Tuesday 24 November 2020

SHIRIKA LA AGRI THAMANI FOUNDATION KUTOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI NCHINI

Mkurugenzi wa Agri Thamani, Mh Neema Lugangira (MB) kushoto akiwa na taulo za kike ambazo amezinunua kupitia ufadhili wa Ubalozi wa China kwa ajili ya kutoa msaada huo kwa wanafunzi wa kike wa sekondari sasa unaanza rasmi ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha watoto wa kike wanaondokana na changamoto za kukosa masomo wakati wa kipindi cha hedhi kulia ni Mama Simba ambaye ni muzaji wa taulo hizo
Mkurugenzi wa Agri Thamani, Mh Neema Lugangira (MB) kulia akikagua taulo hizo
Mkurugenzi wa Agri Thamani, Mh Neema Lugangira (MB) kulia akikagua taulo hizo
Sehemu ya taulo ambazo zimezinunuliwa na Mbunge Neema Lugangira kwa ajili ya wanafunzi
kupitia ufadhili wa Ubalozi wa China kwa ajili ya kutoa msaada huo kwa wanafunzi wa kike wa sekondar
Sehemu ya taulo ambazo zimezinunuliwa na Mbunge Neema Lugangira kwa ajili ya wanafunzi wa kike shule za Sekondari  kupitia ufadhili wa Ubalozi wa China

 MPANGO wa Asasi ya Kiraia NGOs ya Agri Thamani Foundation kutoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wa sekondari kupitia ufadhili wa Ubalozi wa China kuanza rasmi ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha watoto wa kike wanaondokana na changamoto za kukosa masomo wakati wa kipindi cha hedhi.

 Hatua hiyo inatokana na leo Mkurugenzi wa Agri Thamani, Mh Neema Lugangira (MB) kufika kwenye Kiwanda cha Kays Hygiene na kukutana Mkurugenzi  wa kiwanda hicho Mama Simba  kuangalia oda ya taulo za kike za mabinti 1,500 ilipofikia.  

 Alipoulizwa  kwanini amekuja na mradi huu na kwanini amenunua taulo za kike nchini,Mh Lugangira alisema kwamba ameamua kufanya hivyo ili kuweza kuwasaidia mabinti wa kike kuondokana na vikwazo mbalimbali ambavyo wanakumbana navyo wakiwa kwenye siku za hedhi.

 Alisema  Agri Thamani wanalengo la kuimarisha lishe kwa vijana balehe hususani wa kike na hii inajumuisha hedhi safi na salama ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao mengine ikiwemo kusoma kwa juhudi kubwa.

“Nimejionea changamoto kubwa ambao watoto wa kike wa vijijini hupata kila wanapokuwa kwenye hedhi na jinsi inavyoathiri masomo yao kupitia mahudhirio hafifu kipindi cha siku hizo”Alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha alisema ili kuimarisha ufaulu wa mtoto wa kike Agri Thamani imekuja na programu ya kumsaidia mtoto wa kike aliye sekondari na ambae ataingia kidato cha 4 mwakani 2021 na anatoka mazingira magumu kupata msaada wa taulo za kike kwa kipindi cha mwaka mzima. 

“Tunaamini hii itamsaidia binti huyu kutokosa shule hivyo kumuongezea nafasi ya kufaulu vizuri zaidi katika awamu hii ya kwanza tutafikia wanafunzi wa kike 1,500 kutoka Mikoa ya Dodoma, Tabora, Kigoma, Kagera, Geita, Tanga na Lindi. 

Kwa upande wa Mama Simba alipoulizwa alipokeaje wazo hili na kwanini ameamua kuunga mkono juhudi za Mh Neema Lugangira alisema wameamua kuunga mkono juhudi za Neema Lugangira kwa sababu ni binti ambaye alikaa na kufirikiria watoto wa kike wa vijijini wasiojiweza kupitia shule.

“ Sisi Kays Hygiene tunauzoefu wa karibia miaka 40 na ni nadra sana kukutana na binti mwenye kujitoa kwa jamii namna hii hivyo huu ni mfano wa kuigwa hivyo tunampongeza sana Mh Neema Lugangira na tunaamini atakwenda kuwa mtetezi mzuri wa hedhi salama bungeni”Alisema

Hata hivyo alisema amefarijika kufanya kazi na Neema na huu ni mwanzo huku akihaidi kuendelea kumuunga mkono kwa kuhakikisha wanampa bei nafuu ambayo hawezi kupata kokote pale ili punguzo la bei iwe pia ni mchango wetu katika kuendeleza juhudi zake.

 

Share:

SAVE THE CHILDREN YAENDESHA MAFUNZO YA MCHAKATO WA BAJETI NGAZI YA HALMASHAURI

 


Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, akielezea madhumuni ya mradi na mafunzo.
Na Marco Maduhu -Shinyanga. 

Shirika la Save The Children ambalo linatetea haki za watoto, limetoa mafunzo ya mchakato wa bajeti ngazi ya halmashauri, ili kuisaidia Serikali uaandaaji wa bajeti nzuri ambayo itatoa dira ya maendeleo kwa kuzingatia vipaumbele vya wananchi.


Mafunzo hayo ambayo yatachukua siku mbili kuanzia leo, yameshirikisha watendaji wa Kata, wataalamu kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, waandishi wa habari, pamoja na wadau kutoka mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali, 

Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wadau mbalimbali katika kushiriki kikamilifu kuandaa masuala ya bajeti, na kutambua wajibu wao katika kushiriki uundaji wa bajeti. 

Alisema mradi huo wa masuala ya kibajeti utadumu ndani ya miaka miwili, ambapo ulianza june (2020) na utakoma Decemba (2021), ambao unatekelezwa Zanzibar maeneo ya unguja mjini, magharabi “A” na “B”, Mbozi mkoani Songwe, pamoja na manispaa ya Shinyanga, kwa ufadhili wa Ubalozi wa ulaya. 

“Lengo pia la mafunzo haya ni kujenga uwezo kwa watendaji wa Serikali ngazi ya halmashauri, na wadau mbalimbali katika kupata elimu ya mchakato wa kibajeti ya Serikali, na kutambua miongozo inayo simamia michakato hiyo, ili kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa haki za watoto hasa katika masuala ya kiafya, elimu, pamoja na kupinga matukio ya ukatili,” alisema Enock. 

Naye Mgeni Rasmi akifungua mafunzo hayo Katibu tawala msaidizi mipango na uratibu mkoani Shinyanga Joachim Otaru, aliwataka washiriki hao wayashike vizuri mafunzo hayo, na kwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo katika uaandaji wa bajeti, kwa kuzingatia vipaumbele vya wananchi pamoja na kushirikisha makundi yote. 

“Mafunzo haya ya bajeti ni muhimu sana, sababu yanagusa maisha yetu, hivyo na waomba katika uaandaji wa bajeti ijayo ya Serikali, mshirikishe wadau na makundi yote kuanzia ngazi ya chini,”alisema Otaru. 

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo ya kibajeti mchumi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Allex Mpasa, alisema kuwa sasa hivi bajeti hua zinaandaliwa kwa kuzingatia jitihada za wananchi, na siyo kuzingatia vipaumbele vyao, jambo ambalo siyo sahihi. 

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo hasa watendaji wa Serikali, walishukuru kupewa elimu hiyo ambayo itakuwa msaada mkubwa kwao, katika uaandaji wa bajeti kwa kuzingatia vipaumbele vya wananchi, na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 
Katibu tawala msaidizi mipango na uratibu mkoani Shinyanga Joachim Otaru,akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, akielezea madhumuni ya mradi na mafunzo.
Mchumi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Allex Mpasa, akitoa elimu ya uaandaaji wa bajeti.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Afisa mipango mwandamizi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Zanzibar Masika Baraka, akichangia kwenye mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoinem akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Glory Mbia ambaye ni mwakilishi wa (UN WOMEN) Mkoani Shinyanga, akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
John Shija kutoka shirika la Paceshi mkoani Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Salum Sudi ambaye ni mtendaji wa Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Victor Kajuna mtendaji wa Kata ya Ibinzamata manispaa ya Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Ponsian Isaack mtendaji wa Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Sara Wamkuru mtendaji wa Kata ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye kazi ya vikundi.
Washiriki wakiwa kwenye kazi ya vikundi.
Washiriki wakiwa kwenye kazi ya vikundi.
Washiriki wakiwa kwenye kazi ya vikundi.
Washiriki wakiwa kwenye kazi ya vikundi.

Na Marco Maduhu- Shinyanga. 


Share:

NKULILA ACHAGULIWA KUWA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA..MBOJE ATETEA UENYEKITI SHY DC, LUHENDE JIJIMYA ATOBOA KISHAPU

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila

Na Damian Masyenene- Shinyanga
Madiwan wa Halmashauri za Wilaya ya Shinyanga na Kishapu wamefanya uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu wa halmashauri hizo, huku wale wa Manispaa ya Shinyanga wakiwachagua Mstahiki Meya na Naibu wake, ambapo Diwani wa Kata ya Ndembezi, David Nkulila (CCM) amepita bila kupingwa katika nafasi ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga akipigiwa kura zote 23 za ndiyo.

Nkulila amechaguliwa leo Novemba 24, 2020 katika uchaguzi uliofanyika kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, huku Esther Festo Makune akishinda nafasi ya Naibu Meya kwa kupata kura 17 kati ya 23, akifuatiwa na Mariam Nyangaka wa Kata ya Kitangiri aliyepata kura nne na Ruben Kitinya wa Kata ya Kizumbi akipata kura mbili.

Katika Halamashauri ya Wilaya ya Shinyanga, aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ngassa Mboje ametetea nafasi hiyo kwa ushindi wa kura 20 dhidi ya Amos Mshandete wa Kata ya Ilola aliyepata kura 16.

Isack Sengerema wa Kata ya Iselamagazi ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kupata kura 19 dhidi ya Hamis Masanja wa kata ya Samuye aliyepata kura 17.

Kwa upande wa halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambao walifanya uchaguzi jana Novemba 23, 2020, Diwani wa Kata ya Mondo, William Luhende Jijimya alishinda nafasi ya Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kura 24, huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikienda kwa Anderson Mandiya wa Kata ya Ukenyenge aliyepata kura 15.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Said Bwanga (kushoto) pamoja na baadhi ya madiwani wa manispaa ya Shinyanga waliohudhuria uchaguzi wa Mstahiki Meya wa manispaa hiyo leo katika ofisi za chama hicho.
Mstahiki Meya Mteule wa Manispaa ya Shinyanga, David Nkulila (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (aliyevaa miwan) na madiwani wa manispaa hiyo leo baada ya kukamilika kwa zoezi la uchaguzi katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Esther Festo Makune (kulia) na Mstahiki Meya, David Nkulila (kushoto wakiwa katika picha ya Pamoja na Diwani wa Kata ya Kitangiri, Mariam Nyangaka (katikati) baada ya kukamilika kwa uchaguzi huo, huku diwani huyo akiambulia nafasi ya pili kwenye kinyang'anyiro cha Unaibu meya.

Share:

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI..YUMO RAIS MSTAAFU WA ZANZIBAR NA MWAKYEMBE


Kushoto ni Dkt. Harrison Mwakyembe na kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Rais Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamesd Shein, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta, ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Novemba 24, 2020, kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, ambapo pia Rais Magufuli, amemteua Dkt. Harrison Mwakyembe, aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), akichukua nafasi ya Mariam Joy Mwaffisi.

Mwingine aliyeteuliwa hii leo ni aliyewahi kuwa Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), akichukua wadhifa huo kwa kipindi cha pili sasa.

Uteuzi wa viongozi wote hao watatu unaanza hii leo.
Share:

WABUNGE VITI MAALUM CHADEMA WAAPISHWA UBUNGE DODOMA


Wabunge wa viti maalum wa CHADEMA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kula kiapo cha ubunge, kilichoongozwa na Spika Ndugai.
***
Wabunge wateule wa viti maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Halima Mdee, wamekula kiapo hii leo katika viwanja wa Bunge jijini Dodoma.

Zoezi la uapisho wa wabunge hao limeongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, hii leo Novemba 24, 2020.

Akizungumza mara baada ya kula kiapo, Halima Mdee amesema kuwa, "Nakishukuru chama changu cha CHADEMA kikiongozwa na Mwenyekiti wetu Freema Mbowe, ambao kupitia wao sisi tumepata nafasi ya kukiwakilisha chama chetu, viti hivi siyo hisani ila ni sehemu ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata".

Waliokula viapo hivyo hii leo ni wabunge 19, akiwemo Ester Bulaya, Salome Makamba, Grace Tendega, Kunti Majala, Esther Matiko, Halima Mdee, Cecilia Paresso, Agnesta Lambati, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Tunza Malapo, Konchester Leonce Rwamlaza.

Chanzo - EATV 
Share:

HATIMAYE TRUMP AKUBALI KUANZA KUMKABIDHI OFISI JOE BIDEN


Rais mteule Joe Biden Kushoto na rais Trump kulia

Donald Trump amekubali kuanza kwa mchakato rasmi wa kumkabidhi madaraka Rais mteule Joe Biden.

Rais amelitaka shirika linaloshughulikia mabadilishano hayo "lifanye kile kinachostahili kufanywa", hata wakati anaahidi kuendelea kupinga matokeo.

Ofisi ya utawala wa huduma za serikali imesema inamtambua Bwana Biden kama "mshindi".

Hilo linawadia wakati Bwana Biden ameidhinishwa rasmi kama mshindi wa jimbo la Michigan na kuwa pigo kubwa kwa Trump.

Timu ya Bwana Biden imefurahishwa na kuanza kwa mchakato huo wakati rais mteule anajiandaa katika sherehe za kuapishwa Januari 20,2021.

"Uamuzi wa leo ni hatua iliyohitajika kuanza kukabiliana na changamoto zinazokumba taifa letu ikiwemo kudhibiti ugonjwa wa virusi vya corona na kuboresha uchumi tena," taarifa iliyotolewa imesema.

"Uamuzi huo ni hatua ya kiutawala ya kuanza rasmi kwa mchakato wa mabadilishano ya madaraka na mashirika husika."

Mapema Jumatatu, Bwana Biden alizindua timu itakayoangazia sera ya fedha na usalama wa taifa iliyojumuisha watu wa zamani wa miaka hiyo katika utawala wa Obama.

Biden atamchagua Anthony Blinken kuwa waziri wa mambo ya nje na John Kerry kama mjumbe wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, huku Janet Yellen ikidokezwa kwamba ndiye atakayekuwa mwanamke wa kwanza kuwa waziri wa fedha.

Trump aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter wakati ofisi ya utawala wa huduma za serikali ambayo ndiyo yenye jukumu rasmi la kuanza mchakato wa mabadilishano ya madaraka inaarifu timu ya Biden kwamba itaanza mchakato huo.

Afisa wa ofisi hiyo Emily Murphy alisema dola milioni 6.3 sawa na (£4.7m) amezitenga kwa ajili ya rais mteule.

Wakati anaahidi kuendelea na "vita hivyo muhimu", rais alisema: "Haidhuru, kwa maslahi ya nchi yetu, Napendekeza Emily na timu yake kufaya kile kinachostahili kwa kuzingatia itifaki za awali na pia nimearifu timu yangu kufanya vivyo hivyo."
Chanzo - BBC
Share:

MAPACHA WA KIUME WAOA MAPACHA WENZAO


Mapacha wa kiume walifunga ndoa na mapacha wenzao wa kike.
****
Hassan Sulaiman na Hussaini Dey ni mapacha wawili wa kiume wenye miaka 33, wameoa mapacha wenzao wa kike ambao wamefahamika kwa majina ya Hassana na Hussaina huko Kano Kaskazini mwa nchi ya Nigeria.

Mmoja wa mapacha wa kiume Hassan Sulaiman amesema tangu walivyokuwa wadogo walikuwa wanasema kitu bora kwao ni kuoa mapacha wenzao ambapo wametimiza ndoto zao.

"Tangu tulipokuwa wadogo, tulikuwa tunafanya kila kitu pamoja, tulikuwa tunavaa nguo zinazofanana, kula chakula cha aina moja na tulisoma katika darasa moja, hata tulipoenda kusomea masuala ya afya namba ya usajili wa mtihani yake ilikuwa 010 wakati yangu ilikuwa 011" ,amesema.

Aidha ameongeza kusema "Kwa muda mrefu tulipanga kuoa mapacha na hata familia yetu walituambia tuoe mapacha, kabla ya sasa, tumekuwa tukijaribu bahati yetu na sasa tuna furaha sana ndoto zetu zimetimia".

Chanzo : Opera News Nigeria , Daily Trust Nigeria, BBC Swahili.
Share:

WADAU WATAKA SERIKALI KUJIPANGA MPANGO WA TATU WA MAENDELEO


Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dk Tausi Kida (kulia) wakati wa mkutano wa mashauriano kuhusu mpango wa maendeleo wa tatu (FYDP III) wenye lengo la kushirikisha zaidi sekta binafsi katika kuufanya uchumi wa Tanzania kuwa wa kishindani kilichofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendani wa UN Global Compact Network Tanzania , Bi Marsha Macatta Yambi akizungumza na wadau waalikwa wakati wa mkutano wa mashauriano kuhusu mpango wa maendeleo wa tatu (FYDP III) wenye lengo la kushirikisha zaidi sekta binafsi katika kuufanya uchumi wa Tanzania kuwa wa kishindani kilichofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mtafiti Mshiriki wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dr. Hoseana Lunogelo akiendesha mashauriano wakati wa mkutano kuhusu mpango wa maendeleo wa tatu (FYDP III) wenye lengo la kushirikisha zaidi sekta binafsi katika kuufanya uchumi wa Tanzania kuwa wa kishindani kilichofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mtafiti Mshiriki Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Prof Samuel Wangwe akizungumza wakati wa mkutano wa mashauriano kuhusu mpango wa maendeleo wa tatu (FYDP III) wenye lengo la kushirikisha zaidi sekta binafsi katika kuufanya uchumi wa Tanzania kuwa wa kishindani kilichofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Biashara ya Utalii Wazawa (TLTO), Bw. Samwel Diah akielezea changamoto za utalii nchini ambazo zisizopatiwa ufumbuzi sekta hiyo haiwezi kusaidia kuinua maendeleo ya Tanzania wakati wa mkutano wa mashauriano kuhusu mpango wa maendeleo wa tatu (FYDP III) wenye lengo la kushirikisha zaidi sekta binafsi katika kuufanya uchumi wa Tanzania kuwa wa kishindani kilichofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Meneja MKuu wa Hoteli ya Whitesand, Bi. Nadine Atallah akifafanua jambo katika mkutano wa mashauriano kuhusu mpango wa maendeleo wa tatu (FYDP III) wenye lengo la kushirikisha zaidi sekta binafsi katika kuufanya uchumi wa Tanzania kuwa wa kishindani kilichofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Taifa (ACT), Jitu V. Soni akizungumza katika kikao cha mashauriano cha mpango wa tatu wa maendeleo(FYDP III) nchini kilichofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau walioshiriki wa mkutano wa mashauriano kuhusu mpango wa maendeleo wa tatu (FYDP III) wenye lengo la kushirikisha zaidi sekta binafsi katika kuufanya uchumi wa Tanzania kuwa wa kishindani uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.


Na MwandishiWetu
Serikali imeshauriwa kuhakikisha kwamba inakuwa na wataalamu wakisekta kama itataka kufanikisha lengo la kuwa nchi yaviwanda ifikapo mwaka 2025.

Kauli hiyo imetolewa na washiriki katika mkutano wa mashauriano wa sekta binafsi kuhusiana na matayarisho ya Mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka ujao.

Washiriki hao wamesema kwamba mambo yanayotendeka Wizara ya fedha na mipango pamoja na kauli nzuri zilizopo hazi ashirii kutoa ushirikiano kwa sekta binafsi iliiweze kushiriki kikamilifu katika uwezeshaji waukuaji wa uchumi.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huou lioratibiwa na Taasisi yaUtafiti wa Uchumi naKijamii (ESRF) Samwel Diah alisema serikali imekuwa ikikazania kukusanya ushuruna kodi bila kuangalia uendelezaji wa sekta husika yautalii, kilimo au viwanda.

"Hili ni tatizo lakukosekana kwa wabobezi wanaojua sekta na kushughulikia changamoto kwa lengo la kusongesha mbele gurudumu la maendeleo"alisema Diah na kuongeza kwamba vijana wengi wahitimu wa shahadambalimbali wana vyeti vizuri lakini hawajui changamoto zinazokumba sekta hivyo kusaidia kutatua kutokana na kutokuwa na uzoefu katika sekta husika.

Alipendekeza kuwa katika rasimu hii inayoandaliwa yaMpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo wa awamu ya tatu kuwa na nafasi inayowatambua waliobobea katika fani ili waweze kutoa ushauri unaofaa katika uendeshaji wa dira mbalimbali za maendeleo.

Naye Jitu Soni ambaye ni Makamu Mwenyekikti wa Baraza la Kilimo la Taifa (ACT) alisema kwamba kuna haja ya kufanya kazi kwa pamoja kwa kuangalia misingi ya sekta na kuiunganisha ili iweze kutoa matokeo chanya.

Alisema ilikuwepo na maendeleo ya kilimo lazima kuwepo na viwanda vya kuwezesha kusindika bidhaa za kilimo ili ziweze kuwa katika hatua nyingine na hiii tasaidia sana katika kuimarisha kilimo chenyewe.

Alisema inasikitisha kuona kwambawakati taifa linategemea kilimo hakuna ufungamanishajiwa kilimo na viwanda na hivyo bidhaa nyingiz za kilimo kutokuwa na ushindani katika soko la dunia.

Pia alitaka kuwepo na uzalishaji wa wataalamu (skills) kwa lengo la kuhakikisha kwamba sekta zinanufaika na uwapo wao badala ya hali ya sasa kwamba wataalamu wanaozalishswa wanashindwa kukidhi mambo ya kitaalamu katika sekta zote ikiwamo ya kilimo.

Naye NadineAtallah alisema kwamba sekta ya utalii imekuwa ikizungumza kila mara kuhusu changamoto zake na imekuwa ikialikwa kila mahali kuelezea namna bora ya kupambana na changamoto hizo lakini mpaka leo hawajaona hatua zinazochukuliwa.

Alitaka kuwepo na mabadiliko ya kweli na kusikiliza ushauri wanaotoa kwa lengo la kuendeleza sekta hiyo na wala sio kukwamisha.

Baadhi ya wajumbe walisema kwamba japo inatakiwa kufikiri kuongeza watalii wa ndani kupambana na majanga na changamoto za sasa za sekta hiyo gharama zinazoambatana na uwekezaji zinafanya mtu wa kawaida Tanzania asiweze kutumia miundo mbinu iliyopo ya kitalii.

"Tusimung'unye maneno utalii wa kuzalishwa na wananchi hauwezekani kwa gharama zilizopo labda uandaliwe mkakati mwingine' alisema mmoja wa washiriki.

Akielezea DirayaTaifa (vision 2925) iliyotengenezwa miaka ya 1990, mmoja wawaasisi wa dira hiyo yenye mipango ya miaka mitano kwa awamu tatu, Profesa Samwel Wangwe alisema kusudia la mwanzo la mpango huo ni kuiweka Tanzania katika uchumi wakati wenye kipato cha dola 3000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025, huku viwanda vikichangia.

Aidha alisema ukuaji wa uchumi ulipangwa kuwa wa asilimia nane kila mwaka.

Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuchambuana kuweka fikira nzito zaidi za kusonga mbele hasa ikizingatiwa kwamba dira hiyo iko katika hatua za mwisho za utekelezaji wake.

Naye Profesa Nyange alisema kwamba nguvu zaidi zinatakiwa kuinua zaidi pato la taifa na pia kupunguza umaskini wa kupitiliza.

 Aidha alisema kwamba zifikiriwe njia za kuendeleza mabadiliko ya kweli katika kilimo na kuimarisha viwanda nchini.
"Naona kuna watu wanaanza kulima mashamba makubwa na uzalishaji wa kilimo kuongezeka haya nia mabadiliko mazuri lakini tunatakiwa kufanya zaidi.

Awali akifungua mkutano huo wa mashauriano kuangalia namna bora za utekelezaji wa ngwe ya tatu na ya mwisho katika mpango wa taifa wa Vision 2025, Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango aliwataka wajumbe kuhakikisha kwamba wanatoa mawazo yao kwa uhuru zaidi.

Alisema Taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1994 ina majukumu makubwa ya kitafiti na pia kusaidia kukutanisha sekta binafsi na umma kutengeneza mustakabali wa maendeleo ya taifa.

Anasema lengo lakuwa na mkutano huo ni kushauri namna bora ya kuwezesha mpango wa tatu wa taifa kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia sekta binafsi kuwezesha mapinduzi ya viwanda na kilimo nchini.

Aliwataka washiriki kutoa ushauri wao namna ya kufanya uchumi wa Tanzania kuwa shindani katika soko la dunia.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger