Monday 2 May 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 3,2022



Magazetini leo Jumanne May 03 2022

Share:

WAZIRI NAPE NNAUYE ATEMBELEA BANDA LA LHRC MAONESHO YA KIHABARI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI




Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akisoma kitabu katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre - LHRC) leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'Picha na Kadama Malunde 1 blog 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akisoma kitabu katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre - LHRC) leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akizungumza katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre - LHRC) leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog



Share:

Picha : WAZIRI NAPE NNAUYE ATEMBELEA BANDA LA TCRA MAONESHO YA KIHABARI MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akiwa katika Banda la TCRA akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala kuhusu huduma zinazotolewa na TCRA leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. Waziri Nape Nnauye ametembelea banda la TCRA wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'Picha na Kadama Malunde 1 blog 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akiwa katika Banda la TCRA akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala kuhusu huduma zinazotolewa na TCRA leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akiwa katika Banda la TCRA akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala kuhusu huduma zinazotolewa na TCRA leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha.
Share:

NAPE NNAUYE ATEMBELEA BANDA LA SHIRIKA LA POSTA AKIZINDUA MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ( wa pili kulia) akitembelea banda la Shirika la Posta Tanzania leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara Shirika la Posta Tanzania, Costantine Kasese. Picha na Kadama Malunde 1 blog 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Posta Tanzania leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Posta Tanzania leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

WAZIRI NAPE NNAUYE ATEMBELEA BANDA LA STAMICO MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI JIJINI ARUSHA


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akiwa katika Banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Madini Shirika la STAMICO Happy Mbenyange kuhusu shughuli wanazofanya leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. Waziri Nape Nnauye ametembelea banda la STAMICO wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'. Picha na Kadama Malunde 1 blog 
Mhandisi wa Madini Shirika la STAMICO Happy Mbenyange akimwelezea Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) kuhusu Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira - Kabulo mkoani Mbeya.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiipongeza STAMICO kwa shughuli wanazofanya alipotembelea banda la STAMICO wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani Jijini Arusha yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'. Kulia ni Mhandisi wa Madini Shirika la STAMICO Happy Mbenyange.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

NAPE NNAUYE : WANA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUSAIDIA BARA LA AFRIKA RASILIMALI ZILIZOPO ZIBADILIKE KUWA BARAKA KWA WATU WAKE

 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani  leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. Picha na Kadama Malunde
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani  leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani  leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. 

Na Agness Nyamaru,Arusha.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewataka  wanahabari kutumia kalamu zao kukabiliana na changamoto zilizopo nchini na barani Afrika juu ya rasilimali zinazoharibiwa ili tatizo liweze kutatuliwa.


Ameyasema hayo leo wakati akizindua maonyesho kuelekea Kilele cha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani, Mei 5 mwaka huu ambapo mgeni rasmi katika kilele hicho anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa kauli mbiu ya yake ni "Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti" ambapo alisema wajibu wa sekta ya habari ni kusaidia bara la Afrika, rasilimali zilizopo zibadilike kuwa baraka kwa watu wake ili kuona matokeo  ya rasilimali hizo.


Alisema wakati umefika kwa wanahabari kuchukua maamuzi ya kusaidia bara hilo kufaidika na rasilimali zake na watu wake wajivunie kuwa waafrika na wajivunie kuwa kwenye bara lenye rasilimali za kutosha.

"Tukipewa hesabu ya rasilimali tulizonazo na ukilinganisha na mabara mengine hatupaswi kuwa hapa tulipo lakini kila mmoja wetu anapaswa kutimiza wajibu wake na wanahabari tunalo jukumu hilo kubwa la kubadilisha mambo maana hayapo sawa", alisema Nnauye.


"Angalia maovu mengi yaliyopo kwenye bara la Afrika sehemu ambapo kuna rasilimali nyingi ndipo watu wanapogombana zaidi, na sehemu ambapo kuna rasilimali za kutosha ndipo watu wake wanapoteseka sana sasa umefika wakati wa waandishi kusimama kusaidia kubadilisha mambo hayo, "alisisitiza Waziri huyo.


Aliongeza kuwa Serikali ina wajibu wa kutekeleza mazingira mazuri ikiwa kwa sasa maendeleo mazuri  ya Sayansi na teknolojia ni vyema kuwe na uwezekano wa kaona namna ambavyo tasnia ya habari inasaidia jamii kwa kuona fursa kwenye mabadiliko hayo.

Alisema kutokana na siku hiyo ya uhuru wa vyombo vya habari na kuwasilishwa kwa mada tofauti tofauti wanahabari watapata uelewa juu ya Sheria mbalimbali zinazogusa sekta hiyo nchini,mijadala na uelewa wa Sheria mbalimbali zinazogusa tasnia ya habari hasa sheria za huduma za habari ya mwaka 2016 pamoja na kanuni zake.


"Hapa nchini kwetu sheria zinatungwa na bunge nichukue nafasi hii kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Tulia Aksoni kwa utayali wake alionieleza kuwa wanasubiri tukamilishe... leteni tufanye mabadiliko ili tasnia ya habari iende kwa kasi, hivyo bunge lipo tayari sisi tukamilishe kwani bunge letu lina kazi ya kutunga na kufuta sheria zinazo kwaza ukuaji wa sekta mbalimbali, "alisema Waziri huyo.


Alisema anatumaini waandishi hao watatumia fursa nyingi katika kujadili na kutafuta njia bora za  kushughulikia na kukabiliana na changamoto zinazowakumba huku wakiainisha fursa zilizopo katika kuendeleza  sekta ya habari barani Afrika.


Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo Jimmy Yunaz alisema kupitia mkutano huo sekta ya habari inaendelea kuchangia ukuaji wa uchumi na kuchagiza uhuru wa Vyombo vya habari Duniani.


"Sekta ya habari inaendelea kuchangia vyema katika ukuaji wa uchumi wa nchi na pato la taifa kupitia mitandao ya kijamii," alisema

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) ,Rose Reuben alisema uandishi wa habari ni jambo linalogusa jamii na kuleta maendeleo katika jamii na nchi kwa ujumla.


Alisema kwa sasa wapo kuangalia ukuaji wa teknolojia unavyokuwa kwa kasi,huku wakiangalia changamoto zinazowakumba waandishi wa kike katika kazi zao na kuzifanyia kazi.


Mkurugenzi huyo alisema kwa sasa wanapaswa kubadilika maana uandishi wa zamani umepitwa na wakati na wanapaswa kuandika habari kwa ajili ya mabadiliko ya taaluma yao wenyewe,jamii,na nchi kwa ujumla.


Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Abubakar Harssan alisema dunia imebadilika na vitu vingi vimehamia kwenye mitandao ya kijamii hivyo amewataka waandishi wote kutumia vyema mitandao hiyo ili kufanya jamii ikawa na uelewa mpana wa kile kinachoendelea na kuweza kupata mambo muhimu ya kihabari.

Share:

GGML YAIBUKA MSHINDI MAONESHO YA AFYA NA USALAMA MAHALA PA KAZI


Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia masuala ya afya, usalama, mazingira na mafunzo Dk. Kiva Mvungi akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (katikati), kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri kutoka OSHA, Dk. Adelhelm James Meru. GGML imeibuka mshindi wa jumla katika maonyesho ya usalama na afya mahala pa kazi jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Prof Joyce Ndalichako (katikati) akifurahia jambo na wafanyakazi wa Geita Gold Mine alipotembelea banda lao katika maonyesho ya usalama na afya mahala pa kazi jijini Dodoma.Pembeni yake ni Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Patrobas Katambi

 

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeibuka mshindi wa jumla katika maonesho ya afya na usalama mahala pa kazi jijini Dodoma.

 

Maonesho hayo ya afya na usalama mahala pa kazi yameratibiwa na Wakala wa Afya na Usalama Mahala pa Kazi nchini (OSHA) jijini Dodoma katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi ambayo huadhimishwa duniani Aprili 28 kila mwaka.

 

Pia OSHA wameipatia pia GGML tuzo ya kampuni bora inayoifikia zaidi jamii katika

uelimishaji wa masuala ya afya na usalama

kwenye maeneo yao.

 

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako ameipongeza kampuni ya GGML kwa kutoa kipaumbele kwenye afya na usalama wa wafanyakazi na kutoa wito kwa kampuni nyingine nchini kuwekeza katika kuboresha mazingira ya afya na usalama wa wafanyakazi wao.

 

“Waajiri wengi nchini hawatoi msisitizo kwenye masuala ya afya na usalama kwa sababu ya kuogopa gharama. Lakini linapokuja suala la ajali na vifo, gharama huwa ni kubwa zaidi na kuwaathiri waajiri wenyewe, kampuni, wafanyakazi, jamii, taifa na uchumi kwa ujumla.

 

“Tuendelee kushirikiana kujenga utamaduni bora wa afya na usalama mahala pa kazi kama kauli mbiu ya siku ya afya na usalama mahala pa kazi mwaka huu inavyosema,” aliongeza Profesa Ndalichako.

 

Aidha, Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia masuala ya afya, usalama, mazingira na mafunzo Dk. Kiva Mvungi alisema siri ya kampuni ya GGML kuibuka kidedea katika masuala ya afya na usalama kwa muda mrefu ni kuwa na utamaduni bora wa kushirikisha wafanyakazi na wakandarasi katika kuenzi tunu ya afya na usalama mahala pa kazi.

 

“Changamoto ya ajali na vifo mahala pa kazi ni suala linaloathiri wafanyakazi wengi duniani pamoja na familia zao. Tumejitahidi kuzuia vifo na ajali katika mgodi wetu ndiyo sababu hatujapata ajali ya kuondoa maisha ya mfanyakazi ndani ya mgodi kwa zaidi ya miaka 10 hivi sasa.

 

“Mara ya mwisho mtu kupata majeraha yaliyomzuia kuendelea na kazi ilikuwa mwaka 2018 wakati mwaka 2017 tulipata tukio moja la mtu kupata jeraha dogo lilomzuia kuendelea na kazi.

 

“Hii kwetu ni rekodi nzuri ukilinganisha na migodi mingine na tunaendelea kuwaelimisha wafanyakazi wetu kuendelea kuwa makini na kufuata taratibu zote za usalama wanapokuwa kazini ili tuhakikishe tunaendelea na rekodi yetu ya kuwa mgodi kinara katika kuzingatia usalama kuliko migodi yote duniani,”alisema Dk. Kiva Mvungi.

 

Alisema miongoni mwa kampuni zote za AngloGold Ashanti ambayo ni kampuni mama ya GGML imeendelea kuwa kampuni bora ya kwanza inayozingatia usalama kwa kiwango kikubwa.

 

Ameongeza kuwa kampuni ya GGML inathamini maisha ya wafanyakazi na wakandarasi wake na ndiyo maana imeweka suala la usalama kuwa kipaumbele chake cha kwanza katika shughuli zake.

 

“Tumekuwa tukishirikiana na OSHA kila mwaka kuielimisha jamii na taasisi zinazoshiriki katika maonesho haya mifumo na teknolojia za kuboresha afya na usalama sehemu zetu za kazi.

 

“Lengo ni kuikumbusha jamii kuwa maisha na uhai ni jambo la msingi kuliko hata uchumi au faida ambayo inaweza kuzalishwa na kampuni,” alisema Dk Kiva Mvungi.

 

Katika maonesho ya afya na usalama mahala pa kazi mwaka jana, GGML iliibuka mshindi wa pili.

 

Mapema mwaka huu, GGML iliibuka mshindi wa jumla katika kampuni zinazofanya vizuri kwenye sekta ya madini nchini Tanzania kwa mwaka wa fedha 2020/2021 baada ya kunyakua tuzo katika vipengele vya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii, mazingira, usalama, mlipaji bora wa mapato (kodi) na uendelezaji wazawa, ikiwa ni mara ya pili mfululizo.

Xxxxxx

 

CAPTION

 

 

4.

Share:

Picha : NAPE NNAUYE AFUNGUA MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI... ATEMBELEA BANDA LA MISA - TAN MAONESHO YA KIHABARI


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akisoma kipeperushi katika banda la Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'. Kulia ni  Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Bi. Salome Kitomari akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na MISA - TAN. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akisoma kipeperushi katika banda la Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. Wa kwanza kulia ni Afisa Habari na Utafiti wa MISA TAN, Bi. Neema Kasabuliro
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akifurahia jambo katika banda la Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha wakati akifungua Maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'. Wa pili kulia ni  Mwenyekiti wa  MISA-TAN Bi. Salome Kitomari akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na MISA - TAN. Wa kwanza kulia ni Afisa Habari na Utafiti wa MISA TAN, Bi. Neema Kasabuliro
Kulia ni  Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Bi. Salome Kitomari akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na MISA - TAN kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kushoto).
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akifurahia jambo katika banda la Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani  leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani  leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani  leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kitaifa Mei 3,2022 jijini Arusha.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

MAXENCE MELO: DIJITALI INACHOCHEA MAMLAKA KUCHUKUA HATUA MAPEMA


Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo



Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo amesema Dijitali imetoa fursa kwa Maudhui ambayo huenda yasingekuwa rahisi kuruhusiwa na Mhariri au Chombo cha Habari.


Ameeleza hayo Mei 01, 2022 katika Mjadala kuhusu Vitisho vya Kidijitali kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari uliofanyika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.


Akizungumza kwenye Mjadala huo amesema kuna uoga wa mabadiliko kwenye safari ya Dijitali "Najua kuna uoga wa mabadiliko, na changamoto kubwa anayoona ni digitali imekuwa ikidhibitiwa kisiasa".




Vilevile akizungumza Mjadala mwingine kuhusu Mikakati na Mbinu za kupambana na ufuatiliaji wa kidijitali, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums amesema katika dunia ambayo Nchi haiweki Sheria ya Faragha, utu wa watu wake unaweza kuwa matatani.


Amesisitiza Utu katika ulimwengu wa kidijiti ni wa kupigania kwa nguvu zote, akisema JamiiForums kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali inaendesha mafunzo ya usalama wa kidijiti.


Amesema "JamiiForums ni rafiki mkubwa wa Wanahabari na tunaahidi kufanya mafunzo haya kwa Waandishi wa Habari"



Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mwaka 2022 yanayobeba Kaulimbiu isemayo, "Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti" yatahusisha Wadau wa Tasnia Habari kutoka ndani na Nje ya Nchi.



Kilele chake ni Mei 03, 2022 na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.
Share:

Sunday 1 May 2022

TUCTA WATAKA KIMA CHA CHINI MISHAHARA IWE MILIONI MOJA NA ELFU 1O


Hery Mkunda, Katibu Mkuu TUCTA

Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Hery Mkunda amesema TUCTA imependekeza kiwango cha kima cha chini cha mshahara kwa mwezi kiwe shilingi milioni moja na elfu kumi.

Mkunda ameyasema hayo leo Mei Mosi, 2022 wakati wa hotuba yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgeni rasmi katika sherehe hizo za siku ya wafanyakazi ambayo yamefanyika kitaifa mkoni Dodoma katika uwanja wa Jamhuri.

Mkunda amesema licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzitekeleza hoja mbalimbali za wafanyakazi ikiwemo punguzo la makato ya kodi, kupandisha madaraja, bado TUCTA inapendekeza kuongezewa mishahara walau shilingi milioni Moja na elfu kumi kama kima cha chini.

"Kauli yako ya 2021 ulisema 'Mimi ni Mama, na Mama ni mlezi', hivyo mama tuna imani na matarajio makubwa juu ya ile ahadi uliyotoa kuhusu kutupandishia mishahara wafanyakazi wote Tanzania, mishahara walau iwe shilingi milioni Moja na elfu kumi kama kima cha chini. TUCTA tunapendekeza, bila shaka hotuba yako leo itakuwa tiba sahihi"- Hery Mkunda, Katibu Mkuu - TUCTA.

CHANZO - EATV
Share:

HUYU NDIYO BILIONEA ALIYEUNUNUA MTANDAO WA TWITTER KWA FEDHA ZA KUFURU


Elon Musk.

MIONGONI mwa habari zilizoshtua Dunia mapema wiki hii ni kuhusu mtu anayeitwa Elon Musk kuununua Mtandao wa Twitter kwa pesa za kufuru.

Amefikia makubaliano ya kuinunua Twitter kwa pesa taslim Dola za Kimarekani bilioni 44.Wengi wameshtushwa na kiasi hicho cha pesa hivyo kujiuliza huyu Elon Musk ni nani hasa?


Huyu ni mtu tajiri mno duniani ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tesla inayotengeneza magari ya umeme yaliyopata soko kubwa kwa sasa duniani.

Mei 30, 2020 ilikuwa ni siku ya kukumbukwa katika historia ya sayansi ya anga, astronomy duniani kote na hiyo ilikuwa ni baada ya kufanikiwa kwa chombo maalum kiitwacho Falcon 9 kuwapeleka salama wanasayansi wawili, Doug Hurley na Bob Behnken kwenda kwenye kituo cha anga cha kimataifa, International Space Station.



Waliowezesha safari hiyo ya kihistoria, ni kampuni ya Space X inayomilikiwa na Elon Musk! Ndiyo, Elon Musk, mfalme wa sayansi ya kizazi kipya.



Sasa; kwa nini Elon Musk anatukuzwa kama mfalme wa sayansi ya kizazi kipya? Kwa taarifa yako, jamaa anatisha kwelikweli kwenye ubunifu wa hali ya juu wa kisayansi, pengine kuliko binadamu mwingine yeyote aliyewahi kuishi duniani.

Falsafa kuu ambayo imekuwa ikimuongoza, ni kuibadili Dunia na hiyo imemfanya kutajwa kuwa miongoni mwa watu wachache wenye akili, wanaoishi katika karne ya 21.

Amezaliwa Juni 28, 1971 kutoka kwa baba yake, Errol Musk, mhandisi na tajiri mkubwa kwa wakati huo, raia wa Afrika Kusini na mama Maye Musk, mwanamitindo mwenye asili ya Canada, alipewa jina la Elon Reev Musk FSR.

Hiyo ilikuwa ni Pretoria nchini Afrika Kusini, ambako baba yake alikuwa akifanya kazi za uhandisi wa vifaa vya kielektroniki, rubani na nahodha. Hapo ndipo safari ya maisha ya Musk ilipoanza, akilelewa pamoja na kaka yake, Kimbal na dada yake, Tosca.

Katika umri wake wa utoto, inaelezwa kwamba Musk alikuwa akipenda kucheza peke yake, akiwa kimya kabisa kiasi kwamba kuna wakati wazazi wake walihisi kwamba pengine alikuwa na matatizo ya kusikia, akapelekwa kwa daktari kufanyiwa uchunguzi lakini hakubainika kuwa na tatizo lolote.


Alianza shule, lakini akakutana na changamoto nyingine! Licha ya uwezo wake mkubwa darasani, Musk alikuwa na umbo dogo kuliko watoto wengine wa umri wake, alikuwa mkimya na alipenda kujisomea vitabu, jambo lililosababisha awe anaonewa.

Wakati f’lani amewahi kupigwa na kundi la watoto wenzake, wakamsukumia kwenye ngazi alikoporomoka na baadaye kupoteza fahamu.


Alipofikisha umri wa miaka 10, wazazi wake walitengana, akachukuliwa na mama yake na kwenda nchini Canada.

Ni katika kipindi hicho, alianza kuonesha mapenzi kwenye elimu ya kompyuta, akawa anajifunza mwenyewe mambo mbalimbali ikiwemo programming na alipofikisha umri wa miaka 12, tayari alikuwa na uwezo wa kutengeneza program mbalimbali za kompyuta.


Akafanikiwa kutengeneza gemu akiwa na umri wa miaka 12 na kuvunja rekodi ya mtaalam wa kompyuta mwenye umri mdogo zaidi baada ya kugundua video-game iliyopewa jina Blastar.


Alipofikisha miaka 15, alichoshwa na uonevu wa wanafunzi wenzake, akaamua kuanza kujifunza kareti na miereka, sasa akaanza kuwa tishio miongoni mwa waliokuwa wakimuonea.


Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Queen’s University. Miaka mitatu baadaye, alihamia nchini Marekani alikokwenda kujiunga na Chuo Kikuu cha Pennsylvania ambako alifanikiwa kuhitimu masomo ya Fizikia (Physics) na biashara.


Hizo ndizo zilizokuwa ndoto za Musk, kwenda kusoma Marekani. Baada ya kuhitimu Chuo Kikuu cha Pennsylvania, alijiunga na Chuo Kikuu cha Stanford, nacho cha Marekani, lakini baadaye aliamua kuachana na masomo ya chuo ili atimize ndoto kubwa zaidi.


Inaelezwa kwamba kipindi anaacha chuo, tayari alikuwa amefungua kampuni yake ya Zip2 Corporation kwa kushirikiana na kaka yake na hakuacha chuo ili akazurure, aliacha ili apate muda wa kuisimamia kampuni hiyo.


Kampuni aliyoifungua na kaka yake, Zip2 Corporation, ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuwezesha malipo ya kimtandao! Ni katika kipindi hicho cha mwishoni mwa miaka ya tisini, ndipo matumizi ya kompyuta yalipoongezeka.


Watu wengi walikuwa wakitaka kununua vitu mtandaoni na hakukuwa na mfumo ambao ungerahisisha kazi hiyo, lakini kwa Elon Musk na kaka yake ilikuwa ni fursa ya kupiga pesa.


Hilo lilifanikiwa kwa sababu Kampuni ya Zip2 iliwezesha wateja kuwa na uwezo wa kulipia bidhaa mbalimbali mtandaoni, jamaa wakaanza kuogelea kwenye utajiri ndani ya muda mfupi.


Baadaye Elon Musk aliamua kuuza hisa zake katika Kampuni ya Zip2, pesa alizozipata akaanzisha kampuni nyingine ambayo ilikuwa ikihusika na miamala ya kielektroniki, X.com.


Kampuni hiyo ilikuja kubadilisha mfumo wa utendaji kazi na jina na hapo ndipo ilipozaliwa PayPal; mtandao mashuhuri duniani wa kufanya manunuzi.

Jamaa aliendelea kutengeneza pesa ndefu, baadaye akaja kuiuza PayPal kwa kampuni nyingine kubwa, eBay kwa gharama ya Dola za Kimarekani, bilioni 1.5 (zaidi ya shilingi trilioni 3.5 za Kitanzania).


Inaelezwa kwamba mkwanja huo sasa ulimpa nguvu Musk ya kuibadili dunia kadiri awezavyo na hapo ndipo miradi mikubwa ya mabilioni ya pesa yalipoanza kutekelezwa, ikiwemo kutengeneza roketi, kurisha satelite, kutengeneza magari ya umeme na kufuru nyingine nyingi anazoendelea kuzifanya.

Mwaka 2002, Elon alianzisha kampuni nyingine ya SpaceX, ambayo mwanzo wa makala haya nimekueleza kwamba ndiyo iliyofanikisha safari ya kwanza binafsi kwenda kwenye kituo cha anga za juu cha kimataifa, International Space Station.


Pia mwaka 2003, Musk alianzisha kampuni nyingine ya Tesla Motors ambayo baadaye ilibadilishwa na kuwa Tesla Inc. Kwa taarifa yako, kampuni hii ni miongoni mwa kampuni zinazoongoza kwa ugunduzi wa teknolojia mpya duniani.

Tesla ndiyo waliogundua magari ya kisasa yanayotumia umeme, ndiyo waliogundua magari yanayojiendesha bila dereva, ndiyo waliogundua treni yenye kasi ya ajabu, Hyperloop na mengine mengi.


Ni Elon Musk huyu ndiye ambaye baada ya kuchoshwa na foleni za magari kwenye miji mikubwa, alikuja na wazo jipya, la kutengeneza barabara za chini ya ardhi, kupitia kwa kampuni yake ya The Boring Company.

Bila shaka sasa umeanza kumuelewa Elon Musk, lakini hiyo ni kama tone tu ndani ya bahari, ana mengi.

Sasa; jamaa ameinunua Twitter na anasema anataka kuona Twitter ina uwezo wake wa ajabu na hata hataki kutengeneza pesa kwa njia ya Twitter. Anazo za kutosha tayari na anaweza kuwa na vipaumbele tofauti vingine vya kumpatia pesa.

Makala; Hash Power na Mtandao
Share:

MTOTO WA MBUNGE ALIYEZIKWA JUZI AFARIKI DUNIA





Marehemu Irene Ndyamkama
Mtoto mchanga aliyeachwa na marehemu Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rukwa Irene Ndyamkama, amefariki dunia jana Aprili 30, 2022, baada ya kuishi kwa siku saba.

Mbunge Irene alifariki dunia Aprili 24, 2022, katika hospitali ya Tumbi wakati akipatiwa matibabu na alizikwa Aprili 29 mwaka huu kijijini kwa mama yake Isinde, Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger