Thursday 24 February 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARI 25,2022


Magazetini leo Ijumaa February 25,2022















Share:

WAMILIKI WA ARDHI WAPEWA SIKU 60 KUKAMILISHA KULIPA KODI YA PANGO LA ARDHI


Afisa ardhi mkuu , wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Biswalo Makwasa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwajibika kulipa kodi huku akitoa Siku 60 kukamilisha zoezi hilo.
Mkuu wa kitengo cha kodi,Wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Denis Mesemu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwakumbusha Watanzania kulipa kodi ya pango la ardhi Kwa mujibu wa sheria.

Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 Blog-DODOMA.

WIZARA ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi inawataka wamiliki wa ardhi kote nchini kujua wajibu wao kisheria wa kulipa kodi ya pango la ardhi  huku ikitoa siku 60 kwa wale ambao hawajalipa kodi hiyo na waliopimiwa viwanja kuwasilisha maombi ya kumilikishwa na wasipofanya hivyo  Serikali itachukua hatua za  kisheria.

Hayo yameelezwa leo 24 Februari,2022 na Afisa Ardhi Mkuu kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Biswalo Makwasa wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu umiliki ardhi kwa viwanja vilivyopimwa pamoja na ulipaji wa kodi ya pango la ardhi.

Amesema,wamiliki wa ardhi wanapaswa kujua wanawajibika kisheria kuwasilisha maombi ya kumikikishwa Ardhi kwa Kamishna wa Ardhi na kusisitiza kuwa kinyune na hapo itatolewa adhabu ya  kufuta umiliki,kupiga mnada na kumilikisha viwanja  vilivyopimwa kwa wananchi wengine wenye uhitaji.

“Wizara inatoa muda wa siku 60 kuanzia tarehe 5 mwezi wa pili 2022 ya kuhakikisha wale walipopimiwa viwanja wanawasilisha maombi  ya kumilikishwa  na wale wenye milki za ardhi wawe wamelipa kodi ya pango la ardhi,

Kila mmiliki wa ardhi anakumbushwa wajibu  wa kisheria kulipa kodi ya pango la ardhi,nisisitize TU kwamba zoezi la kufuta umiliki Kwa kutokidhi vigezo litaanza rasmi 6 Aprili,2022,"amesema

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Kodi,Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Denis Mesamu  ametoa rai kwa watanzania kulipa kodi ya pango la ardhi kwa njia ya kieletroniki kwa kutumia simu  kwani ni rahisi na ni rafiki.

Amesema ili kuboresha sekta hiyo,Serikali kupitia Wizara hiyo imefanya jitihada za kumfikia mwananchi moja kwa moja kupitia kituo cha huduma kwa wateja na kuondoa usumbufu wa ufuatiliaji wa masuala ya ardhi,kutunza kumbukumbu za wateja kielektroniki na kuwawezesha wananchi kupata taarifa zao kwa urahisi.

"Kodi ya pango la ardhi inakusanywa na Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia mifumo ya Kieletroniki hivyo niwaombe wananchi wote wanaodaiwa kodi hiyo walipe kwa wakati kwani ni sheria na wajibu,"amesisitiza Mkuu huyo wa kitengo cha kodi,Wizara ya ardhi .

Licha ya juhudi hizo ameeleza kuwa bado kumekuwa na changamoto kwa watanzania kushindwa  kutofautisha kati ya  kodi ya pango la ardhi na kodi ya majengo  ambapo amesema kodi ya majengo  inakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kwa sasa  inakusanywa kupitia luku kwenye umeme.

Akieleza mikakati ya Wizara hiyo amesema ina mkakati wa kwenda nyumba kwa nyumba kuhakikisha kila kipande cha ardhi kinachodaiwa kinapelekewa hati ya madai ambapo amedai hali hiyo inaleta tija na hamasa.

"Kwa Mkoa wa Dodoma ulipaji wa kodi ya ardhi umeongezeka ambapo katika kipindi cha Disemba mwaka jana wiki mbili za kwanza ulipaji wa kodi ulikuwa wamiliki 200 lakini baada ya kuanza zoezi la kupeleka hati za madai walifika mpaka 800 kwa wiki na mapato yalitoka shilingi milioni 40 kwa wiki mpaka milioni 102,"amesisitiza.

Pamoja na mambo mengine ameeleza mipango endelevu ya ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi kwa mwaka na kueleza kuwa wamejiwekea malengo ya ukusanya shilingi bilioni 221 kwa mwaka ambapo makusanyo yaliyopo kwa sasa ni bilioni 81.2.

Share:

BARRICK YATANGAZWA KINARA WA KULIPA KODI KATIKA SEKTA YA MADINI NCHINI


Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi tuzo ya Mlipa kodi mkubwa katika sekta ya madini, Meneja wa Barrick nchini Georgia Mutagahywa wakati wa hafla ya usiku wa mlipa kodi, kushoto ni Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko.

***
Kampuni ya madini ya Barrick Gold Corporation,imetangazwa kuwa kampuni inayoongoza kuchangia pato la Taifa katika sekta ya madini nchini katika kipindi cha mwaka 2021 na imetunukiwa tuzo ya mlipa kodi bora.

Tuzo hiyo ilitangazwa na kutolewa wakati wa hafla ya Usiku wa Madini ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne nchini, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo pia ilihudhuriwa na viongozi wa Serikali na wadau kutoka katika sekta ya madini.

Barrick ni mchangiaji mkubwa katika wa pato la Serikali kupitia ulipaji wa kodi mbalimbali na mdau mkubwa wa kuchagia uchumi wa kijamii kupitia mtandao wa biashara zake, pia imekuwa mstari wa mbele kufanikisha miradi ya kusaidia jamii katika maeneo yanayozunguka migodi yake ya Bulyanhulu,Buzwagi na North Mara.

Akizungumza na vyombo vya habari vya hapa nchini karibuni, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Mark Bristow alisema kampuni imetumia zaidi ya dola bilioni 1.8 katika kodi, mishahara na malipo kwa wafanyabiashara wa ndani. Pia imewekeza dola milioni 6.7 katika miradi ya elimu katika jamii, afya na miundombinu.

Migodi pia iliendelea kuajiri na kuwapatia ujuzi Watanzania. Asilimia 97% ya wafanyakazi ni watanzania , huku 41% wakitoka katika vijiji vinavyoizunguka. Pia imeimarisha ushirikiano na wazabuni wa ndani.

Mbali na Tuzo ya Mlipa kodi bora,kampuni imetunukiwa tuzo mbalimbali.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi moja ya tuzo hizo Meneja Uhusiano wa Barrick  Neema Ndossi kwa niaba ya kampuni katika hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Barrick wakifurahia tuzo mbalimbali ambazo kampuni imejishindia.

Share:

WADAU WAOMBA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII KUFUNGUA TAWI LAKE MIKOA YA KUSINI



Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt Shogo Mlozi Sedoyeka akizungumza na wadau wanaoshiriki mafunzo ya watoa huduma katika mnyororo wa Sekta ya Utalii yanaofanyika kwa siku tano Songea Mkoani Ruvuma. Dkt. Sedoyeka amewatembelea wadau hao kujionea shughuli za ufundishaji zinavyoendela na kupata maoni yao kuhusu mafunzo hayo.
Mzee Richard Charles mshiriki wa mafunzo hayo akiwasilisha maoni yake kuhusu mafunzo hayo.
Mshiriki wa Mafunzo Tulahigwa Kaduma akiwasilisha maoni yake kwa Chuo Cha Taifa cha Utalii.
Anthony Masebe Mshiriki wa Mafunzo hayo kutoka Mamlaka ya Usimamizi wanyamapori Tanzania (TAWA) akitoa ufafanuzi kuhusu vibali vya kuanzisha mabucha ya wanyamapori. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)


Na: Hughes Dugilo, SONGEA.

Wadau wanaoshiriki mafunzo ya watoa huduma katika mnyororo wa Sekta ya Utalii yanayoendelea Katika Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wamekiomba Chuo cha Taifa cha Utalii kufungua Tawi lake Katika ukanda wa kusini ili kutoa fursa kwa vijana wa maeneo hayo kupata Elimu na ujuzi katika fani mbalimbali ikiwemo ya Utalii.

Wadau hao wametoa maombi hayo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka alipowatembelea na kuzungumza nao kwa lengo la kupata maoni yao kuhusu mafunzo hayo.

Dkt. Sedoyeka amewaeleza wadau hao nia njema ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika mapambano dhidi ya UVIKO 19 na kwamba mafunzo hayo yanalenga kusaidia Sekta hiyo kwa kuhakikisha kila mdau anapata uelewa sahihi wa namna ya kukabiliana na janga hilo.


"Ndugu zangu nimekuja kuwatembelea kuona vile mnavyopata mafunzo haya, lakini pia kupata maoni yenu kuhusiana na mafunzo haya", amesema Dkt. Sedoyeka.

Aidha amesema kuwa amefurahishwa na mwitikio mkubwa wa wadau hao waliofika kushiriki mafunzo hayo kutoka Katika Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma, na kwamba ana imani kubwa mafunzo hayo yatawawezesha kufanya shughuli zao kwa kuzingatia kanuni za kujikinga na UVIKO 19.


Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Kwa wakati tofauti wametoa maoni yao kwa Serikali kupitia Chuo cha Taifa cha Utalii chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.


Tulihigwa Kaduma ni mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Songea amekipongeza Chuo hicho kupeleka mafunzo Mkoani humo huku akiomba uongozi wa Chuo hicho kufungua Tawi lake Katika mikoa ya kusini ili kutoa fursa kwa vijana wao kupata Elimu ya Mambo mbalimbali katika Sekta hiyo.


"Niombe pia uongozi wa Chuo mfungue Tawi lenu huku kusini kwani kwa kufanya hivyo mtakuwa mmewasaidia vijana wetu kupata Elimu Katika fani hii"


Na kuongeza kuwa "Lipo jambo lingine tulikuwa tunaomba mtusaidie kupata vibali vya kuwezesha uwepo wa mabucha ya wanyamapori ili wadau waliopo kwenye Sekta hiyo waweze kupata kipato" aliongeza Tulahigwa, huku Dkt. Sedoyeka akimkaribisha Afisa Mhifadhi wa Mkoa wa Ruvuma kutoka Mamlaka ya Usimamizi wanyamapori Tanzania (TAWA) Anthony Masebe kulitolea ufafanuzi.


Katika hatua nyingine akizungumza kwenye mahojiano maalum Mratibu wa Mafunzo hayo Mkoa wa Ruvuma Elina Makanja amesema kuwa mafunzo hayo yanaendelea vizuri katika Mkoa huo na kwamba kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa wadau hao ambapo jumla ya washiriki 124 kutoka katika Wilaya zote za Mkoa huo wanashiki Mafunzo hayo.


"Kwakweli mafunzo haya yanakwenda vizuri sana tumepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau wetu na maudhurio ni mazuri sana, washiriki wanauliza maswali na kunakuwa na majadiliano ya pamoja katika kila mada kwakweli tunakwenda vizuri sana" Amesema Elina.


Mafunzo hayo ya siku tano yanaendelea Mkoani Ruvuma ikiwa ni muendelezo, ambapo pia yanatolewa katika mikoa nane ikijumuisha Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Mara na Mwanza. Ambapo mpaka sasa mafunzo hayo yamekamilika katika mikoa ya Lindi na Mtwara, na sasa yanaendelea katika mkoa wa Ruvuma na Njombe.


PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO KATIKA MAFUNZO HAYO.
Msimamizi wa mafunzo katika Mkoa wa Ruvuma na Mkufunzi Mwandamizi wa masomo ya Lugha na ujuzi wa Mawasiliano wa Chuo cha Taifa cha Utalii Elina Makanja akifundisha somo la masiliano ya kitaalamu Katika utoaji wa huduma za utalii na Ukarimu kwa wadau wa sekta ya utalii Mkoani Ruvuma.
Mkufunzi kutoka chuo cha Taifa cha Utali Zara Mwanga akifundisha somo la usafi mahala pa kazi.

Share:

MKAZI WA MTONGANI ASHINDA MILIONI 10 ZA BIKO

Meneja wa Bank ya CRDB Tawi la Palm Beach Primier jijini Dar es Salaam, Pendo Kitula kulia akishirikiana na balozi wa Biko Kajala Masanja kushoto kumkabidhi mshindi wao wa biko Ahmad Ally Mbwana jumla ya sh milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili. Picha na Mpigapicha Wetu.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kushoto akifurahia jambo na mshindi wake Ahmad Ally Mbwana aliyeshinda sh milioni 10 za bahati nasibu ya Biko na kukabidhiwa jana kwenye Bank ya CRDB, Tawi la Palm Beach Primier, jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Biko wa sh milioni 10, Ahmad Ally Mbwana, akionesha tabasamu pana baada ya kuibuka kidedea kwenye droo kubwa ya biko iliyofanyika Jumapili. Picha na Mpiga picha wetu.


Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkazi wa Mtoni Mtongani, wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam, Ahmad Ally Mbwana, ameibuka Milionea wa biko baada ya kushinda sh milioni 10 za droo kubwa inayofanyika kila Jumapili kwa kucheza live kwa kuingia www.biko.co.tz au kwa namba ya Kampuni ya 505050 na kumbukumbu namba 2456.


Biko ni mchezo unaochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unachezwa kwa kufanya miamala kuanzia sh 1000 na kuendelea ambapo Watanzania wamekuwa kuanzia sh 2500 hadi Milioni 5 papo kwa hapo pamoja na droo kubwa za kila Jumapili.


Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.
Share:

WATUMISHI SITA WAFUKUZWA KAZI HALMASHAURI YA SHINYANGA


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 23,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy. Wa Kwanza kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Christina Mzava akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Isaack Sengelema.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga limewafukuza kazi Watumishi Sita kutokana na makosa mbalimbali ya kiutumishi.

Uamuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 23,2022.

Mboje amesema Baraza la Madiwani limewafukuza watumishi hao baada ya kupitia utetezi wao na baadhi yao hawajaonekana kutokana na kutokuwepo kwenye maeneo yao ya kazi.

“Baraza la Madiwani limewafukuza kazi watumishi sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kutoka Idara ya Afya watumishi wawili wamefukuzwa kazi na kutoka Idara ya Utawala waliofukuzwa kazi ni wanne”,amesema Mboje.

Mbali na watumishi hao sita kufukuzwa kazi, pia watumishi wengine wawili Baraza hilo limeagiza wakatwe asilimia 15 ya mishahara yao na watafanya hivyo kwa muda wa miaka mitatu.

Watumishi Idara ya Afya waliofukuzwa kazi ni Daktari Fidelis Benedict Mushi wa Kituo cha afya Nindo na Andrew Israel Mwakisambwe ambaye ni Mteknolojia Maabara Kituo cha Afya Salawe.

Watumishi wanne kutoka Idara ya Utawala waliofukuzwa kazi ni Maafisa Watendaji wa Vijiji ambao Charles Dominick Mayunga (Bukene), Mercy Gasper Kyando (Kilimawe), Omary Hamis Omary (Igembya) na Robert Surika Mbuti (Mwabagehu).

Soma pia : 

HALMASHAURI YA SHINYANGA YAPOKEA SH. MILIONI 900 KUPANGA, KUPIMA NA KULIPA FIDIA VIWANJA



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 24,2022














Share:

DC MBONEKO ATEMBELEA UJENZI MRADI WA RELI YA KISASA SGR

 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ametembelea kuona shughuli za maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano kutoka Mwanza hadi Isaka, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na wafanyakazi na kuzitafutia ufumbuzi, ambapo ujenzi huo unapita kwenye maeneo mbalimbali wilayani Shinyanga.


Mboneko amefanya ziara hiyo leo Februari 23,2022, akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya, pamoja na Naibu Meneja wa mradi wa Reli ya kisasa Mhandisi Alex Bunzu kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), ambao ndiyo wasimamizi wa mradi huo ambao unatekelezwa na Wakandarasi kutoka China.

Akizungumza kwenye ujenzi huo wa mradi wa Reli ya kisasa,Mboneko ameagiza vijana ambao wanatoka kwenye maeneo husika mradi ambapo unapopita wapatiwe ajira, na siyo kupewa vijana kutoka maeneo mengine.

“Mradi huu wa ujenzi wa Reli ya kisasa ujenzi unachukua muda wa miaka mitatu kukamilika, hivyo tunataka wananchi wa maeneo husika ambao wanapitiwa na mradi huu wanufaike nao ikiwamo  vijana kupata ajira, na siyo kupewa ajira vijana kutoka maeneo mengine na wakati eneo hilo la mradi kuna vijana wengi na hawana ajira,”alisema Mboneko.

“Na nyie vijana ambao mmepata ajira kwenye mradi huu wa Reli ya kisasa hasa madereva acheni wizi, sababu kumekuwa na wimbi kubwa sana la wizi wa mafuta, huko ni kuhujumu mradi huu, na ninatoa onyo la mwisho mkiiba tena mafuta tunafukuza kazi madereva wote,”aliongeza.

Alisema pia Madereva wanapokuwa wakiiba mafuta hayo na kuwauzia wananchi na kutunza ndani ya nyumba zao ni kutengeneza janga jingine, ambalo linaweza kusababisha maaafa makubwa kwa wananchi kulipukiwa na mafuta hayo.

Aidha Mboneko, aliagiza  wananchi ambao bado hawajalipwa Fidia waliopisha maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa Reli ya kisasa walipwe wote pesa zao, na kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa hakuna ambaye hatalipwa pesa yake ya Fidia bali wote watalipwa, huku akiwataka pesa hizo wazitumie kwa maendeleo ikiwamo kujenga nyumba bora.

Katika hatua nyingine Mboneko aliagiza suala la mikataba mibovu ya wafanyakazi litafutiwe ufumbuzi wa haraka, pamoja na upewaji wa chakula bora na cha uhakikisha ili kutodhoofisha Afya za wafanyakazi.

Pia aliagiza ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya wafanyakazi wa Mradi huo wa Reli ya kisasa zijengwe kwa kasi inayotakiwa na kwa kuzingatia ubora, huku akiwataka wanawake ambapo mradi huo unapita wachangamkie fursa ya kuuza vyakula kwenye ujenzi huo na kupata pesa.

Kwa upande wake Naibu Meneja wa mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu, alisema maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa wilaya watayafanyia kazi, likiwamo suala hilo la ulipwaji wa Fidia, na upewaji wa mikataba mizuri, huku akibainisha kuwa pia kuna kamati ilishaundwa ambayo itapita kukusanya maoni na malalamiko ya wafanyakazi na kutafutiwa ufumbuzi.

Bunzu aliwataka pia vijana ambao wanafanyakazi kwenye ujenzi huo wa Reli ya kisasa, wawe wazalendo na nchi yao na kuacha tabia ya wizi wa vitu mbalimbali, ambapo kumekuwa na wizi mkubwa sana, huku akisema mradi huo utakamilika 2024 wenye gharama ya Sh.Trilioni 3.062.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisikiliza malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Maskati wilayani humo, ambao wanapitiwa na mradi wa Reli ya kisasa (SGR) ambapo walikuwa wakidai hawajalipwa fidia na ukosefu wa ajira kwa vijana wao, na kuahidi kutatua malalamiko yao yote.

Naibu Meneja wa mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya na kuahidi changamoto zote zitafanyiwa kazi.

Baadhi ya wafanyakazi katika mradi huo wa Reli ya kisasa, wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko juu ya utatuzi wa malalamiko yao.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na Wakandarasi ambao wanatekeleza mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha tano, na kuwataka wazingatie maelekezo ya ajira na kufuata sheria za nchi, pamoja na kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea na ukaguzi wa maendeleo ujenzi wa Reli ya kisasa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (wapili kushoto) akisikiliza maelezo ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya wafanyakazi wa Reli hiyo ya kisasa (SGR), ambazo zipo Luhumbo wilayani Shinyanga, akitoa maelezo hayo ni Naibu Meneja wa mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akiwa na Naibu Meneja wa mradi wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu, akikagua ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa mradi huo wa Reli ya kisasa.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea.

ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea.

ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger