Monday 29 August 2022

MLINZI WA KANISA ATUPWA JELA KWA KUMUIBIA SISTA

MLINZI wa Hospitali ya Kanisa Katoliki la Kijiji cha Mwanzugi wilayani Igunga, Peter Marco apata kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kumuibia kwa kutumia silaha Sista Aline Nicette vitu kadhaa, ikiwamo simu ya mkononi, vyote vikiwa na thamani ya Tsh.720,000/-


Mahakimu Augustine Mwarija, Lugano Mwandambo na Lilian Mashaka walitupilia rufaa ambayo Marco, mrufani, aliwasilisha kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu.

“Tumeridhika kwamba ushahidi ulithibitisha kesi dhidi ya Marco bila shaka yoyote, kiwango cha uthibitisho kinachotumika katika kesi za jinai. Hatuoni umuhimu wa kukata rufaa na tumeitupilia mbali,” walisema katika hukumu yao waliyoitoa Tabora hivi karibuni.


Wakati wa kusikilizwa kwa rufaa hiyo, Marco alilalamika kuwa ushahidi wa utambulisho wa vielelezo kupitia mashahidi wawili wa upande wa mashtaka ambao ni Mlinzi na Sista Aline uliotegemewa na Mahakama Kuu kuthibitisha hukumu yake ya unyang’anyi wa kutumia silaha unatia shaka na kesi inayomkabili haikuthibitishwa.

Shahidi wa tukio hilo ambaye alikuwa mlinzi mwenza wa mtuhumiwa(Marco) alisema majambazi nane walivamia kanisani hapo, huku wanne wakiwa na mapanga. Alifanikiwa kumtambua Marco ambaye alimuona akiwa ameshika panga na bunduki.

Shahidi huyo aliiambia mahakama ya mwanzo kuwa aliweza kumtambua Marco kupitia taa ya umeme inayomulika mahali hapo na majambazi hao walikuwa karibu naye kiasi kwamba hata baada ya kuumia kufuatia kupigwa risasi na kupoteza fahamu, aliweza kumkumbuka Marco kuwa mmoja wao.

Imeandikwa na: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.
Share:

TPDC MARATHON KUCHANGIA GHARAMA ZA UPASUAJI WA WATOTO 511 JKCI

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC), DKT. James mataragio akizungumza katika uzinduzi wa TPDC Marathon leo Agosti 29,2022 katika Ofisi za TPDC Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi akizungumza katika uzinduzi wa TPDC Marathon leo Agosti 29,2022 katika Ofisi za TPDC Jijini Dar es Salaam. Mratibu wa mbio hizo Bw.Fred Kwezi akizungumza katika uzinduzi wa TPDC Marathon leo Agosti 29,2022 katika Ofisi za TPDC Jijini Dar es Salaam.

********************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wamezindua mbio za hisani (TPDC Marathon) zenye lengo la kuchangia gharama za upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya moyo ambapo imebainishwa kuwa kuna watoto 511 wanasubiri upasuaji katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 29, 2022 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC), DKT. James mataragio amesema Malengo yao ni kusaidia na kuunga mkono juhudi za kuokoa maisha ya watanzania na kwa kuanzia mbio hizo ambapo watarajiwa kusaidia upasuaji wa watoto 50 wenye matatizo ya moyo.

"Tumelenga kusaidi Taasisi ya Jakaya kikwete (JKCI) na tumeamua kuunga mkono katika kuokoa maisha ya watanzania wenzetu ambapo baada ya kukamilika mbio hizi tunategemea kusaidia watoto 50 kwa kuanzia"

Aidha Dkt.Mataragio alisema kuwa Mbio hizo ni endelevu kwa kila mwaka hivyo amewaasa wananchi kushiriki kwa wingi kama sehemu ya mazoezi ili kulinda afya zao lakini pia kwa upande mwingne kusaidia watoto wenye matatizo ya moyo.

"Mbio hizi ni za kila mwaka na tutakua tunaendelea kuchangia kwa kadri ambavyo tutakua tunafanikiwa hivyo wananchi wote washiriki katika mbio hizi ili kuweza kuwasaidia wananchi wenzetu kuokoa maisha yao".Amesema Dkt.Mataragio.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi alisema kila mwaka asilimia moja ya watoto milioni mbili wanaozaliwa nchini Tanzania sawa na watoto elfu ishirini huzaliwa na matatizo ya moyo na kati yao asilimia ishirini na tano sawa na watoto elfu tano wanafanyiwa upasuaji wa moyo katika taasisi ya jakaya kikwete.

"Fedha zitakazopatikana zitatumika kikamilifu kwa malengo yaliyokusudiwa lakini pia kwa siku hiyo kutakuwa na upimaji wa magonjwa wa moyo bure, utoaji wa chanjo UVIKO-19 na uchangiaji wa damu kwa hiyari". Amesema

Nae Mratibu wa mbio hizo Bw.Fred Kwezi aliwahakikishia washiriki wa mbio hizo kuwa kutakuwepo na huduma zote za kimichezo, kiusalama na kiafya na kuwa Usajili unafanyika kwa kupitia TPDC pamoja na waratibu wa mbio hizo ambao ni Goba Rose Runners.

Mbio hizo zenye kauli mbiu isemayo “kimbia kwa afya yako” zinatarajiwa kufanyika septemba 11 mwaka huu katika viwanja vya farasi oysterbay jijini dar es salaam huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa raisi mstaafu wa serikali ya awamu ya nne Mhe. Jakaya mrisho kikwete.
Share:

PSPTB YAPIGA MARUFUKU WATAALAMU WANAOFANYA KAZI ZA MANUNUZI NA UGAVI ZA SERIKALI AMBAO HAWAJASAJILIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Manunuzi na Ugavi (PSPTB) Bw.Godfrey Mbanyi akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za PSPTB leo Agosti 29,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Manunuzi na Ugavi (PSPTB) Bw.Godfrey Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za PSPTB leo Agosti 29,2022 Jijini Dar es Salaam.

*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Bodi ya Umma Manunuzi na Ugavi (PSPTB) iwapiga marufuku Wataalamu wanaofanya kazi za Manunuzi na Ugavi za serikali ikiwa hawajasajiliwa na yeyote atakayebainika yuko kinyume sheria itachukuliwa dhidi yake.

Agizo hilo limetolewa leo Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Manunuzi na Ugavi (PSPTB) Bw.Godfrey Mbanyi ambapo amesema Wizara ya Fedha na Mipango inaendelea kukamilisha wa Mfumo mpya hivyo kabla ya kuanza kufanya kazi bodi watakwenda kufanya ukaguzi katika taasisi, Ofisi zote za serikali na ikibainika kuwa kuna mtu ameajiriwa kufanya kazi hiyo na hana sifa stahiki mwajiri aliyemuajiri atawanibika kisheria .

Sanjari na hayo amesema hapo awali kulikuwa na madhaifu mengi ambayo yalikuwa yakitokea kupitia mfumo wa zamani sababu wataalamu ambao waliokuwa hawana sifa stahiki kufanya shughuli hizo na kusababisha madhaifu ambayo Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali akija kukagua anakuta hasara hivyo jambo hilo halitavumiliwa linakwenda kutafutiwa mwarobaini.

"Mtaalamu yeyote hata Kama ni Afisa Manunuzi mwandamizi ana cheo kama hana usajiliwa na bodi hii Psptb hatoweza kutoka kwenda hatua moja nyingine kufanya kazi hatoweza kama hajaainisha taarifa zake za usajili katika mfumo huu mpya hivyo tunapofanya ukaguzi tukimbaini Mwajiri aliyemuajiri atawajibika kisheria "alisema Mbanyi

Hata hivyo mfumo huo upo kwenye majaribio na wote watakaokuwa katika usajili wa Mfumo mpya itasaidia kutoa huduma kwa urahisi bila kuchelewesha kazi za serikali hivyo nawasisitiza Waalamu wote wa Manunuzi na Ugavi kujisajili mapema .

Hata hivyo amesema ikitokea taasisi,Ofisi yeyote ya serikali Maafisa wake hawajasajiliwa na Mfumo huo mpya sheria Kali zitachikuliwa kwani hapo awali kabla ya mfumo huo mpya kulikuwa na changamoto ambapo hata ambao siyo wataalamu wasio na sifa ikiwemo taaluma usajili walikuwa wakitumia mfumo na kusababisha taarifa za Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali akikagua kukuta mapungufu .

Aidha Serikali mpaka sasa inaingia gharama ya kujenga mfumo huo mpya wa Manunuzi na Ugavi na inakwenda kukamilika hivyo utasaidia kurahisisha huduma na kuwatambua wataalamu wote wanaofanya kazi hiyo ambao wana sifa stahiki.
Share:

DOWNLOAD/ INSTALL UPYA APP YA MALUNDE 1 BLOG..Tumeboresha zaidi

Share:

PAPA FRANCIS ATEUA MAKARDINALI 20 WATAKAOSHIRIKI KUTEUA MRITHI WA KITI CHAKE


Papa Francis akiwatawaza Maaskofu kuwa Makardinali
Papa Francis akiwa katika kanisa la St.Peter’s

BABA Mtakatifu na mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis (85) amewateua maaskofu 20 na kuwatawaza kuwa makardinali watakaoongezeka kwenye jopo litakaloshiriki kumteua mrithi wa kiti chake.


Papa Francis katika uteuzi wake huo alijaribu kuwapa kipaumbele makardinali wa jamii zilizotengwa zaidi.

 Mmoja wa waliochaguliwa ni Askofu Hyderabad Anthony Poola kutoka nchini India mwingine ni Askofu Peter Ebere Okapaleke kutoka Nigeria.

Hafla hiyo ya kuwatawaza Maaskofu hao ilifanyika katika kanisa la St.Peters huko Vatican. Katika waliotawazwa 16 kati yao wana umri chini ya miaka 80.


Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 29,2022




















Share:

Sunday 28 August 2022

TAIFA STARS ILIVYOJIANDAA KUIVURUGA UGANDA JIONI HII




KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Uganda utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es salaam.


Mchezo huo wa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni.


Akizungumza na Spoti Xtra, Poulsen alisema wanatambua Uganda ni moja ya timu ngumu inayohitaji umakini kwenye kupambana nao.

“Uganda tunawatambua hasa kwa namna ambavyo wanatumia nguvu kutafuta ushindi, utakuwa ni mchezo ambao unahitaji nguvu na akili kubwa kwenye kutafuta ushindi ila tupo tayari, muunganiko unazidi kuwa imara.


“Kiakili na mbinu tumejipanga ukizingatia wachezaji wametoka kucheza mechi za ligi, hiyo inaongeza uimara, mchezo huu wa Uganda ni wa kwanza na mchezo wa pili ugenini utatupa picha ya sisi kufuzu CHAN ukichanganya na nguvu ya mashabiki basi kutakuwa na kitu cha kipekee,” alisema Poulsen.


Aishi Manula, Nahodha Msaidizi wa Taifa Stars, alisema: “Wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda, ambacho tunahitaji ni kufuzu CHAN, benchi la ufundi limefanya kazi kubwa na tunawatambua Uganda na wao wanatujua pia.”
Share:

Video Mpya : NYASANI - SENSA


Msanii Maarufu Nyasani kutoka Shinyanga ameachia video mpya ya wimbo wa Sensa. Audio producer ni  Sheddy the Mix, Paradox Empire Records, Video grapher📸 Davy Skerah, CM Production.

Tazama video  Hapa chini
Share:

JAMAA AUA CHUI KWA MIKONO



Chui

NDUMISO MONA; ni mwanaume mwamba kabisa wa nchini Afrika Kusini ambaye kwa sasa ni gumzo nchini humo baada ya kupambana na chui na kumuua kwa mikono yake mwenyewe.

Ndumiso alipambana na chui anayedaiwa kutoroka kutoka Hifadhi ya Kitaifa ya Kruger (KNP) huko Afrika Kusini.


Akiwa amesimama kwenye mwinuko wa nyumba yake katika Kijiji cha Matsulu Manispaa ya Mbombela huko Mpumalanga, Ndumiso aliyevalia ovaroli, soksi za kijivu na viatu alisimulia masahibu yake yaliyotokea asubuhi ya Julai 21, mwaka huu.


Ndumiso anasema; “Nilikuwa nikibarizi nje ya duka moja na marafiki zangu tuliposikia kuhusu chui anayezurura karibu na nyumba yangu.

“Akili yangu iliniambia nikimbilie nyumbani. Nilikuwa na wasiwasi na wadogo zangu wawili ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi.

“Nilikimbia na kupita nyumbani kwangu nilipomuona chui. Niligeuka na kushangaa akiunguruma nyuma ya mgongo wangu.

“Tulitazamana machoni. Sote tulisimama kwa takriban dakika mbili tukitazamana.


“Moyo wangu ulikuwa ukipiga sana. Nilimuona akifungua kinywa chake, nikaona meno makali. Alikuwa tayari kuruka. Nilikunja ngumi. Hakukuwa na kurudi nyuma.


“Nilijiambia kwamba mmoja kati yetu lazima afe.”


Ndumiso anasema kuwa, dakika 2 baadaye chui huyo alimrukia, wakaanza kupigana hadi chui akafa.”

Cc; @sifaelpaul
Share:

MAMA AFUNGIWA CHUMBANI NA MWANAE AKIDAIWA ELFU 7 NA MWENYE NYUMBA SHINYANGA MJINI


Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Abdi Adam akizungumza na Mariam Hamis  kupitia dirishani akiwa amefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela 
Kulia ni Mariam Hamis  akizungumza kupitia dirishani akiwa amefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela 
Mlango wa chumba cha Mariam Hamis ukiwa umefungwa na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela huku yeye akiwa ndani

Zoezi la kuvunja kufuli kwenye Mlango wa chumba cha Mariam Hamis uliofungwa na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela likiendelea
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Abdi Adam akifungua mlango wa Mariam Hamis  aliyefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela 
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Abdi (kushoto) akizungumza na Mariam Hamis  aliyefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mwanamke aitwaye Mariam Hamis mkazi wa mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga amefungiwa ndani ya chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela takribani saa 10 hadi serikali ya mtaa ilipofika kuvunja mlango kutokana na kile kilichoelezwa kuwa anadaiwa shilingi Elfu saba na mia nne (7400) ya bili ya maji.


Mariam Hamis amefanyiwa ukatili wa kufungiwa ndani ya chumba chake tangu jana Jumamosi majira ya saa tano usiku mpaka leo asubuhi saa tatu asubuhi wajumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi walipopata taarifa kuhusu tukio hilo na kufika nyumbani kwake na kulazimika kuvunja kufuli lililofungwa na mwenye nyumba aliyopanga aliyejulikana kwa jina la Evodia Charles Mahela.

Wajumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mabambasi wakiongozwa na Abdi Adam wamesema wamelazimika kuvunja kufuli hilo kutokana na kwamba kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki za binadamu.


Akielezea kuhusu kisa hicho, Mariam amesema ameshangaa kuona mama mwenye nyumba anafunga chumba hicho kwa madai kwamba hajalipa bili ya maji shilingi 7,400/=.


“Wapangaji tupo wanne,kila mpangaji anadaiwa shilingi 7400, mmoja amelipa bili ya maji, watatu hatujalipa bili ya maji lakini nashangaa mimi nimefungiwa nyumba. Humu ndani naishi na mtoto wangu mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu. Kanifungia mlango kwa kufuli tangu jana saa tano usiku, hiki chumba hakina choo ndani”,ameeleza Mariam.

Malunde 1 blog imemtafuta Evodia Charles Mahela ambaye kwa kujiamini amesema amemfungia mpangaji wake kutokana na kwamba alitaka kutoroka na pesa.

“Alikuwa anataka kutoroka na pesa,nikawaambia wafunge mpaka nitakapokuja,nikampigia simu huo usiku nikamwambia akitaka kuondoka atoe pesa au aache kitu maana wamekuwa na tabia ya kuondoka bila kulipa halafu mimi nabaki na madeni,sasa namwambia anaanza kunijibu vibaya na alikuwa anatoroka anatoroka na deni sasa mimi nitakuwa wa kulipa madeni ya watu..na geti jana usiku alilifunga funguo akakaa nazo yeye kwamba usiku huo atoroke.

“Nimeomba kufuli kwa mmoja wa wapangaji nikafunga nikawaambia asubuhi nichukue kitu chochote atoe hela, wameshahama wawili na hela na kwanini atoroke? Kwani asiage?”,amesema 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI 28,2022


Magazeti ya leo Jumapili August 28 2022

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger