Saturday 23 January 2021

DC MBONEKO ATINGA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA SAKATA LA MLINZI KUPIGA MTU..AITAKA KAMPUNI YA ULINZI SUMA JKT KUCHUKUA HATUA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiondoka katika Wodi ya Wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga baada ya kumaliza kuendesha kikao cha kujadili tukio la Mlinzi wa Kampuni ya Suma JKT Guard, Geofrey Paul anayetuhumiwa kumpiga Daudi Lefi aliyekuwa akifuatilia dawa za mama yake aliyelazwa hospitalini hapo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kikao kuhusu tukio la mlinzi kupiga mwananchi aliyekuwa anahudumia mgonjwa wake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mlinzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Gofrey Paul akimshambulia Daudi Lefi kama inavyoonekana kwenye video ya tukio hilo iliyosambaa mtandaoni 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ameiagiza Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT Guard kumuondoa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Mlinzi wake Geofrey Paul anayetuhumiwa kumpiga Daudi Lefi aliyekuwa akifuatilia dawa za mama yake aliyelazwa hospitalini hapo. 

Mbali na kuagiza kuchukulia hatua za kinidhamu kwa mlinzi huyo, Mboneko pia ameitaka Kampuni hiyo kuwaondoa hospitalini hapo walinzi wanaolalamikiwa 

Mboneko amechukua uamuzi huo leo Jumamosi Januari 23,2021 wakati akiongoza kikao cha kujadili kuhusu tukio hilo lililotokea katika hospitali hiyo Januari 22,2021 kilichodumu takribani saa tatu kilichohudhuriwa na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Shinyanga, Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga pamoja na Viongozi wa Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT Guard. 

Mboneko amesema viongozi wa serikali waliona taarifa ya tukio kupitia mitandao ya kijamii na kuanza kuchukua hatua mara moja ili kubaini ukweli kuhusu tukio hilo ambapo amevipongeza na kuvishukuru vyombo vya habari vilivyoripoti kuhusu tukio hilo. 

“Tumeona tukio hili kupitia mitandao ya kijamii, kama uongozi wa serikali hatukufurahishwa na jambo hili,baada ya kuona tukio hili tulianza kupata ufafanuzi kutoka hospitalini lakini pia nilimuagiza Mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kufuatilia tukio hili ambapo tayari hospitali walikuwa wameshaanza kuchukua hatua. Kwa hiyo ikapendeza kuwa leo Jumamosi tufanye kikao kujadili tukio hili, pia tuwaita wahusika kwa maana ya Yule kijana aliyepigwa bwana Daudi Lefi na Mlinzi Geodfrey Paul aliyekuwa akimpiga,tumepata ufafanuzi kutoka pande zote mbili,uongozi wa hospitali na kiongozi wa Suma JKT Guard kanda ya Ziwa kwamba ni hatua gani wamechukua”,ameeleza Mboneko. 

"Kwa sababu tuko na mkataba na Suma JKT Guard na tukio hili limetokea kwa mara ya kwanza kutokea,tumewapa nafasi ya kutafuta walinzi wazuri na tumewaambia kwamba hatutaki kusikia tukio jingine likihusisha walinzi kuharibu taswira ya hospitali yetu. Kwa hiyo kuanzia sasa nimewaambia warekebishe", amesema. 

Amesema serikali inakemea jambo hilo na isingependa kuona linaendelea mahali popote penye hospitali zetu, zahanati na vituo vya afya na sehemu zingine na kwamba serikali inataka watu wapate huduma nzuri hospitalini. 

“Jambo hili limetokea baada ya watu hawa kupishana lugha lakini nimewaelekeza SUMA JKT Guard na Idara ya afya wahakikishe wanatoa elimu kwa watoa huduma hospitalini na walinzi wanaolinda hospitali kuhusu namna ya kuhudumia watu,namna ya kuzungumza na watu kama huyu changamoto yake ilikuwa ni kumhudumia mama yake zaidi alitakiwa kuelimishwa kuliko kupigwa”,amesema Mboneko. 

Amesema wamelikemea jambo hilo na kumwelekeza kiongozi wa SUMA JKT Guard Kanda kuchukua za kinidhamu mara moja juu ya mtumishi wao na watuletee maandishi ofisini kwangu kuhusu hatua za kinidhamu walizochukua. 

“Lakini SUMA JKT Guard wamesema wameshachukua hatua ya kumuondoa hospitalini mtumishi wao, na sisi tunasema sawa sawa. Lakini nataka na wale wote walinzi wote wanaolalamikiwa kuwa na kauli mbaya kwenye Geti letu,kwenye mapokezi pale lakini pia kwenye kuondoa watu wanaokuja kuona wagonjwa. Nimewaelekeza wawaelimishe kuliko kufukuza watu utadhani wamekuja kuiba. 

“Waliopo hapa hospitalini wanahitaji faraja zaidi, wanahitaji upendo,wamekuja kuhudumia ndugu zao lakini pia wanatoka maeneo tofauti tofauti,pengine hawana ndugu hapa Shinyanga kwa hiyo muda anaopata yeye anakuja kuhudumia mgonjwa,akija pale mtu akajieleza,asikilizwe,apewe fursa ili apate kuhudumia mgonjwa wake kwani wengine wanakuja mbio mbio baada ya hali ya wagonjwa wao kubadilika”,ameongeza Mboneko. 

Mkuu huyo wa wilaya pia amesisitiza watoa huduma na Walinzi wa hospitali kudhibiti kauli mbaya na kuepuka vijembe wa wagonjwa na watu wanaohudumia au kuona wagonjwa huku akiwataka viongozi wa hospitali kuhakikisha wanachukua hatua dhidi ya malalamiko yanayotolewa. 

“Lakini pia nimewaelekeza kutoa namba za viongozi wa hospitali na nimeelekeza pia namba zangu ziwekwe ili wananchi waweze kutoa maoni na malalamiko yao,zionekane sehemu za kuingilia, kutoka na hata kwenye wodi wanazolala wagonjwa”,amesema. 

Amewataka walinzi kutumia muda mwingi kusaidia wananchi kuwaelimisha badala ya kuwapiga na kuwatolea lugha chafu ili watoa huduma nao wapate muda mzuri wa kuhudumia wateja wao na wanaotembelea wagonjwa wapate muda wa kufariji wagonjwa. 

Amesema lengo la serikali ni kuona kila mwananchi anafurahishwa na huduma zinazotolewa kwenye vituo vya afya kwani serikali inataka kuona wananchi wanapata huduma nzuri,bora na wanakuja salama na kuondoka salama wasipate taharuki yoyote. 

“Hatutaki taharuki hospitali, hatutaki misongamano hospitali. Tunataka watu waje kuhudumiwa na sisi tutaendelea kusimamia maboresho ya hospitali yetu. 

"Tulikuwa tumepokea pia malalamiko ya watu wanakaa muda mrefu bila kuhudumiwa kutokana na foleni kwenye eneo la Control number,Mapokezi kote huko nataka waboreshe,waweke walau watu wawili wawili ili kurahisisha huduma, mtu akija atumie muda mfupi aondoke akafanye shughuli zingine za kiuchumi na kijamii”,amesema Mboneko. 

Aidha amesema hataki kuona wala kusikia watumishi wa hospitali,zahanati na vituo vya afya wanafanya kazi huku wakichati nyakati za kazi badala yake watumie muda wao kuhudumia wagonjwa na kwamba hataki kusikia mgonjwa anatoka hospitali bila kupata dawa akiambia akanunue kwenye maduka ya dawa. 

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Nuru Mpuya amesema tukio hilo lilizua taharuki hospitalini na kwamba tayari hatua zimeshachukulia na kuahidi kuwa tukio kama hilo lililofanywa na mlinzi wa Kampuni ya walinzi waliyoingia nayo mkataba halitatokea na kwamba wataboresha huduma ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu walinzi hao. 

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Shinyanga, Dkt. Luzila John Boshi amesema uongozi wa hospitali umesikitishwa na tukio hilo na kwamba kinachofuata ni kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko. 

Meneja wa Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT Guard Kanda ya Ziwa, Captain Manika Kihiri amesema mara baada ya kutokea kwa tukio hilo,hatua za awali walizochukua ni kumuondoa mlinzi huyo eneo la hospitali na kwamba watatekeleza maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga na ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kinidhamu kwani Suma JKT haipo kwa ajili ya kuzua taharuki katika jamii bali ni kuleta amani katika jamii. 

Tukio hilo limetokea Ijumaa Januari 22,2020 majira ya saa 11 na dakika 45 jioni wakati Daudi Lefi (45) akiwa katika wodi ya wanawake namba 1 ambako mama yake mzazi Victoria Lugano Mwakagari amelazwa hospitalini hapo alishambuliwa kwa kupigwa mkanda sehemu mbalimbali za mwili wake na mlinzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kutoka Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT Guard Geofrey Paul akimtaka aondoke wodini kwamba muda wa kusalimia wagonjwa umeisha. 

Akisimulia kuhusu tukio hilo, ndugu wa kijana huyo Lydia Lefi aliiambia Malunde 1 blog kuwa kaka yake alikutwa na mkasa huo wakati akiwa katika harakati za kulipia dawa za mama yao ambaye amelazwa katika hospitali hiyo Januari 21,2021 lakini jina lilikuwa halionekani kwenye Computer. 

“Kaka alikuwa alipie dawa, alipewa karatasi ya kwenda kulipia dawa, alipoenda kufuata Control number ili alipie, jina likawa halionekani kwenye Computer, ikabidi aende wodini kwa mgonjwa kuangalia/kuulizia amesajiliwa kwa jina gani,akiwa wodini hao walinzi ndipo walipoingia wodini na kumtaka aondoke kwamba muda umekwisha. 

"Walivyomtaka aondoke wodini akawaambia amekuja kuangalia jina gani mgonjwa ameandikishwa, wale walinzi wakamwambia aondoke muda huo huo, akawaomba lakini wakamwambia Huwezi kutupangia kazi. Kaka akasema nitaondokaje mama hajapata huduma ,wale walinzi wakaanza kumsukuma, ndipo mlinzi mmoja akachomoa mkanda wa suruali na kuanza kumshambulia huku mwingine akimsukuma, wakati purukushani zikiendelea baadae akaja mlinzi wa kike akasogea na kuwaachanisha”,ameeleza Lydia. 

Naye Daudi Lefi alisema mlinzi huyo alidhani amefika muda huo huo hospitalini wakati yeye alikuwa amefika hospitalini hapo muda mrefu lakini Computer za Hospitali zikawa hazisomi jina la mgonjwa wake wakati anataka kununua dawa. 

"Sikurusha ngumi kupigana kwa sababu ni eneo la hospitali, wangesema nimeenda kufanya vurugu. Walionishambulia walikuwa wawili lakini mmoja ndiyo aliyeanza kwa kunichapa na mkanda akisema nitamtambua kuwa yeye ni nani huku akinitukana,nami nikamsihi aache kutumia lugha chafu eneo la kazi",alisema Daudi. 

"Hayo yote yametokea wakati nikimweleza kuwa nimefika wodini kuulizia ndugu zangu na mgonjwa kuwa wameandikisha jina gani mapokezi kwani jina halionekani mapokezi ili nilipie dawa,wakati naendelea kushambuliwa nikamuona mama yangu mgonjwa akitoka wodini huku akihema presha imepanda akifuatilia nini kinaendelea ndipo nikaanza tena kumrudisha wodini kumhudumia nikaulizia jina aliloandikisha nikaenda kuchukua dawa nikamletea wodini", alieleza Daudi. 

Daudi alisema kutokana na kipigo hicho ameumia mkono wa kushoto ambao umevimba na kuchanika kwenye kiwiko.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kikao kuhusu tukio la mlinzi kupiga mwananchi aliyekuwa anahudumia mgonjwa wake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kikao kuhusu tukio la mlinzi kupiga mwananchi aliyekuwa anahudumia mgonjwa wake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Meneja wa Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT Guard Kanda ya Ziwa, Captain Manika Kihiri akizungumza katika kikao hicho na kueleza hatua za kinidhamu zilizochukuliwa na kampuni hiyo juu ya mlinzi aliyepiga mwananchi katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiingia katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kumjulia hali mama ambaye mwanaye alipigwa na mlinzi hospitalini hapo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa ndani ya wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Daudi Lefi akiwaelezea waandishi wa habari namna alivyoshambuliwa na Mlinzi wa hospitali
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiondoka katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiondoka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Share:

Video Mpya : MAMA USHAURI - ABEL REMIX

 Msanii wa Nyimbo za Asili Mama Ushauri kutoka Tinde Shinyanga anakualika kutazama Video yake Mpya ya Wimbo wa Abel Remix..Tazama hapa chini
Share:

WACHAWI WAAPA KUMROGA ALIYECHOMA MOTO KANISA LAO


Hii ni moja ya taarifa ambayo itakushtua sana hii leo unaposoma. 
Mambo yaligeuka mnamo Alhamisi, Januari 14,2021 mwendo wa saa kumi na moja asubuhi wakati mtu asiyejulikana aliteketeza jumba la “Halloween House” jijini New York, nchini Marekani. 

Nyumba hiyo maarufu kama House of Netherworld imejengwa eneo ambalo lilibandikwa jina Witchcraft District mjini Poughkeepsie.

Nyumba hiyo ni mahali patakatifu pa wanachama wa Kanisa la Shetani. 

Kulingana na ripoti ya polisi, kulikuwa na watu wawili ndani ya nyumba hiyo lakini wote walinusurika kifo. 

Katika video ya CCTV, mwanaume mmoja anaonyeshwa akiingia ndani ya nyumba hiyo akiwa amebeba vibuyu vya mafuta ambapo alimwagilia majengo hayo kabla ya kuwasha moto na kisha kutoroka huku akikosa kujulikana mahali alipo hadi sasa.

Katika mahojiano na gazeti la The Poughkeepsie Journal, muumini wa kanisa hilo Isis Vermouth alisema jamii itamlaani aliyechoma nyumba yao. 

“Kila mtu ameshtuka na wanaoishi karibu wana wasiwasi. Ambaye alitenda kitendo hiki atalaaniwa na kila mmoja wetu. Nahisi kama huu ulikuwa mchezo mchafu,” alisema.

 Nyumba hiyo ambayo ilijengwa na Joe Mendilloin miaka ya 1900, imekuwa ikihudumia jamii kwa muda mrefu na hivyo mkasa huo wa moto uliwakasirisha wanachama wengi. Hali ya kanisa hilo kwa sasa itawalazimu jamii kujenga jengo hilo upya.

 “Kwa sasa haijulikani ni lini jengo hilo litajengwa kwa sababu ya uharibifu mbaya wa moto," alieleza Peter Gilmore ambaye ni kuhani mkuu wa kanisa hilo. 

Gilmore pia aliongezea kuwa kanisa hilo haliabudu shetani kama ilivyokuwa ikiripotiwa kwa miaka kadhaa na hata kumfanya mmiliki wa awali Mendillo, kujitokeza hadharani na kuwaalika watoto na kuwapa peremende.
Share:

MAMA AJIUA AKIWA NA UJAUZITO WA MIEZI 9 KISA WIVU WA MAPENZI



Na Anthony Mayunga - Mwananchi
 Mwanamke mmoja amejinyonga kwa kutumia kanga kwenye mti wa mwembe katika kijiji cha Itununu wilayani Serengeti, kwa madai ya wivu wa mapenzi, huku akiwa na mimba ya miezi tisa.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu alithibitisha Mkami Nyamhanga (21) kujinyonga Januari 17 kwenye mti wa mwembe uliopo shambani.

Alisema mwili wake ulionwa na watoto waliokuwa wanakwenda kuangua matunda kwenye mwembe huo na ndio waliotoa taarifa ya kifo hicho.

Kwa mujibu wa Babu, marehemu inadaiwa alikuwa anamtuhumu mume wake kuwa na mpenzi mwingine.

”Asubuhi alitoka bila kuaga mpaka alipogundulika amejinyonga kwa kutumia kitanzi cha nguo ambayo alifunga kwenye tawi la mwembe na kuning’inia,”alisema na kuongeza:

“Mganga aliyefanya uchunguzi alibaini kuwa kifo chake kimetokana na kitanzi shingoni kilichosababisha mzunguko wa damu na hewa kukosekana, ndugu walikabidhiwa mwili kwa ajili ya kuuzika na hakuna mtu aliyekamatwa lakini uchunguzi unaendelea.’’

Mganga mfawidhi wa zahanati ya Itununu, Melick Salapioni alilieleza Mwananchi kuwa mwanamke huyo alikuwa na mimba inayokaribia miezi tisa.

Alisema kutokana na mama kujiua, alikata mawasiliano ya hewa ya oksijeni kati yake na mtoto na hivyo kusababisha kichanga hicho kufa.

Via Mwananchi

Share:

RC SINGIDA AMVUA UONGOZI MWALIMU MKUU KWA TUHUMA ZA UBADHILIFU

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na watendaji na wananchi ambapo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Singida DC  Rashid Mwandoa  kumvua cheo  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwachambia, Edward Ighonde pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi Charles Mtiko kwa tuhuma ya wizi wa vifaa vya ujenzi wa nyumba ya walimu .

Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dkt. Rehema Nchimbi akikagua ujenzi wa mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wananchi na wanafunzi.

Na Mwandishi  Wetu, Singida

 MKUU wa Mkoa wa Singida  Dkt. Rehema Nchimbi amemwagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Singida Dc Ndugu Rashid Mwandoa  kumvua cheo  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwachambia, Edward Ighonde pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi Charles Mtiko Kwa tuhuma ya wizi wa vifaa vya ujenzi wa nyumba ya walimu (Two in one).

Vifaa vinavyodaiwa kuibiwa ni mbao za kupauliwa, Saruji na nondo ambayo thamani yake bado haijafahamika.

Dkt. Nchimbi  ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo ya ujenzi ambapo watuhumiwa wote wako Polisi.

Aidha ametoa maagizo kwa viongozi kuacha tabia ya kuwatetea watumishi wanao tuhumiwa kwa ubadhilifu na atakaye bainika atashughulikiwa vilivyo.

Nchimbi amewataka viongozi wa Serikali kusimamia miradi na kuwa waminifu katika fedha zinazoletwa na Serikali ya Rais Magufuli pia wananchi wa hakikishe wanalinda mali hizo kwani miradi hiyo ni kwa ajili ya maendeleo yao.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 23,2021






























Share:

Various Posts at Musoma Utalii Training College

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

About the College Musoma Utalii Training College is a college registered by Ministry of Education, National Council for Technical Education (NACTE) and Vocational Education Training Authority (VETA). We are offering different courses as per society needs. The College is located near Bweri Bus Terminal in Musoma municipality. It is an oldest College in Lake Zone […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Many (Various) Hotel Jobs in Moshi (Kilimanjaro)

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

A new Hotel in Moshi (Kilimanjaro) is looking for a dynamic and experienced person to take the role of following vacancies – Apply free to these various Hotel job openings. Many (Various) Hotel Jobs in Moshi (Kilimanjaro) January, 2021 SOURCE: Mwananchi newspaper The deadline for submitting the application is 23 January, 2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Marketing & Sales Officer in Insurance at Speed Ways Limited

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Marketing & Sales Officer in Insurance   SPEEDWAYS LIMITED is a privately owned Insurance Agents Under Phoenix Assurance Company Limited and established in 1978, with its offices based in Dar-Es-Salaam- TANZANIA. Our mission is to serve our customers by providing them with cost- effective solutions that continually meet and exceed our customers’ expectations and provide unquestionable […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Pastry Chef at Meliá Hotels International

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Pastry Chef   Meliá Hotels International Arusha, Tanzania At Meliá Hotels International, you have the power to create your future. For us, the most important thing is your talent: We share the passion that makes you put your heart into everything you do, day after day. We are by your side to help you go […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Interns at Gwala Digital

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Interns Gwala Digital Dar es Salaam, Tanzania Gwala Digital is a digital marketing agency based in Dar Es Salaam – Tanzania. We are currently offering limited internship opportunities to passionate individuals who are willing to learn, practice and grow their skills. We are looking for people with the skills listed below: 1 – Videography 2 […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Friday 22 January 2021

Video Mpya : NYUMBU MJANJA - PEKE YANGU


Msanii Nyumbu Mjanja ameachia wimbo mpya unaitwa Peke yangu..Tazama Video hapa chini

Share:

BARAZA LA MCHELE TANZANIA (RCT) LAWAFUNDA WASINDIKAJI WA ZAO LA MPUNGA 100 KANDA YA ZIWA KULETA USHINDANI SOKO LA KIMATAIFA


Mkurugenzi mkuu  baraza la Mchele Tanzania (RCT) Winnie Bashagi akielezea kuhusu usindikaji wa zao la mpunga katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wa kusindika mchele yanayoendelea mjini Kahama.
Katibu tawala wa wilaya ya Kahama Timothy Ndanya akizungumza na baadhi ya wasindikaji hawapo (pichani) kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ambao wanaendelea na mafunzo maalumu ya kusindika mchele katika viwango vya kimataifa.
Mtafiti kutoka taasisi ya Utafiti nchini(REPOA) Steven Mombela akizungumza na wasindikaji wa zao la mpunga katika mafunzo maalumu yanayoendelea kufanyika wilayani kahama na kuhudhuriwa na washiriki 100 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wasindikaji wa zao la mpunga wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi hayupo pichani ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Kahama Timothy Ndanya.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wasindikaji wa zao la mpunga wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi hayupo pichani ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya kahama Timothy Ndanya.
**
Na Salvatory Ntandu - Kahama

Baraza la mchele Tanzania(RCT) kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti Tanzania (REPOA) wanaendesha mafunzo kwa wasindikaji wa mpunga 100 kutoka mikoa ya Geita,Shinyanga, na Tabora ili kuwajengea uwezo wa kusindika bidhaa hiyo kwa viwango vya kimataifa.

Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi mkuu wa baraza hilo, Winnie Bashagi katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasindikaji wa zao la mpunga kutoka mikoa ya kanda ya ziwa  na kusema  kuwa mchele wa Tanzania unakosa soko kimataifa kutokana na kutofungashwa kwa viwango vya kimataifa.

Alisema  zaidi ya asilimia 80 ya mchele unaozalishwa na wakulima wadogo  katika wilaya zaidi ya  64  hapa nchini unakosa sifa katika masoko ya kikanda ya jumuia ya afrika mashariki (EAC) na (SADC) kutokana kutosindikwa kwa viwango vinavyotakiwa licha ya kuwa na uzalishaji mkubwa.

“RCT na REPOA tulifanya utafiti katika wilaya zinazolima zao hili tulibaini kukosekana kwa elimu ya usindikaji,wasindikaji wengi wanachanganya madaraja,usafi,usimamizi usiridhishwa wa magahala ya kuhifadhia mpunga,matumizi yasiyosahihi ya pembejeo kwa wakulima wakati wa kuandaa mashamba,”alisema Bashagi.

Awali akifungua mafunzo hayo ya siku tatu Katibu tawala wa wilaya ya Kahama Timoth Ndanya kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack aliwataka (RCT) kufungua ofisi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wakulima na wasindikaji katika kuongeza thamani mazao yao.

“Kahama tunazalisha mpunga wa kutosha hakikisheni mnawajengea uwezo wasindikaji na wakulima wa zao hili la biashara ili kuwainua kiuchumi hakuna sababu ya wao kuendelea kukosa masoko ilihali wanamchele safi ambao unahitaji kupangwa katika madaraja yanayotakiwa kimataifa,”alisema Ndanya.

Naye Steven Mombela mtafiti kutoka (REPOA) alisema wao kwa kushirikiana na baraza la mchele wanatekeleza mradi huo ujulikanao kama Tradecom II kwa ufadhili wa jumuiya ya ulaya (EU) na waliandaa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo ili waweze kuzalisha mchele wenye viwango vinavyokidhi ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi.

“Mradi huu ni wa miaka miwili ulianza mwaka 2020 na unatarajiwa kukamilika mwaka huu,na tukimaliza kwa kanda hii tutaelekea katika kanda nyingine inayojumuisha wasindikaji kutoka mikoa ya Morogoro,Njombe,Iringa na Mbeya,”alisema Mombela.

Asha Hassan Msangi ni mmoja wa  wasindikaji wa zao mpunga kutoka Kahama ameiomba  Serikali kuboresha mazingira ya biashara ya mchele ikiwa ni pamoja na kufungua masoko ya mchele na kuwazuia wafanyabiashara wa nje kununua mpunga kwa wakulima.

Share:

SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA WATAFITI KUBORESHA TIBA ASILI NCHINI


Mratibu wa Tiba asili Mkoa wa Morogoro Dkt. Ngalula Wille wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya siku moja ya wadau wa tiba asilina bidhaa zake yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa niaba ya katibu tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo. 
Muwakilishi wa Naibu Mkamu mkuu wa Chuo upande wa Taaluma Prof. Samweli Kabote akitoa shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya hutuba yake ya ufunguzi, 
Mkuu wa Mradi wa GRILI, Dkt. Faith Mabiki ambao ndio waandaaji wa maonesho akieleza malengo ya maonsh hayo na uzinduzi wa jukwaa la ubunifu wa tiba asili Tanzania. 

Waoneshaji kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUAwakimpa maelekezo Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mhe, Fredirick Sumaye wakati akiwa kwenye banda la SUA kwenye maonesho hayo ya tiba asili. 
Mgeni rasmi na ujumbe aliofuatana nao wakitembelea mabanda ya maonesho ya waganga wa tiba asili kuona bidhaa mbalimbali waliozokuja kuonesha kwenye maonesho hayo toka mikoa mbalimbali nchini. 
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Amandus Mhairwa Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua maonesho hayo kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Prof.Raphael Chibunda. 
Picha ya Pamoja ya mgeni rasmi na viongozi wa meza kuu mara baada ya kufungua maonesho hayo. 
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mhe, Fredirick Sumaye akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa waoneshaji kutoka shirika la SAT bwana Allen alipotembelea maonesho hayo kuona bidhaa mbalimbali za wataalamu wa Tia asili.

******************

Serikali ya Mkoa wa Morogoro, na hasa vitengo vya Uchumi na Mali Asili vimewahakikishia wadau wa tiba asili kuwa wako tayari kushirikiana nao kikamilifu ili kuona kuwa mimea dawa nchini inatumika kwa uangalifu na kwa mpango endelevu.

Wito huo umetolewa na katibu tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo kwa niaba yake na Mratibu wa Tiba asili mkoa wa Morogoro Dkt. Ngalula Wille wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya siku moja ya wadau wa tiba asilina bidhaa zake yaliyofanyika mkoani Morogoro nankuandaliwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia Mradi wa GRILI.

"Hivyo tunawaahidi kuwa tutaendelea kuwa nanyi bega kwa bega kwa kusaidia jitihada za wadau wote kwenye sekta hii katika kuboresha biashara hii ya bidhaa zitokanazo na mimea dawa kwa kadri mazingira yatakavyoruhusu" Alisisitiza Dkt. Ngalula.

Mratibu huyo wa tiba asili mkoa wa Morogoro amewataka wazalishaji wa bidhaa hzo za mimea dawa kipindi hiki ambacho kuna ugonjwa wa mlipuko kama COVID-19, waone namna gani watatengeneza dawa ilikusaidia jamii kukabiliana na majanga kama haya yanayiweza kujitokeza.

"Nimefurahishwa sana na taarifa kwamba maonesho haya yamendaliwa na Chuo chetu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Kurugenzi yake ya Uzamili kitengo chake cha Uhaulishaji wa tekinolojia pamoja na mradi wa utafiti wa GRILI Hii inatokana na uzoefu na ueledi walionao kwenye masuala ya utafiti na Biashara za aina hii zikiwemo za bidhaa zinazotokana na mimea dawa hivyo ni matumaini yangu kuwa maonesho haya, yataangalia pia namna yakupunguza changamoto za uzalishaji na za kibiashara zilizopo na zinazoweza kujitokeza katika biashara nzima ya bidhaa za mimea dawa" Alisema Dkt. Ngalula.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua maonesho hayo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Amandus Mhairwa kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Prof.Raphael Chibunda amesema kuwa ingawa kwenye kanuni zabiashara ya madawa kuna mitizamo tofautikuhusu kutangaza dawa za mimea zitokanazona mimea tiba, lakini ukweli ni kwamba bilikujitangaza, wateja hawatatambua biashara za bidhaa na soko.

“Biashara hii iko pia kwenye biashara ya huduma zinakuzwa sana na watoa huduma wenyewe hivyo hii sio tu yatatangaza biashara zao bali pia yatatangaza watoa huuma wenyewe na kauli zao kwa wateja ni muhimu sana ili waweze kupata masoko ya bidhaa na huduma zao hvyo lengo la maonesho haya nikuwakutanisha wazalishaji, wasambazaji, watengenezaji na wanunuzi wa bidhaa za mimea dawa” alifafanua Prof Mhairwa.

Aliongeza"Napenda niwahakikishie wadau hawawanaozalisha dawa zinazotokana na mimeadawa kwamba, Chuo Chetu cha SUA, kupitia kurugenzi ya Uzamili, Utafiti,Uhaulishaji waTekinolojia na Ushauri wa Kitaalaamu, kwakushirikiana na Watafiti tulionao na wamasuala ya kisayansi na tekinolojia, na wale wa masuala ya biashara, tutaendelakushirikiana bega kwa bega na wajasiriamalihawa ili kuboresha bidhaa wanazozalishatukishirikiana na wadau wengine katika sektahii kwa kadri uwezo wetu utakavyoturuhusu".

Akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Ras wa Ndaki ya Sayansi za jamii na Insia Prof. Samweli Kabote kwa niaba ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Maulid Mwatawala amesema wamepokea ushauri na maelekezo yote aliyoyatoa mgeni rasmi na kuahidi kutafanyia kazi na kushirikiana nao zaidi katika kuboresha bidhaa za tiba asili kufikia viwango vya kimataifa ili kuinua uchumi wao na taifa sambamba na kuboresha afya za jamii.

Amesema maonesho hayo ni mwanzo wa maonesho ya fursa nyingi za katika tafiti za mimea dawa na tiba asili na kuwataka wataalamu wa tiba asili kuwatumia watafiti wa SUA kwenye mambo mbalimbali yanayohitaji sayansi zaidi.

Kwa pande wake Mkuu wa Mradi wa GRILI ambao ndio waandaaji wa maonesho hayo Dkt. Faith Mabiki amesema tafiti nyingi zimefanywa na watafiti wa SUA kwenye Mradi huo kwenye masuala ya miti dawa na kupata matokeo mazuri ambayo yatassidia kwenye kuongeza thamani na kuboresha tiba asili na uendelevu wake.

Dkt. Mabiki ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau wote wa Tiba asili nchini kushiriki kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Ubunifu katika tiba asili na bidhaa zake litakalofanyika kwenye Ndaki ya Solomon Mahlangu ya Sayansi na Elimu kwenye kampasi ya Mazimbu kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 7:00 Mchana.

Amesema uzinduzi wa jukwaa hilo utakuwa mwanzo mzuri wa kupata jukwaa la pamoja kati ya wadau wote wa tuba asili na wasimamaizi wa tiba asili upande wa serikali kujadiliana kwa pamoja mambo muhimu ya kuendeleza sekta hiyo ambayo imeshika kasi sana ikilinganishwa na huko nyuma kabla ya Ugonjwa wa Covid-19.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger