Friday 25 September 2020

C –FM DODOMA YAPAZA SAUTI KUPINGA UKEKETAJI

Balozi wa ''Nisitiri nina haki ya kutimiza ndoto zangu,Usinikekete na usinipe Mimba Utotoni'' Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Diana Exavery maarufu kwa jina la Malaika,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukeketaji kwa Mikoa ya Kanda ya Kati inayoratibiwa na Redio hiyo iliyofanyika leo jijini Dodoma

Msimamizi Mkuu wa vipindi vya Redio ya C-FM,Emmanuel Likuda,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukeketaji kwa Mikoa ya Kanda ya Kati inayoratibiwa na Redio hiyo iliyofanyika leo jijini Dodoma

Balozi wa ''Nisitiri nina haki ya kutimiza ndoto zangu,Usinikekete na usinipe Mimba Utotoni'' Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Diana Exavery maarufu kwa jina la Malaika,akiwa katika picha ya pamoja na Msimamizi Mkuu wa vipindi vya Redio ya C-FM,Emmanuel Likuda mara baada ya kuzindua kampeni ya kutokomeza ukeketaji kwa Mikoa ya Kanda ya Kati inayoratibiwa na Redio hiyo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

...........................................................................................

Na. Alex Sonna, Dodoma

Kituo cha Redio C FM Mkoani Dodoma kimezindua Kampeni ya ''Nisitiri nina haki ya kutimiza ndoto zangu,usinikekete,usinipe mimba utotoni'' kwa mtoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao.

kampeni hiyo imezinduliwa leo Jijini Dodoma kwa lengo la kutokomeza ukeketaji kwa Mikoa ya Kanda ya Kati inayoratibiwa na Redio ya C-FM ya jijini Dodoma na Msimamizi Mkuu wa vipindi wa Redio hiyo,Emmanuel Likuda .

Likuda ameeleza kuwa kwa mujibu wa ripoti ya Tanzania Demographic and Health Survey and Malaria (TDHS) kwa mwaka 2015-2016 inaonesha Mkoa wa Manyara unaongoza kwa kukeketa wasichana huku ripoti hiyo ikieleza kuwa wasichana wanaozaliwa au kulelewa na mama aliyekeketwa hukeketwa pia.

“hali ya ukeketaji nchini inaonesha kuwa Mkoa wa Manyara unaongoza kwa ukeketaji kwa asilimia 58 ukifuatiwa na Dodoma kwa asilimia 47,Arusha asilimia 41,Mara 32 na Singida asilimia 31”, ameeleza Likuda.

Aidha Likuda amesema kuwa ripoti hiyo imefafanua kuwa ukeketaji hufanywa kwa asilimia 86 na mangariba au wakeketaji wa jadi na asilimia 25 hukeketwa katika umri wa miaka 13 na zaidi.

Vile vile Ripoti hiyo imeeleza kuwa wasichana wanaozaliwa au kulelewa na mama aliyekeketwa hukeketwa pia na kuwa na asilimia 95 ya asilimia 86 ya wanawake waliokeketwa hawakubaliani na kitendo hicho na wanatamani kisiwepo kabisa

Naye Balozi wa kampeni hiyo Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Diana Exavery maarufu kwa jina la Malaika, amesema madhara ya ukeketaji ni makubwa kiafya kwa mtoto wa kike ikiwemo kupata athari za kisaikolojia kama msongo wa mawazo kwani wengi hufanya hivyo bila ridhaa yao.

Pia Balozi huyo ameongeza kuwa Madhara ya afya ya uzazi ambayo hupelekea kuongezeka kwa vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua pia maumivu makali wakati wa kukeketwa,kumwaga damu nyingi,kovu la kudumu sehemu za siri pamoja na kutokufurahia tendo la ndoa.

Kutokwa na damu nyingi,kovu la kudumu sehemu za siri pamoja na kutokufurahia tendo la ndoa.
Share:

Thursday 24 September 2020

1,352 NEC Temporary Jobs at BAHI Constituency | Ajira Za Uchaguzi 2020 | National Electoral Commission (NEC) Jobs 2020

The Background on the National Electoral Commission of TanzaniaIn 1991 the then President of the United Republic of Tanzania, His Excellency Ali Hassan Mwinyi appointed a commission under the Chairmanship of the late Chief Justice of Tanzania, the Honourable Francis L. Nyalali. The task of that Commission was to collect public opinion as to whether […]

The post 1,352 NEC Temporary Jobs at BAHI Constituency | Ajira Za Uchaguzi 2020 | National Electoral Commission (NEC) Jobs 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

1,508 NEC Temporary Jobs at MBINGA VIJIJINI Constituency | Ajira Za Uchaguzi 2020 | National Electoral Commission (NEC) Jobs 2020

The Background on the National Electoral Commission of Tanzania In 1991 the then President of the United Republic of Tanzania, His Excellency Ali Hassan Mwinyi appointed a commission under the Chairmanship of the late Chief Justice of Tanzania, the Honourable Francis L. Nyalali. The task of that Commission was to collect public opinion as to […]

The post 1,508 NEC Temporary Jobs at MBINGA VIJIJINI Constituency | Ajira Za Uchaguzi 2020 | National Electoral Commission (NEC) Jobs 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MWANAFUNZI AMCHARANGA MAPANGA MWALIMU AKIFUATILIA WATORO SHULENI

Jeshi la polisi mkoani Mara linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha tatu Mwita Machamo,(17) katika shule ya sekondari ya Kiagata kwa kumkata na panga mwalimu wake Majogoro John, baada ya mwanafunzi huyo kushindwa kumpeleka mzazi wake shuleni kama alivyoagizwa na mwalimu.

Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 24, 2020, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Daniel Shillah, na kusema kuwa tukio hilo lilitokea shuleni hapo majira ya asubuhi wakati mwalimu anakagua wanafunzi watoro, na ndipo mwanafunzi huyo alimgeukia mwalimu wake na kumkata mapanga.

"Baadhi ya wanafunzi waliwaleta wazazi wao, lakini huyu mwanafunzi kwa utovu wa nidhamu uliopindukia alikuja na upanga akiwa ameuficha kwenye nguo zake na mwalimu alipohoji kwanini hujaja na mzazi, mwanafunzi akachomoa upanga na kumshambulia mwalimu na akawatisha tisha wanafunzi wengine akapata nafasi ya kukimbia lakini wakamkata na tumemshikilia na atafikishwa mahakamani", amesema Kamanda Shillah.

Majogoro John ni mwalimu aliyejeruhiwa na mwanafunzi wake hapa amesimulia hali ilivyokuwa:

"Nilipita darasani kuangalia watoro nikamambia fuata mzazi tuje tuongee ili nijue shida nini yule akatembea hatua kama tatu kwenda mlangoni akageuka alivyotoa upanga akageuka haraka akanikata begani akageuka tena ili anikate kichwani ndipo nikaweka mkono wa kushoto akaiga panga nikaona tu mkono unaning'inia".

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara Joachim Iyembe, amesema kuwa wamempokea mgonjwa huyo na kumpa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

 Chanzo - Eatv
Share:

WASINDIKAJI WA MAFUTA YA KULA WATAKIWA KUFUATA KANUNI ZA USAFI KULINDA AFYA KWA MLAJI


Afisa mdhibiti ubora Sileja Lushibika akizungumza na mmoja wa Wazalishaji mafuta ya kula Mkoani Singida baada ya kutembelea Wazalishaji hao na kuwapatia elimu ya usindikaji wa mafuta.
Meneja wa Mafunzo na Utafiti TBS Bw. Hamisi Mwanasala, akitoa elimu ya vifungashio kwa wadau wa mafuta ya kula yanayoendelea kanda ya kati, katika ukumbi wa shule ya sekondari Shelui wilaya ya Iramba.

********************************

Wazalishaji na wauzaji wa mafuta ya kula wametakiwa kufuata kanuni za usindikaji wa mafuta ili kuweza kuzalisha bidhaa iliyobora na kumlinda mlaji.

Akizungumza na baadhi ya wasindikaji wa Mafuta ya Kula Mkoani Singida Afisa mdhibiti ubora Sileja Lushibika amesema sio kila mtu anaruhusiwa kuingia katika eneo la usindikaji ili kuzuia bidhaa inayozalishwa kuwa na uchafuzi na anaeruhusiwa kuingia katika eneo la usindikaji ni yule ambaye amefuata kanuni zote.

Nae Meneja wa Mafunzo na Utafiti Hamisi Sudi amewataka wasindikaji hao kueleza changamoto zao mahali husika ili kuweza kutatuliwa changamoto ambazo zinawakabili na baadae kukuza biashara zao na kufikia malengo yao.

"Kama mkiwa na changamoto zenu, maafisa biashara wapo,maafisa SIDO wapo ombeni nafasi ya kupata elimu hii wale wakisikia kilio chenu watawaita taasisi inayohusika na kuwasaidia".

Hata hivyo kwa upande wake Meneja wa Mafunzo na Utafiti TBS Bw. Hamisi Mwanasala, akitoa elimu ya vifungashio kwa wadau wa mafuta ya kula yanayoendelea kanda ya kati, katika ukumbi wa shule ya sekondari Shelui wilaya ya Iramba amesema ili vifungashio viwe bora vinatakiwa kuwa na vitu mbalimbali ikiwemo jina la biashara (Bidhaa inayowekwa kwenye kifungashio),anuani ya mzalishaji, uzito na ujazo,namba ya toleo,utunzaji,taarifa za kutumia/kuuza.

Share:

Tumeimarisha Miundombinu Ya Usafiri - Majaliwa


MJUMBE wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema Serikali ya CCM imeimarisha miundombinu ya usafiri nchini ili wananchi waweze kuchagua aina ya usafiri wanaotaka pindi wanapotaka kusafiri.

"Tunataka tuhakikishe Watanzania wanatumia njia zote za usafiri kulingana na matakwa yake ndio maana tunatengeneza barabara, tumenunua ndege, tunajenga reli pamoja na kuendelea kuboresha usafiri wa majini," amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Septemba 24, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa Misungwi kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Amani wilayani humo, mkoani Mwanza.

"Tunajenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na Dodoma, baadaye itatengenezwa ifike hadi Tabora na Mwanza. Ukitaka kupanda ndege una uhuru, ukitaka treni nenda, ukitaka basi, barabara nzuri zipo na ukienda majini nako pia tumeboresha usafiri,” amesema.

Mheshimiwa Majaliwa yuko mkoani Mwanza kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli. Aliwasisitiza wakazi hao wasiache kupiga kura siku hiyo. Mbunge wa jimbo la Misungwi, Bw. Alexander Mnyeti na madiwani wote 27 wa jimbo hilo wamepita bila kupingwa.

“Tunataka tuwe na kiongozi ambaye anaweza kuratibu maendeleo ya Watanzania, kiongozi ambaye anaweza kurudi chini na kujua kuna changamoto gani, tunataka kiongozi ambaye ana uwezo wa kusimamia rasilimali zetu, na huyo si mwingine bali ni Dkt. John Pombe Magufuli,” amesema.

Akielezea sekta ya mifugo, Mheshimiwa Majaliwa amesema: “Rais wetu amefanya maboresho makubwa sana katika sekta ya mifugo, Rais anataka kuona wafugaji na wavuvi wananufaika na shughuli zao, yale mapori makubwa tunachukua ili wafugaji wapate sehemu za malisho pia tunajenga mabwawa hukohuko, tunajenga maabara kwa ajili ya kutibu mifugo yetu. Kwenye uvuvi tunaimarisha sekta hiyo, ili kuhakikisha tunaendelea kuinua sekta hiyo, tumepunguza kodi pamoja na kuondoa tozo mbalimbali.”

(mwisho)


Share:

Majaliwa Asema Kiti Cha Urais Siyo Mchezo....Ataka Wananchi Wampe Kura Zote Dkt. Magufuli


MJUMBE wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kassim Majaliwa amesema kiti cha urais siyo cha mchezo, kinahitaji mtu makini.

"Uongozi wa nchi siyo jambo la mchezo, linataka kiongozi makini, kiongozi anayetetea rasilmali na anayetetea wanyonge dhidi ya rushwa na ufisadi," amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Septemba 24, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata za Hungumalwa na Ngudu wilayani Kwimba, mkoani Mwanza kwenye mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya sokoni.

"Wengine watakuja kuomba kura lakini kazi yao kubwa ni kukashifu kila jambo linalofanywa na Serikali. Naomba kura za wananchi wote, wana CUF, CHADEMA, ACT mkipigie kura Chama cha Mapinduzi sababu maendeleo hayana chama."

"Wakija hapa muwasikilize; mkiwauliza Ilani yao watakwambia wanayo ila iko kwenye website. Sisi ya kwetu tunayo hii hapa," alisema huku akionesha Ilani ya CCM ya 2020 - 2025."

Amewataka wakazi hao wafanye maamuzi thabiti ya kutafuta viongozi tena wanaozungumza lugha moja. "Viongozi hao ninawaombea kura ni Rais, Mbunge na Diwani. Msichague viongozi ambao kazi yao ni kusema hapana kwenye mambo ya maendeleo au kwenye bajeti ya Taifa. Naomba kura kwa viongozi hao watatu," amesema.

Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko mkoani Mwanza kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alitumia fursa hiyo kumwombea kura mgombea ubunge wa jimbo la Kwimba, Bw. Shanif Mansoor, mgombea udiwani wa Hungumalwa, Bw. Bukaba  Majoge na madiwani wa kata zote za wilaya ya Kwimba.

Wakati huohuo, mgombea ubunge wa jimbo la Geita Vijijini, Bw. Joseph Kasheku Msukuma ambaye aliwepo kwenye mikutano huo, alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali iwajengee soko la kisasa wakazi wa Hungumalwa kwa sababu eneo hilo pana biashara kuwa ya dengu, choroko na kunde.

(mwisho)

  


Share:

Doto James: Miradi Ya Kimkakati Inayotekelezwa Nchini Ni Kwa Mujibu Wa Sheria

Na. Farida Ramadhani na Ivona Tumsime, WFM, Dodoma
Serikali imesema kuwa miradi yote mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa nchini imeshapangwa ndani ya bajeti za kisekta za Wizara husika ambazo hupitishwa na Bunge kila mwaka.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanamipango nchini kwa Mwaka 2020, jijini Dodoma.

Bw. James alitoa ufafanuzi huo baada ya kusambaa kwa taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa kuwa Serikali inakurupuka kuibua miradi ambayo haijulikani na haijapangiwa fedha za kuitekeleza.

“ Miradi inatekelezwa kwa mujibu wa bajeti inayopitishwa na Bunge ambayo inairuhusu Serikali kukopa ndani na nje ya nchi, kukusanya Kodi na kupokea misaada ili itekeleze bajeti yake”, alieleza Bw. Doto James.

Alisema kuwa baada ya bajeti kupitishwa kinachofuata ni utekelezaji wa bajeti ambapo Serikali hutumia fedha za makusanyo ya mapato, mikopo na misaada kwa mujibu wa sheria kwa kuwa Serikali haipokei fedha kiholela.

 Bw. James alisema kuwa Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada inampa Waziri wa Fedha wajibu kutafuta fedha za utekelezaji  wa bajeti iliyoridhiwa na Bunge.

Kwa upande wa utekelezaji wa mipango ya miradi Bw. James alisema kumekuwa na changamoto ya upatikanaji na utunzaji wa taarifa za miradi ambazo huwezesha maandalizi ya mipango na kufanya tathmini ya utekelezaji jambo lililosababisha Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kutengeneza Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo ili kutatua  changomoto hiyo.

“Mfumo huo utakuwa na sehemu zote za mzunguko wa mradi yaani kuanzia uibuaji, ugharamiaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini, utoaji taarifa na ufungaji wa mradi baada ya utekelezaji kukamilika”, alieleza Bw. James.

Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Fedha na Mipango aliwaagiza wanamipango wote nchini kuongeza ubunifu katika kupanga mipango mbalimbali ya nchi  ili kuiwezesha nchi  kufikia malengo kwa wakati.

Alisema kutokana na hadhi ambayo Tanzania imefikia ya kuwa na Uchumi wa Kati, inabidi wanamipango wabadili namna ya kupanga na kutekeleza mipango ya nchi na kuwakumbusha kuwa suala sio kupanga tuu bali ni kupanga mipango inayotekelezeka na kuhakikisha inatekelezwa ipasavyo ili kupata matokeo yaliyokusudiwa.

Naye Kamishna wa Mipango ya Kitaifa kutoka Wizara ya  Fedha na Mipango, Dkt.  Nicolaus Shombe, alisema kuwa dhima ya Kongamano hilo ni Mipango ya Kujenga Uchumi Shindani Unaoongozwa na Mauzo Nje inayotokana na Mpango wa Tatu wa Taifa wa Miaka Mitano unaotarajiwa kuanza mwaka 2021/22.

Kwa upande wa washiriki wa Kongamano hilo akiwemo Dkt. Joel Mmasa, wameahidi kushiriki kikamilifu kutoa maoni na ushauri utakaosaidia Serikali kuja na Mpango wa Tatu wa Taifa wa Miaka Mitano pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22.

Aidha wameeleza kuwa watatumia maoni na ushauri utakaotolewa katika  Kongamano hilo kupanga mipango itayowezesha nchi  kupiga hatua zaidi katika hadhi ya Uchumi wa Kipato cha Kati na kuwa nchi ya kipato cha kati katika kiwango cha juu.

Mwisho.


Share:

Sh. Bilioni 58 Zatumika Mradi Wa Maji Ukerewe - Majaliwa


SERIKALI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imekamilisha ukarabati na upanuzi wa miradi ya maji katika miji mikuu ya wilaya, miji midogo na miradi ya kitaifa kwa sh. bilioni 58.8 ukiwemo mji wa Nansio, Ukerewe.

“Shilingi bilioni 58.8 zimetumika kwenye ukarabati na upanuzi wa miradi ya maji ambapo miradi ya maji katika Mji ya Longido, Sengerema na Nansio-Ukerewe imekamilika,” alisema.

Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa mji wa Nansio jana jioni (Jumatano, Septemba  23, 2020) kwenye uwanja wa Getrude Mongella, mjini Nansio, mkoani Mwanza.

Alisema kati ya fedha hizo, sh. bilioni 13 zimetolewa kwa ajili ya miradi ya maji ikiwemo sh. bilioni 10.9 za uboreshaji wa huduma ya majisafi mjini Nansio ambapo wakazi wapatao 108,653 wananufaika na mradi huo katika eneo lote la mji wa Nansio. Alisema sh. bilioni 2.1 zilitumika kwa uboreshaji huduma ya usafi wa mazingira mjini Nansio.

Aliitaja miradi mingine ya maji kuwa ni miradi ya maji Pamoja na uchimbaji visima ambapo zilitolewa sh. bilioni 1.3 kwa miradi hiyo ikiwemo ukarabati wa mradi wa maji Irugwa, mradi wa maji ya bomba ya Nansore, mradi wa maji wa Muriti/Ihebo, upanuzi wa mradi wa maji wa Chabilungo na upanuzi na ukarabati wa mradi wa maji Kazilankanda.

Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko mkoani Mwanza kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alitumia fursa hiyo kumwombea kura mgombea ubunge wa jimbo la Ukerewe, Bw. Joseph Mkundi na madiwani wa kata zote za wilaya ya Ukerewe.

Akielezea sekta ya uvuvi, Mheshimiwa Majaliwa alisema katika kutekeleza Ilani ya CCM, Serikali iliondoa kuondoa kodi katika zana na malighafi za uvuvi zikiwemo injini za kupachika, nyuzi za kushonea nyavu (twines) na vifungashio.

“Pia tumepunguza ada ya leseni ya kuuza samaki na mazao ya uvuvi yanayovuliwa kwenye maji baridi. Serikali itaendelea kufanya upya mapitio ya tozo mbalimbali katika sekta ya uvuvi ili kuwapunguzia kero wavuvi. Tumeweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa vifaa bora vya uvuvi, kuzuia uingizaji na uzalishaji wa zana haramu za uvuvi na kuhamasisha uwekezaji katika uzalishaji wa zana na vyakula vya samaki,” alisema.

Kuhusu sekta ya afya, Mheshimiwa Majaliwa alisema hospitali ya wilaya hiyo ilipatiwa sh.  milioni 570 ujenzi jengo la kisasa la upasuaji (theatre), ujenzi wa duka la dawa, ukarabati wa jengo la kuhifadhia maiti na ukarabati mkubwa wa wodi saba ambazo zote zinatumika.

Kuhusu umeme, alisema kati ya vijiji 76, vijiji 70 vimepelekewa huduma ya umeme na vijiji sita bado havina umeme. Alivitaja vijiji hivyo kuwa ni Kaseni, Busangumugu, Murutilima, Kitanga, Namakwekwe na Muhande.

Kuhusu elimu, Mheshimiwa Majaliwa alisema mpango wa elimu bila malipo kuanzia 2015/2016 – 2019/2020 uliwezesha shule za msingi 123 zipatiwe sh. bilioni 3.29 kwa ajili ya ukarabati, utawala, michezo, mitihani na posho kwa maofisa elimu kata na walimu wakuu.

Chini ya mpango huo, shule za sekondari 23 zilipatiwa sh. bilioni 2 kwa ajili ya fidia ya ada, chakula kwa shule za bweni na posho ya madaraka kwa wakuu wa shule.

Akielezea utekelezaji wa mfumo wa uboreshaji wa miundombinu ya shule wa Lipa Kutokana na Matokeo (EP4R) uliotekelezwa tangu 2015 hadi 2020, Mheshimiwa Majaliwa alisema sh.  milioni 309 zilitolewa kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu ya madarasa, vyoo na ofisi kwa shule mbalimbali zikiwemo Kalendelo, Murutunguru na Kakerege.

Kwa upande wa shule za sekondari, alisema shilingi milioni 873 zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa, vyoo na maabara kwa shule mbalimbali ikiwemo; Bukongo, Pius Msekwa, Bwisya, Muriti na Lugongo.

Mapema, akiwa Bwisya kwenye kisiwa cha Ukara, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kituo cha afya cha Bwisya na kukagua wodi ya wanaume na ya wazazi. Akiwa wodini, alielezwa kwamba uwepo wa kituo hicho umewaokoa akinamama wajawazito ambao zamani walilazimika kuvuka kwenda hospitali ya wilaya iliyoko Nansio ili kupata huduma za upasuaji.

Mkazi wa Bwisya, Bibi Chausiku Kalemo Kategu alisema amepita mjukuu baada ya mwanaye kuwafanyiwa upasiaji kwenye kituo hicho na akajifungua salama saa 8 za usiku. “Taarifa kuwa ukipata mtoto wa kike unadaiwa sh. 40,000 na na kiume sh. 50,000 siyo za kweli kabisa. Tena watu walikuwa wanasema kituo hiki kimejengwa kwa damu za watu, ni uongo mtupu,” alisema mama huyo.

Kabla ya kukagua kituo hicho, Mheshimiwa Majaliwa alikwenda kuweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya watu waliokufa kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere, Septemba 20, 2018. Ibada fupi ya kuwaombea marehemu hao iliongozwa na Padre Peter Paul wa Parokia ya Nyamwaga, Ukara na Sheikh Mudhakiru Maguza wa msikiti wa Bwisya.

Kuhusu usafiri wa majini, Mheshimiwa Majaliwa alisema kivuko cha Ukara hadi Bugolora  ujenzi wake umefikia asilimia 95 na kwamba imebakizwa kazi ya ukaguzi ili kiwe tayari kwa matumizi..

Aliuagiza uongozi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) uhakikishe unakamilisha kazi ya ukaguzi wa kivuko hicho ili ifikapo Oktoba mosi, kivuko hicho kianze kufanya safari zake kati ya Ukara na Bogolora (Nansio).

(mwisho)

  


Share:

Botswana Kuanza Kutumia Lugha ya Kiswahili Shuleni

Serikali ya Botswana inakusudia kuanzisha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Shule za Msingi. Waziri wa Elimu ya Msingi, Fidelis Molao amesema matumizi ya lugha ya Kiswahili yataanzishwa katika Shule ndani ya siku chache  zijazo

Kiswahili ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa sana katika eneo la Maziwa Makuu na sehemu zingine za Mashariki na Kusini Mashariki mwa Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na sehemu za Malawi.

Ikiwa Kiswahili kitatumika Botswana itakuwa ni lugha ya kwanza ya Kiafrika kutumika kutoka nje ya mipaka ya nchi hiyo ambayo ni mzalishaji mkubwa wa Almasi Ulimwenguni.

Molao amesema, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) itakuwa na washirika wakubwa wa kibiashara na nchi nyingi zinazozungumza Kiswahili katika siku za usoni jambo ambalo hata Botswana inalihitaji zaidi katika kukuza uchumi na mauzo ya nje.


Share:

Mazingira ya malezi ni sababu ya watoto wengi kubaki mtaani.


Na Samirah Yusuph, Bariadi. 
Watoto ni miongoni mwa vibarua wanaoupamba mji wa Bariadi mkoani Simiyu, ambapo wamekuwa wakifanya shughuli mbali mbali mtaani kwa ajili ya kijipatia kipato.

Wapo walioacha shule kwa sababu mbali mbali na kuingia mtaani lakini pia wapo wanaosoma huku wakiendelea kufanya shughuli hizo kwa ajili ya kujiingizia kipato na kuendesha maisha ya familia zao.

Baadhi ya watoto hao walisema kuwa mazingira ya nyumbani na malezi ni sababu ya ongezeko hilo kwani kuna baadhi ya wazazi wanawatuma watoto kufanya kazi mitaani ili waweze kusaidia familia.

"Unakuta mtoto hapati mahitaji yake yote kutoka kwa mzazi pengine mtoto anakuwa na uhuru uliopitiliza hata akirudi usiku wa manane mzazi hawezi kumuiliza alikuwa wapi hiyo inachangia sana mtoto kuharibikiwa," alisema Yohana Daud (19) mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari biashara.

"Hata hapa tunaona mtoto anatoka nyumbani hafiki shule anaenda mtaani kutafuta pesa na mzazi hajui wala hafuatilii na hapo ndipo ndoto zinaanza kufifia na mwisho anajikuta anaharibikiwa," aliongeza Yohana.

Matarajio ya watoto wengi ni kutimiza ndoto zao kama inavyokuwa tangu awali wanapoanza kwenda Shule licha ya wengi kutokufikia malengo yao na kuishia mtaani jambo ambalo linawakatisha tamaa.

"Binafsi sijisikii vizuri ninapoona wasicha wenzangu wanashindwa kwenda shule na kubaki kufanya kazi mitaani, sisi sote ni sawa lakini inashindikana ni wapi watoe taarifa waweze kutimiza ndoto zao,"alisema Beatrice Baraka (18) mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kidinda.

Wakati huo baadhi ya watoto walio katika vibarua hivyo walisema kuwa, wao hawapendi kuwa katika mazingira hayo kwani wao pia wanatamani wasome ili waweze kufanikiwa na kutimiza ndoto zao jambo ambalo kwao limekuwa haliwezekani tena.

 Adela 15 (jina sio halisi) ambae ni mfanyakazi za ndani alisema kuwa baada ya kumaliza darasa la saba shule ya msingi Mbiti wilayani Bariadi mwaka 2019, hakutakiwa kuendelea na shule tena kwa sababu baba yake hakuwa na uwezo wa kumnunulia sare za shule hivyo ilimlazimu kutafutiwa kazi za ndani ili aweze kusaidia familia.

"Nilikuwa natamani kuwa daktari lakini kwa sasa sitaki tena kwa sababu najua haiwezekani, ninafanya kazi ninalipwa tsh 30,000 ambayo inatumwa nyumbani ninabaki na tsh 10,000 kwa ajili ya matumizi yangu," alisema Adela.

Adela anatamani pesa anayopata walau abaki nayo ili aweze kununua vitu ambavyo vitamsaidia katika maisha yake ya baadae.

Agatha 15 (jina sio halisi) ambaye ni mhudumu wa ukumbi wa starehe, alisema baada ya kumaliza darasa la saba hakufanikiwa kuendelea na masomo kwa sababu familia yake ilihitaji mtu wa kusaidia ili wapate chakula hivyo ikamlazimu yeye kutafutiwa kazi ili asaidie familia.

"Siku ya mtihani wa darasa la saba nilipigwa nikavimba jicho, nilipokuwa kwenye mtihani sikuweza kufanya chochote hata matokeo yalivyoka nimefeli nilimuomba baba nirudie shule lakini hakuniruhusu kwa sababu ilibidi mimi nitafute pesa ili ndugu zangu wengine wasome," alisema Agatha.

Aliongeza kuwa anatamani kuwa Mfanyabiashara lakini haiwezekani kwa sababu malipo yake ya mwezi ni tsh 30,000 ambayo inatumwa kwa wazazi wake na anabakiwa na tsh 5000 pekee kwa ajili ya matumizi.

Wakati huo huo Ramadhani 14 (jina sio halisi) mtoto anayejishughulisha na kazi ndogo ndogo mtaani alisema kuwa, amezoea changamoto za mtaani na hivyo anafurahia maisha hayo kwa sababu hawezi kukaa nyumbani akaishi kwa kuongozwa na mzazi.

"Nikiwa darasa la nne niliacha shule nikaanza kufanya kazi na nikawa ninarudi nyumbani jioni, baadae nikaona isiwe shida baada ya kunisema sana ninalala kwenye banda la video na ninaishi tu mtaani lakini sifikilii kurudi nyumbani hata siku moja," Alisema Ramadhani

Uwepo wa kundi hilo la watoto katika mji wa Bariadi baadhi ya wazazi wametafsiri kuwa ni namna ya kumnyima mtoto uhuru lakini pia ni malezi ambayo watoto wanakuwa wanayapata tangu wakiwa katika familia ndiyo yanapelekea hali hiyo.

"Watoto hawa sio kama hawana kwao, lakini kunabaadhi wameamua kuishi maisha hayo japo kuna wale wanaotumwa ili kusaidia familia, na kingine kinacho haribu watoto ni hawa ma dada poa ambao wanapokuja kujiuza na baada ya kuondoka tabia hiyo wanakuwa wameiambukiza kwa watoto wetu waliopo kwenye makuzi," alisema Mama Najima.

Jambo hilo lilitolewa ufafanuzi na Afisa ustawi wa jamii mji wa Bariadi Janeth Jackson, Ambapo amesema tatizo hilo lipo lakini kwanza wazazi ama Jamii inatakiwa kujua wajibu wao kwa watoto, hasa pale wanapoona vitendo vya kikatili vinapotokea ama kufanyika kwa watoto Jamii inayo wajibu wa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika.

" Ninachoamini ni kwamba unapotoa taarifa fulani ni ngumu sana kwamba kila mtu itamfikia hasa ya kufikisha ujumbe kwa jamii na watoto walioko mashuleni,nikiwa na maana kwamba kwa wale ambao hawako shule ni sehemu ya jamii na hata kama hakuipata kupitia mimi basi yule aliyeipata tunahakikisha wanakuwa mabalozi wazuri kwa waliobaki," alionheza Janeth.

Aliongeza kuwa sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009 kifungu Cha 95 kinaitaja jamii kutoa taarifa kwa kitendo chochote Cha ukatili kikitokea ama kuhisi ukatili wa aina yoyote kutokea na jamii hailewi  juu ya wajibu wao wa kutoa taarifa kwa vitendo hivyo.

Mwisho.


Share:

TARI Naliendele Yaagizwa Kutafiti Mbegu Bora Zenye Mavuno Mengi Kwa Wakulima


Wizara ya Kilimo imekiagiza kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Naliendele kuongeza kasi ya utafiti wa mbegu bora nyingi za korosho na mazao ya mafuta ili wakulima waweze kuwa uhakika wa mavuno na kuinua kipato cha kaya.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema hayo jana mjini Mtwara alipotembelea kukagua shughuli za utafiti wa mbegu za korosho na mazao ya mafuta katika kituo hicho.

Kusaya amewataka watafiti wa kilimo kujikita katika kuzalisha mbegu bora za korosho kisayansi zenye kutoa mavuno mengi na kumsaidia mkulima kuwa na kipato cha uhakika.

“Bado tunalo deni la kugundua zaidi mbegu bora za mazao mengi tukiwa na lengo baada ya miaka kumi nchi ijitosheleze kwa mahitaji ya mbegu na kupunguza utegemezi toka nje ya nchi” alisisitiza Kusaya

Katibu Mkuu huyo aliwaeleza watafiti hao kuwa wanafanya kazi nzuri na serikali inatambua hilo lakini waongeze jitihada zaidi hususan kwenye upatikanaji wa mbegu nyingi bora za mazao ya mafuta kama ufuta, karanga na alizeti ili kuondoa tatizo la upungufu wa mafuta ya kula.

Aliongeza kusema kwa mwaka nchi inatumia shilingi bilioni 443 kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi wakati tunayo ardhi kubwa na bora inayofaa kwa uzalishaji mazao ya mafuta ikiwemo michikichi na ufuta.

“Rais Dkt.John Pombe Magufuli amekwisha agiza na kuiwezesha TARI kupata zaidi ya shilingi bilioni 1.7 mwaka huu kwa ajili ya utafiti wa mazao ya michikichi ili nchi iondokane na upungufu wa mafuta, ni jukumu lenu watafiti kuongeza uzalishaji wa mbegu bora za ufuta, alizeti na michikichi” alisema Kusaya.

 Lengo la wizara ya kilimo ni kuwa na aina nyingi za mbegu za mazao ikiwemo ufuta ,alizeti, michikichi, karanga na muhogo ili eneo ambalo halistawi korosho basi mkulima apande zao jingine la kumwingizia kipato na uhakika wa chakula alisema Kusaya.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha TARI Naliendele Dkt. Fortunus Kapinga alisema wamefanikiwa kugundua aina 54 za mbegu bora za korosho ambazo  zinazaa sana, kuvumilia magonjwa na kustawi maeneo mengi nchini.

Alitaja mafanikio mengine ya kituo hicho ni pamoja na uzalishaji wa mbegu bora za korosho  tani 106 (2017/18), tani 47.5 (2018/19) na tani 111.2 ambapo tayari   tani 82 zimesambazwa nchini katika msimu wa 2019/20.

“Tunatarajia kuzalisha tani 100 za mbegu bora za korosho msimu wa 2020/21 ili tuweze kuzisambaza kwenye mikoa yote 20 ambayo inalima korosho kwa sasa Tanzania” alisema Dkt Kapinga.

Dkt. Kapinga alimweleza Katibu Mkuu Kilimo kuwa lengo la kituo cha utafiti Naliendele ni kufungamanisha zao la korosho na mazao mengine ili kuwa na uhakika wa soko mfano kuzalisha maziwa ya korosho, kubangua korosho,  kutengeneza mvinyo wa korosho, kuzalisha mafuta ya alizeti na karanga nk

“Kwenye mabibo tumegundua unaweza kupata ‘Ethanol’ inayohitajika sana kwenye maabara na tayari Mkemia Mkuu wa Serikali ameithibitisha ubora wake” alisema Dkt.Kapinga .

Kuhusu Programu ya Utafiti  wa Mbegu za Mafuta na Mikunde Dkt. Kapinga alieleza mafanikio kuwa TARI Naliendele imegundua aina 9 za mbegu bora za ufuta,  aina 15 za karanga na aina 3 za alizeti ambazo zina mavuno mengi kwa wakulima.

Katibu Mkuu Kusaya alitembelea pia Chuo cha Mafunzo ya Kilimo (MATI) Mtwara ambapo alikipongeza kwa kufundisha wanafunzi na wakulima kwa vitendo kilimo cha zao la korosho kupitia mashamba darasa.

Kusaya aliwisihi watumishi wa chuo hicho kuwa wizara itaendelea kuwajengea uwezo wa kuwafanya wajitegemee zaidi kimapato kwa kuwapatia vifaa ikiwemo trekta na kuboresha miundombinu ya chuo hicho kiweze kuongeza udahili na tija katika mafunzo.

Naye Mkurugenzi wa Mafunzo ,Utafiti na Ugani toka Wizara ya Kilimo Dkt. Wilhem Mafuru alimshukuru Katibu Mkuu kwa jitihada zake za kuboresha utendaji kazi wa vyuo vyote 14 na vituo 4 vya mafunzo ya kilimo kwa kuvipatia fedha ya ukarabati, vifaa vya TEHEMA, magari na pikipiki hali inayoongeza morali kwa watumishi.

“Katibu Mkuu tunakushuru sana  tangu uingie wizarani umekuwa msaada kwa vyuo vya kilimo kwani tayari umeshatembelea vyuo 13 kati ya 14 hali inayotia imani kuwa sasa vinatambulika na vinaboreshwa“ alisema Dkt. Mafuru.

Kwa upande wake Maimuna Yakini akizungumza kwa niaba ya watumishi wa MATI Mtwara alisema anaishukuru serikali kwa kuweza kulipa madeni ya wazabuni kwenye vyuo vya kilimo na pia watumishi hali inayowafanya wawe na maisha mazuri.

“Tunakushuru sana Katibu Mkuu Kusaya kwa kututia moyo tufanye kazi kwa bidii na tunamwombea Mungu amsaidie Mhe.Rais Dkt.Magufuli ashinde uchaguzi ujao ili aendelee kutekeleza malengo yake katika kuinua sekta ya kilimo ikiwemo vyuo vyetu vya mafunzo” alihitimisha Maimuna.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Francis Alfred alisema lengo la wizara  ni kuongeza uzalishaji wa korosho toka tani 300,000 msimu wa 2019/20 hadi tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2023/2024 ambapo msimu huu uzalishaji unatarajia kuwa tani 278,000 za korosho ghafi.

Katibu Mkuu Kusaya amemaliza ziara yake mkoani Mtwara jana ambapo aliweza kushiriki kikao cha kujadili mkakati wa kuvipatia malighafi viwanda vya wabanguaji korosho wa ndani, kutembelea bodi ya korosho kuangalia maandalizi ya ununuzi wa korosho msimu wa 2020/21 na Chama Kikuu cha Ushirika Masasi/Mtwara (MAMCU).


Share:

WANAWAKE KISHAPU WAVUNJA MIZIZI YA MFUMO DUME… WAJITOSA KWA WINGI KUGOMBEA UONGOZI

Share:

Watakaoshindwa Kusimamia Fedha Za Mradi Wa Boresha Macho Watachukuliwa Hatua kali


Na.WAMJW-Dodoma.
SERIKALI imesema haitasita kumchukulia hatua Mganga Mkuu wa Mkoa au Wilaya atakayebainika kushindwa kusimamia fedha za Mradi wa Boresha Macho.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Dkt.Ntuli Kapologwe jana wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Boresha Macho unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la Sightsavers kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Uingereza(UKAID).

Dkt.Kapologwe amesema mradi huo unagharimu Shilingi za kitanzania Bilioni 6 “lazima kuwepo na usimamizi mkubwa wa fedha hizo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa”.

Ameendelea kusisitiza kuwa kama kuna Mganga mkuu ambaye atashindwa kusimamia vizuri fedha za mradi huo atajieleza kwanini hawezi kusimamia.

“Tuchukue mradi huu kama mtoto wetu na malengo tuliyoweka lazima yafanikiwe,hatutamvumilia mtu yeyote aidha anatoka shirika lisilo la kiserikali au serikalini ambaye hatatekeleza inavyotakiwa, kwasababi hizi fedha zimeletwa kwa ajili ya watanzania na wanapaswa kunufaika na kila uwekezaji unaofanywa kwenye macho,”Amesema Dkt.Kapologwe.

Aidha, Dkt. Kapologwe ameeleza kuwa suala la ubora wa kazi itakayofanyika ni la msingi ili mradi ufanyike kwa malengo yaliyokusudiwa huku akisema pale itakapobainika mradi hautekelezwi ipasavyo serikali haitasita kuchukua hatua.

“Kila senti moja ambayo imetolewa kwa ajili ya mradi huu lazima iwafikie walengwa ambao ni wananchi, sisi Tamisemi na Wizara ya Afya tutafanya ufuatiliaji wa karibu ili kuona kama kuna thamani ya fedha kwenye utekelezaji wa mradi huu, Sh.Bilioni sita za mradi tunataka tuone vitu,”Amesema.

Hata hivyo amesema serikali imekuwa ikiendelea kuimarisha huduma za afya kwa wananchi ambapo zimeshuka hadi ngazi za kijiji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Afya anayeshughulia magonjwa yasiyo ambukiza, Dkt.James Kiologwe, amesema asilimia moja ya watanzania wanakabiliwa na tatizo la uoni ambao unasababisha kupata upofu.

Hata hivyo, amesema asilimia 75 ya matatizo yanayosababisha upofu yanazuilika na Wizara ya Afya inajivunia kufanya kazi na wadau kuhakikisha idadi hiyo ya watu wanapata tiba ili wasipate upofu.

“Katika ushirikiano huo kuna mambo tunajivunia hadi sasa, tumeweza kuratibu vizuri wadau, tunajua katika viwango vya kimataifa tunatakiwa kuwa na hospitali moja ya kutoa huduma za upasuaji kwa watoto wanaopata matatizo ya macho, tunafurahi hadi sasa kuna hospitali nne ambazo zinauwezo huo,”.

Awali, Meneja Mipango na Mshauri Mwelekezi wa sightsaves Eng. Koronel Kema, amesema mradi huo utagharimu kiasi cha Sh.Bilioni sita na unatarajiwa kupima na kutoa huduma za macho kwa watu 150,000 huku kati yao 13,500 watakaobainika na mtoto wa jicho watafanyiwa upasuaji.

Aidha, amesema mradi huo pia utaongeza uelewa kwa watu 650,000 kuhusu umuhimu wa kupata huduma za macho.

“Mradi utafikia halmashauri tano kati ya tisa za Mkoa wa Morogoro na kwa Mkoa wa Singida Halmashauri zote tisa zitanufaika,”amesema.


Share:

Serikali Ya Tanzania yakanusha tuhuma Wakimbizi kulazimishwa kuondoka nchini


Na Mwandishi Wetu, MOHA, Arusha.
SERIKALI imekanusha tuhuma zilizotolewa na Waziri anayeshughulika na masuala ya Wakimbizi Nchini Uganda, kuwa Tanzania inawalazimisha Wakimbizi walipo katika kambi mbalimbali Nchini kurejea Burundi bila ridhaa yao.

Akizungumza katika warsha ya maandalizi ya uandishi wa kitabu cha historia ya hifadhi ya wakimbizi nchini, iliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha, Simbachawene amesema Tanzania inauzoefu mkubwa na ina historia kubwa katika kuwahifadhi na kuwatunza wakimbizi hivyo tuhuma hizo sio sahihi.

“Nimemsikiliza Waziri anayeshughulika na masuala ya wakimbizi wa Uganda katika kipindi cha BBC Dira ya Dunia akiwa anailaumu Tanzania kwamba inawafukuza wakimbizi na kuwalazimisha waingie Uganda, jambo hilo ni tuhuma nzito, Tanzania inauzoefu mkubwa na ina historia kubwa katika kuwahifadhi na kuwatunza wakimbizi, Tanzania haijawahi kufanya oparesheni wala shughuli yoyote kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda kuwarejesha au kufanya vyovyote vile,” alisema Simbachawene na kuongeza kuwa;

“Tunamshangaa huyu Waziri mwenzangu wa Uganda amelichukua wapi jambo hilo na kulisema kwenye vyombo vya habari vikubwa linatushangaza na kuonyesha masikitiko yetu na kama kulikuwa na njia nyingine tungewasiliana kwanza kwasababu tunafnaya kazi kwa pamoja kuliko hiki alichokifanya, sisi Tanzania ni wazoefu tumehifadhi sio tu wanaotoka nchi nyingine hata Wauganda wenyewe tuliwahifadhi, sasa leo hii sisi tuliowahifadhi wenyewe tukawe watu wabaya katika ukanda huu.”

Aidha, Simbachawene alisema, zaidi ya wakimbizi elfu saba kutoka nchi ya burudi wamejiorozesha kurudi nchini kwao kwahiari na taratibu za kuwarudisha katika nchi hiyo zinaendelea kufanyiwa kazi.

Simbachawene alisema Tanzania ina historia ya yakupokea wakimbizi nchini kwa zaidi ya miaka 60, na zaidi ya wakimbizi elfu tisini tayari walisharudi nchini mwao na hao wengine elfu saba tayari wameshajiorozesha kurudi nchini mwao kwa hiari na si kwakulazimishwa.

“Tanzania imekuwa ikipokea wakimbizi kabla ya Uhuru na baada ya uhuru na yote ni kusema nchi hii ina usalama na ulinzi mzuri kwa wakimbizi kwani takribani wapigania uhuru wa nchi za SADC walijihifadhi katika nchi ya Tanzania,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa, Tanzania ilipokea wakimbizi zaidi ya milioni 1.2 huku wakiwa na kambi 14 za kuhifadhi wakimbidhi hao katika miaka ya 1990, na hadi sasa makundi mengi ya kuhifadhi wakimbizi yamekuwa yakiwatoa wakimbizi katika makazi na kuwapeleka katika makambi maalumu kwa ajili ya usalama zaidi.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Dignity Kwanza, Janemary Ruhundura, ambayo ndiyo Taasisi iliyoandaa warsha hiyo, alisema dhumuni la kuandika kitabu hicho ni kuonyesha kuwa nchi ya Tanzania imekuwa kimbilio kwa wakimbizi hivyo kuna umuhimu wa kutambua nyakati zote za kuhifadhi wakimbizi.

Hata hivyo amesema kuwa mwaka 2003 nchi ya Tanzania ilitoa kibali Cha urai kwa wakimbizi 3000 pia wamatambua mchango mkubwa wa Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Nyerere kwani mwaka 1993 alipata tunzo kubwa ya kupokea na kuhifadhi wakimbizi nchini.

“Tunaandika kitabu hicho ili kuendelea kuwakumbusha wananchi pamoja na mataifa mbalimbali wajue nchi ya Tanzania ilivyopokea wakimbizi na inavyoendelea kuwapokea kwa usalama kwa muda mrefu,” alisema Ruhundura.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR), Antonio Canhandula, alisema nchi za Afrika Mashariki wakimbizi waliopo ni milion 4.2, hivyo nchi hizo zimekuwa na ushirikiano mkubwa katika kuwahifadhi Wakimbizi.

“Jukumu la kuwahudumia wakimbizi sio la Watanzania peke yake bali ni la Jumuiya ya Kimataifa ambapo michango mingi imetolewa na Jumuyiya hiyo kupitia taasisi, mbalimbali za kimataifa ikiwemo Shirika la UNHCR,” alisema Canhandula.

Naye Mkurugenzi wa Huduma kwa wakimbizi, Sudi Mwakibasi amesema Serikali imeridhia kutekeleza mpango mpya wa kimataifa wa kuhudumia wakimbizi ambao unalenga kupunguza mzigo kwa nchi ambayo zinahifadhi wakimbizi ambapo unawezesha wakimbizi kupeleka katika nchi ya tatu.


Share:

Wizara Kuweka Kipaumbele Cha Ajira Za Wauguzi Nchini

Na.WAMJW-Manyara
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatambua upungufu uliopo wa  wauguzi kwenye hospitali za rufaa za mikoa nchini na hivyo kuweka kama kipaumbele kwenye ajira Serikalini.
 
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka wizara ya afya Bi. Ziada Sellah wakati akiongea na wauguzi na wakunga kwenye Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara.
 
“Tayari wizara inatambua upungufu huo na kwamba ajira zitakapotoka vipaumbele vitakuwa ni kuongeza waguzi hospitalini  hapo” Alisema Bi. Ziada.
 
Licha ya upungufu wa wauguzi katika hospitali hiyo Mkurugenzi huyo pia amewataka wauguzi hospitalini hapo kuzingatia maadili ya kazi na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wagonjwa, ili wagonjwa  waweze kupata ahueni kwa kupatiwa huduma nzuri kutoka kwa wauguzi.
 
Aliongeza kuwa kila muuguzi nchini akumbuke kiapo alichokiweka kwa kuzingatia maadili na miiko ya muuguzi katika kumuhudumia mteja wake
 
Imetajwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara  inakabiliwa na upungufu wa  wauguzi 200. Upungufu huu ni zaidi ya asilimia 60% ya mahitaji.
 
Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga yupo kwenye ziara ya kikazi ya kukagua huduma za Uuguzi katika hospitali za Rufaa za mkoa ya Singida,Manyara,Arusha, Kilimanjaro na Arusha pamoja na hospitali maalum na kanda ili kusikiliza changamoto zinazoikabili kada hiyo ya wauguzi na kuzipatia ufumbuzi ili wauguzi waweze kufanya kazi zao katika mazingira rafiki.


Share:

Wimbo Mpya wa Alikiba – Mediocre

Alikiba ameachia Audio ya wimbo wake mpya ‘Mediocre’ Bonyeza Play hapa chini kuusikiliza.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger