itaendelea kutoa michango mbalimbali katika sekta ya elimu.


Akizungumza wakati wa kupokea viti na meza hizo, Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya ameishukuru Benki ya CRDB kwa namna inavyoendelea kushirikiana na serikali kutatua changamoto katika sekta ya elimu huku akibainisha kuwa viti na meza hizo zitasaidia wanafunzi hao kusoma katika mazingira bora.


"Tunawashukuru benki ya CRDB kwa kuendelea kutushika mkono, naomba mtunze viti na meza hizi pamoja na miundombinu mingine ya shule", amesema Ndanya.

Aidha amewashukuru wananchi wakiwemo wafanyabiashara kufungua akaunti katika benki ya CRDB kwani benki ikipata wateja wengi itapata faida na kurudisha faida hiyo kwa wananchi.

Ndanya ameipongeza shule ya sekondari Mama Samia kwa kutokuwa na rekodi ya mimba kwa wanafunzi hivyo kuwataka wanafunzi hao kujitunza na kujiheshimu na kuachana na vishawishi vinavyoweza kukatisha ndoto zao.


Diwani wa kata ya Majengo, Benard Mahongo ameishukuru benki ya CRDB kwa kuendelea kuendelea kuisaidia shule hiyo na kuomba wasichoke kusaidia kwani bado shule hiyo ina uhaba wa vyoo hivyo kuomba benki ichangie nondo kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala ambalo lina sehemu ya choo ili kuondokana na hali iliyopo sasa ambapo walimu na wanafunzi wanatumia choo kimoja.

Awali akizungumza, Mkuu wa Shule ya Sekondari Mama Samia, Joyce Thomas Jewe ameishukuru Benki ya CRDB kutatua changamoto ya uhitaji wa viti na meza katika shule hiyo changa iliyoanzishwa Tarehe 05.05.2021 ambayo sasa ina jumla ya wanafunzi 547 kati yao wasichana ni 267 na wavulana ni 284 ikiwa na walimu 15 kati yao wa kiume ni wawili na wa kike 13.

"Kutokana na uchanga wa shule hii tunakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mashine ya kuzalishia mitihani ya majaribio (Photocopy Mashine) na wamekwama kumalizia boma la jengo la utawala kwa kukosa nondo,kokoto na mifuko ya saruji ili pindi ujenzi utakapokamilika shule ipate mahali salama pa kutunzia nyaraka muhimu",amesema.
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akimkabidhi meza Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Mama Samia iliyopo katika Manispaa ya Kahama. Meza hiyo ni sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2021.  Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akimkabidhi  kiti Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Mama Samia iliyopo katika Manispaa ya Kahama. Kiti hicho ni sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akimkabidhi kiti Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Mama Samia iliyopo katika Manispaa ya Kahama. Kiti hicho ni sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana na Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya  na viongozi mbalimbali pamoja na wanafunzi wakipiga picha wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Muonekano wa sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Muonekano wa sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja Rasilimaliwatu Benki ya CRDB, Benjamini Ngaiwa akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kahama, Evodi Kareti akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Diwani wa kata ya Majengo Manispaa ya Kahama, Benard Mahongo akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Mkuu wa shule ya Sekondari Mama Samia , Joyce Thomas Jewe akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Afisa Elimu Manispaa ya Kahama, Anastazia Vicent akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mama Samia wakifuatilia nasaha mbalimbali wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia 
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mama Samia wakifuatilia nasaha mbalimbali wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia 
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kahama, Evodi Kareti akizungumza na Wanafunzi wa shule ya sekondari Mama Samia
Awali vijana wa Skauti wakimpokea mgeni rasmi Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya akiwasili katika shule ya sekondari Mama Samia
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mama Samia.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger