Sunday 9 August 2020

SERIKALI YAISHUKURU SUA KWA KUSAIDIA UPIMAJI SAMPULI ZA WASHUKIWA WA COVID 19

Kaimu Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Maulid Mwatawala (Kulia) Akimkabidhi Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (Wapili kutoka kulia) kapu lililojaa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa Chuoni hapo.

Na Calvin Gwabara, Morogoro

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Mhe. Umma Mwalimu Amelia huku tu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na Wataalamu wake kwa msaada Mkubwa waliotoa katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa COVID 19.

Mhe. Mwalimu ameyasema hayo alipotembelea Banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwenye maonesho ya Wakulima nanenane Kanda ya Mashariki yanayofanyika Mkoani Morogoro kabla ya kufunga rasmi maonesho hayo Kikanda.

“Nitumie nafasi hii kuushukuru Uongozi mzima wa SUA na Watafiti wake kwa msaada Mkubwa mliotoa wakati wa mapambano ya COVID 19 Kwa kusaidia kwenye upimaji wa sampuli mbalimbali za wagonjwa kwa ubora mkubwa, Hakika Tina kila sababu ya kuwashukuru kwa jitihada hizi kubwa mlizozifanya” Alisisitiza Mhe. Umma Mwalimu.

Aliongeza “Wakati tunahangaika na zoezi la upimaji wa sampuli zilizokuwa zinakuja kwenye Maabara kuu kutoka nchi nzima mlitusaidia sana kupunguza mzigo wa upimaji sampuli zile baada ya nyinyi pia kuthibitika kuwa mnaweza kufanya kazi hii katika viwango vinavyokubalika”.

Waziri huyo wa Afya ametembelea mabanda mbalimbali ya maonesho na kujionea teknolojia na mbinu mbalimbali za Kilimo,Mifugo na Uvuvi kabla ya kufunga rasmi maonesho hayo ya Wakulima nanenane Kanda ya Mashariki.

Akiwa kwenye banda la SUA alijionea vifaa mbalimbali vya maabara na wataalamu ambao walishiriki kwenye zoezi hilo na Upimaji wa sampuli za washukiwa na Ugonjwa wa COVID 19 sambamba na Hospitali pekee Taifa ya Rufaa ya wanyama iliyopo  chuoni hapo.

Waziri huyo wa Afya pia amepata nafasi ya kujionea Wataalamu na wajasiliamali wa masuala ya Lishe kutoka SUA ambao wanazalisha bidhaa mbalimbali kutokana na mazao lishe na kuwataka kuanza kufungasha bidhaa zao kwaajili ya wanunuzi wadogo kwa bei nafuu ili hata watoto waweze kununua kwa hela ndogo.

Maonesho hayo ya Wakulima nanenane yamefanyika kwenye Kanda mbalimbali na yalianza tarehe 1/8/2020 na kufikia kilele tarehe 8/8/2020 lakini Serikali imeongeza siku mbili ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kujifunza na pia waonyeshaji kufanya biashara zao.

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kama Mdau Mkubwa wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi kimeshiriki kwenye maonesho hayo Kitaifa Mkoani Simiyu na Kikanda kwenye Kanda ya Mashariki Mkoani Morogogoro.

Maonesho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi chagua viongozi Bora Mwaka 2020”.
Share:

LORI LA MAFUTA LALIPUKA NA KUZUA TAHARUKI KAHAMA MJINI..LAJERUHI NA KUHARIBU MALI


Muonekano wa tanki la mafuta baada ya mfuniko wake kuripuka gari likitengenezwa Kahama Mjini.

Na Salvatory Ntandu - Malunde 1 blog Kahama
Kijana ambaye jina lake halijafahamika mara moja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30 amenusurika kifo kwa kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya mfuniko wa tenki la mafuta la gari lenye namba za usajili namba T 393 BEZ kulipuka katika eneo la Bijampola Mjini Kahama likifanyiwa matengenezo.

Wakizungumza na Malunde 1 Blog baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, Baraka John amesema kuwa akiwa katika eneo lake la kazi majira ya saa tatu asubuhi leo Jumapili Agosti 9,2020 wakati mafundi wa kuchomelea magari wakiwa wanalifanyia matengenezo gari hilo ghafla lililipuka na kusababisha madhara mbalimbali.

Amesema Mafundi waliokuwa wanatengeneza gari hilo hawakuchukua tahadhari ili kujiridhisha kama kuna mafuta yaliyosalia kabla ya kuanza kulichomelea hali iliyosababisha kujitokeza kwa mlipuko huo ambao umesababisha majeruhi mmoja na kuharibu mali mbalimbali katika eneo hilo ikiwemo vibanda na nyumba.

“Magari kama haya yanayobeba vimiminika vinavyolipuka ni bora yakazuiwa kufanyiwa matengenezo katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu au kwenye makazi ya watu,serikali ipige marufuku uchomeleaji wa magari haya mitaani kwani ni hatari kwa usalama,”amesema John.

Naye Joyce Paulo anayejihusisha na shughuli ya kuuza vyakula 'Mamalishe' katika eneo la Bijampola amesema kuwa tukio hilo limezua taharuki kubwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo kwani mlipuko huo ulikuwa ni mkubwa na baadhi ya vyuma vilikuwa vinaruka katika maeneo mbalimbali huku moshi mkubwa ukiwa unasambaa kwa kasi katika makazi ya watu.

“Tulidhani ni bomu limelipuka katika eneo letu kwani nyumba ya jirani yetu imeharibiwa sana na baadhi ya vyuma vilivyokuwa vinajitokeza baada ya kulipuka,tunaiomba serikali idhibiti uegeshaji ovyo wa magari yenye mafuta katika eneo hili,”amesema Joyce.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama, Dk Lucas David amethibitisha kupokea majeruhi mmoja ambaye ametokana na ajali ya kulipuka kwa tanki la Mafuta iliyotokea leo katika eneo la Bijampola ambaye amepata majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wake na anaendelea kupatiwa matibabu.

“Kwa sasa amepelekewa katika chumba cha X-ray kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi,anaonekana amepata mivunjiko katika maeneo mbalimbali ya mwili wake",amesema Dk. David.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio na kwamba atatoa taarifa rasmi.
Muonekano wa tanki la mafuta baada ya mfuniko wake kuripuka gari likitengenezwa
Nyumba ikiwa imeharibika baada ya mfuko wa tanki la mafuta kuripuka gari likitengenezwa
Share:

UTEUZI MPYA ULIOFANYWA NA RAIS MAGUFULI LEO




Share:

Waziri Mkuu Akagua Ukarabati Wa Mv New Victoria.....Aitaka Mamlaka Inayosimamia Ihakikishe Kuwa Wiki Ijayo Meli Inaanza Kazi

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekagua ukarabati  mkubwa wa meli ya MV New Victoria Hapa Kazi tu na kuagiza mamlaka inayosimamia ihakikishe kuwa kuanzia wiki ijayo meli hiyo inaanza kazi ya kusafirisha abiria na mizigo kwa kuwa ukarabati umekamilika na sasa inaendelea kukaa tu  hali ambayo ni hasara kwa Serikali.

Pia, Waziri Mkuu ametoa siku mbili kwa mamlaka inayohusika na utoaji wa kibali cha kuanza kazi kwa meli hiyo ihakikishe inatoa kibali hicho haraka na  ratiba ya safari itangazwe kwa sababu  Watanzania wanahamu  ya kuanza kuhuduiwa na meli hiyo.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Agosti 9, 2020) baada ya kukagua meli hiyo ambayo tayari imeshafanya safari ya majaribio  kwa  kusafirisha  abiria kutoka Mwanza hadi Bukoba mkoani Kagera ambako ilirudi na abiria na mizigo.

Maeneo aliyokagua kwenye meli hiyo ni pamoja na vyumba vya abiria vikiwemo vyumba maalumu kwa ajili ya huduma za mama na mtoto, chumba cha kuongozea meli, vyumba vya migahawa na chumba cha injini.

“Nimeona ukarabati mkubwa uliofanywa, nimeona injini mpya, meli imekamilika na ilishafanyiwa majaribio ya aina zote kubeba abiria na kubeba mizigo na wataalamu wamejiridhisha kuwa inauwezo wa kubeba abiria na mizigo.”

Waziri Mkuu ameongeza kuwa “Haya yote ni mawazo na mipango ya Rais Dkt. John Magufuli pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015-2020. Tumetekeleza na tunaendelea kutekeleza.”

Baada ya kukagua meli ya MV New Victoria Hapa Kazi Tu, Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa chelezo pamoja na meli mpya na alieleza kuwa ameridhishwa na kazi inayoendelea kufanyika na amewataka Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali yao.

Awali, Meneja Miradi ya Kimkakati inayotekelezwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Luteni Kanali Vitus Mapunda alisema miradi hiyo minne ya ukarabati mkubwa wa meli ya Mv Victoria Hapa Kazi Tu, MV Butiama Hapa Kazi Tu, ujenzi wa chelezo na ujenzi wa meli mpya inayojulikana kama MV Mwanza Hapa Kazi Tu itagharimu sh. 152,916,249,842.

Alisema ukarabati wa meli ya MV New Victoria Hapa Kazi Tu yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mizigo tano 400 umegharimu sh. 22,712,098,200. Meli hiyo itatoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo kati ya bandari ya Mwanza Kaskazini, Kemendo na Bukoba.

“MV Butiama itakayobeba abiria 200 na mizigo tani 100 ukarabati wake umegharimu sh. 4,897,640,000. Meli hiyo itatoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo kati ya bandari ya Mwanza Kaskazini na Nansio Ukerewe. Ukarabati wa chelezo umegharimu sh. 36,152,511,642 na ujenzi wa meli mpya utagharimu sh. 89,154,000,000.”

Alisema kukamilika kwa miradi hiyo ya kimkakati kutafungua fursa nyingi za ajira binafsi na kupunguza gharama za usafirishaji sambamba na kuongeza tija katika shughuli za biashara hivyo kuwafanya wananchi wanyonge wengi kunufaika. Ujenzi wa Meli mpya unatarajiwa kukamilika Agosti 2021.

(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Wasimamizi wa uchaguzi msivuruge amani ya nchi

Na Samirah Yusuph Simiyu
Wasimamizi wa uchaguzi wameaswa kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi na kutokujihusisha na vitendo viovu ambavyo vitaashiria kuharibu uchaguzi na kuvuruga amani ya nchi

Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa uchaguzi mkoa Simiyu Saimon Maganga, alipokuwa akifungua mafunzo ya kuwaandaa wasimamizi wa uchaguzi mjini bariadi.

Maganga alisema kuwa wameaminiwa kubeba jukumu hilo zito kwa hiyo na wao wajiaminishe kwa kufanya kazi kwa utii bila kukiuka kanuni na muongozo ambao umetolewa na tume ya uchaguzi.

" Tunaimani na nyinyi na tunaamini baada ya uchaguzi tutakuwa na amani yetu, msitumike katika kuharibu uchaguzi mkafanye kile kilichokusudiwa na tume yetu kwa uaminifu na uadilifu mkubwa," alisema maganga.

Wakizungumza kuhusu mafunzo wanayo yapata baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi wamesema mafunzo hayo yanawajengea uelewa mpana kuhusu uchaguzi na kuahidi kuwa waadilifu.

"Hapa nimeelewa zaidi wajibu na majukumu yangu kama msimazi msaidizi wa uchaguzi na kwa uelewa huu ninaimani nitafanya vizuri na kufuata taratibu zote," alisema Paul Susu.

"Hapa nimeelewa vifaa ninavyo paswa  kuwa navyo kama msimamizi na inapaswa nitanye nini ninapokuwa katika kituo changu cha kazi," aliongeza Chenya Lugiko.

Mwisho.


Share:

NIDA yafunga mitambo mipya kumaliza tatizo la vitambulisho

Na Samirah Yusuph
Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA imefunga mitambo miwili ya kisasa kwa ajiri ya kukamilisha uzalishaji wa  vitambulisho uliokwama.

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa mamlaka hiyo Geofrey Tengeneza alisema, hapo awali mitambo ilichakaa na kufikia hatua ya kuzalisha vitambulisho 200 hadi 500 kwa siku hali iliyofanya kuwa na mrundikano wa vitambulisho ambavyo vinasubiri kutengenezwa.

"Katika kituo chetu kikuu cha uzalishaji mitambo ilichoka na ikawa inazalisha kwa kiwango kidogo na hiyo ilitufanya kishindwa kufikia malengo yetu ya kutoa vitambulisho kwa wakati," alisema.

Aliongeza kuwa, kwa sasa wamejipanga kumaliza tatizo hilo kwa sababu wamefunga mitambo mikubwa ambayo kwa saa moja itazalisha vitambulisho 4500. na kwa siku vitazalishwa 144,000.

"Mitambo tuliyoifunga kwa sasa tunaamini ndani ya muda mchache tutamaliza zoezi la kutoa vitambulisho, niwaombe wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi ili wapate vitbulisho na ambao tayari wana namba waende ofisi za mtaa wakachukue vitambulisho.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kutunza vitambulisho vyao, kwani umapo poteza atakibidi kuweza kulipia kiasi cha Sh 20000 kwa ajili ya kitambulisho kingine.

"Watu wengi wanakuwa hawapo makini katika kutunza vitambulisho hivi niwatake wananchi kuvitunza kwa dhati kuepuka usumbufu pindi kipoteapo," alisema.



Share:

Waziri Mkuu Apongeza Ujenzi Wa Mradi Wa Kuongeza Uwezo Wa Kuhifadhi Nafaka Unaotekelezwa Na NFRA

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa amepongeza ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa Mradi unaotekelezwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo jana tarehe 8 Agosti 2020 wakati alipotembelea Banda la NFRA kabla ya kuhitimisha maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Waziri Mkuu amesema kuwa ujenzi huo ni mahususi kwa ajili ya Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi Nafaka kutoka tani 251,000 hadi tani 501,000.

Akitoa taarifa ya Mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Ndg Milton Lupa amesema Mradi huo unajumuisha ujenzi wa vihenge 56 na maghala ya kisasa 9 ambavyo kwa pamoja vinaongeza uwezo wa kuhifadhi kwa tani 250,000. Kwa sasa Mradi huu umefikia umefikia asilimia 75 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Amesema Uhifadhi wa nafaka kwa kutumia maghala ya kawaida, akiba inaweza kuhifadhiwa kwa takriban miaka mitatu tu kabla ya kuanza kupoteza ubora. Kwa kutumia vihenge vya kisasa, akiba inaweza kuhifadhiwa hata kwa zaidi ya miaka mitano bila kupoteza kiwango cha ubora

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ni Taasisi ya Umma chini ya Wizara ya Kilimo iliyoanzishwa chini ya Sheria za Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 na kuanza kazi rasmi tarehe 1 Julai, 2008.

NFRA ina jukumu kuu la kuhakikisha usalama wa chakula ndani ya nchi kwa kununua, kuhifadhi na kutoa chakula katika maeneo yenye upungufu na kwa waathirika wa majanga mbalimbali.

MWISHO


Share:

NFRA Yang’ara Maonesho Ya Naneane Kitaifa Simiyu, Kongole Wizara Ya Kilimo Yashika Namba Moja

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA umeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye tuzo zilizotolewa kwa washindi walioshiriki kwenye maadhimisho ya wakulima (Nanenane) yanayofanyika kwenye Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu kwa kupata Pointi 72.9

Tuzo hiyo ya NFRA ina maana kubwa kwani umewaacha nyuma washindani wengine ambao ni Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyoshika nafasi ya pili kwa kupata Pointi 70.3 na mshindi wa tatu ambaye ni Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania-TASAC kwa kupata Pointi 68.9

Kwa upande wa tuzo za Wizara katika maonesho hayo ni Wizara mama ya Kilimo ndio imewaning’iniza wenzake kwa kuongoza kwa Pointi 91.7 huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi yenye Pointi 87.1 na nafasi ya tatu imechukuliwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEM).

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kombe la ushindi Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya amewashukuru wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa wa uandaaji wa maonesho hayo jambo lililopelekea kuibuka washindi.

Kusaya amesema kuwa maonesho hayo yatakuwa endelevu ili wakulima waendelee kunufaika na elimu inayotolewa kuhusu mbinu bora za kilimo ikiwa ni pamoja na matumizi ya zana bora za kilimo.

Maadhimisho ya wakulima (NANENANE) yamefika ukomo jana tarehe 8 Agosti 2020 ambapo mgeni rasmi aliyefunga maonesho hayo kitaifa Mkoani Simiyu Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa amezipongeza Wizara zote za kisekta zinazohusika na kilimo, Taasisi za Umma na binafsi kadhalika wakulima na wananchi wote walioshiriki katika Maonesho hayo.

MWISHO


Share:

Naibu Waziri Mabula Ataka Mikakati Kukamilisha Ujenzi Mradi Hospitali Ya Kwangwa

Na Munir Shemweta, WANMM MUSOMA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa, Wizara ya Afya pamoja na Mshauri Mwelekezi wa mradi Chuo Kikuu cha Ardhi kukutana na kupanga mikakati kuhakikisha ujenzi mradi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mara (KWANGWA) unakamilika kwa wakati.

Hatua hiyo inafuatia kusuasua kukamilika  ujenzi wa mradi huo unaogharimu takriban Shilingi bilioni 15.082 kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya mara kwa mara yanayotolewa na Mshauri Mwelekezi kwenye maeneo ya ujenzi wa mradi.

Dkt Mabula ametoa kauli hiyo jana alipotembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara maarufu kama Kwangwa unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Mara pamoja na miradi inayofanywa na NHC.

Alisema, ujenzi wa mradi wa hospitali ya Rufaa mkoa wa Mara ni mzuri na ni wa kimakakati lakini kwa jinsi unavyoendelea unaweza usikidhi kiu na matakwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano John Magufuli kuona mradi huo unakamilika kwa wakati.

‘’ Nashauri pande zote tatu zikae tena na kuwekeana mikakati ya uhakika kuona  kazi inakamilika vipi na wanakwendaje katika kuhakikisha mradi huu unakamilika’’ alisema Dkt Mabula.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri Mabula, Mshauri Mwelekezi ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi mara nyingi amekuwa hayuko kwenye eneo la ujenzi na amekuwa akileta mabadiliko katika ujenzi jambo alilolieleza kuwa linaongeza gharama na kurudisha nyuma kasi ya ujenzi.

Alisema, kutokuwepo eneo la ujenzi muda wote kwa Mshauri Mwelekezi kunasababisha ujenzi huo kuchelewa na baadhi ya kazi kufumuliwa upya kwa maelekezo ya mshauri jambo linalosababisha mradi kutoisha kwa wakati na kutaka Mshauri huyo kuwepo eneo la ujenzi muda wote ili kumfanya mkandarasi (NHC) asichelewe kumaliza kazi zake .

Dkt Mabula aliongeza kuwa, ratiba ya NHC ni kukamilisha Sehemu C ya mradi huo katika Jengo la Huduma ya Mama na Mtoto Agosti 15, 2020 lakini baadhi ya sehemu imeelekezwa kubomolewa wakati mkandarasi yuko hatua ya umaliziaji jambo linalofanya mradi kutokamilika kwa wakati.

Ameitaka Wizara ya Afya kumbana mshauri Mwelekezi ili aweze kufanya kazi yake vizuri ili Shirika la Nyumba la Taifa lifanye kazi yake bila kukwama na wakati huo lisiongeze gharama za ujenzi kwa kuwa Shirika linategemea fedha za miradi katika kujiendesha.


Share:

Walioshindwa Kuzifuata Hati Za Ardhi Bunda Wamkera Naibu Waziri Mabula

Na Munir Shemweta, WANMM BUNDA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameshangazwa na wananchi wa wilaya ya Bunda waliomilikishwa ardhi kushindwa kujitokeza kuchukua hati pamoja na kutangaziwa siku ya kukabidhiwa hati zao.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanzisha utaratibu kupitia ofizi zake za mikoa kuwapelekea Hati wananchi karibu na maeneo yao ili kuwapunguzia usumbufu wa kuzifuata hati kwenye ofisi za mikoa.

Awali waliomilikishwa ardhi walitakiwa kusafiri umbali mrefu kufuata hati za ardhi ofisi za ardhi za kanda zilizokuwa zikihudumia mikoa zaidi ya mitatu jambo lililowafanya wamiliki hao kutumia gharama kubwa kufuatilia hati ofisi ya kanda.

Katika kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi pamoja na kupunguza gharama kwa wananchi kuzifuata huduma hizo kwa umbali mrefu  Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Julai mwaka huu imezindua ofisi za ardhi za mikoa zinazotoa huduma zote zilizokuwa zikitolewa katika ofisi za kanda. Huduma hizo ni pamoja na upimaji, uthamini, usajili na utoaji hati za ardhi pamoja na shughuli za mipango miji.

Akiwa wilayani Bunda jana katika ziara yake ya kikazi kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na miradi inayoendeshwa na Shirika la Nyumba la Taifa, Naibu Waziri Ardhi Dkt Mabula alishangazwa na idadi ndogo ya wananchi waliomilikishwa ardhi kujitokeza kuchukua hati zao  wilayani Bunda ambapo kati ya wamiliki 143 ni wamiliki sita (6) tu kati ya hao waliojitokeza kuchukua hati.

Naibu Waziri Mabula alisema, inashangaza kuona idadi ndogo ya wamiliki wa ardhi kujitokeza kuchukua hati wakati Wizara ya Ardhi imeamua kuwapelekea hati karibu na maeneo jambo linaloweza kuwasababisha kutumia gharama kuzifuata hati ofisi ya Msajili katika ofisi ya Ardhi mkoa wa Mara.

Katika ziara yake mkoani Mara Dkt Mabula alitembelea pia wilaya za Butiama, Tarime, Rorya na Musoma ambapo alizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi katika wilaya hizo, kuangalia ukusanyaji kodi ya ardhi sambamba na kugawa Hati za Ardhi kwa wananchi waliokamilisha taratibu za kumilikishwa ardhi.


Share:

Mashindano ya Masumbwi Kitaifa kufanyika Manyara

Na John Walter-Babati, Manyara
Kamati ya mchezo wa Masumbwi mkoa wa Manyara imeeleza kuwa mkoa huo umepewa heshma ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya kumtafuta bingwa wa ngumi kitaifa ambayo yatashirikisha vilabu vyote vya ngumi nchini vikiwemo vya majeshi ya ulinzi na usalama.
 
Mkuu wa mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti amesema, Shirikisho la ngumi Tanzania limeamua kuleta mashindano hayo makubwa katika mkoa wa Manyara ambayo yatafanyika kuanzia septemba 6,2020 katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati.
 
Amesema Mashindano hayo yatatanguliwa na pambano la mchujo Agosti 15 mwaka huu ili kupata wachezaji bora watakaounda timu ya mkoa wa Manyara itakayoshiriki Mashindano kitaifa.
 
Mkirikiti amewahakikishia washiriki wote wa ngumi nchini kuwa mkoa wa Manyara umejipanga vyema kuwapokea na kufanikisha jambo hilo la kitaifa kumpata bingwa.
 
Amesema ni fursa kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Manyara kujitokeza kudhamini na kutangaza biashara zao kupitia mashandano hayo makubwa yanayotarajiwa kuhudhuriwa na mamia ya watu kutoka kote nchini.
 
Kwa upande mwingine amewakumbusha wadau wote wa mchezo wa masumbwi watakaohudhuria mashindano hayo kutembelea mbuga za wanyama zilizopo katika mkoa huo,  Tarangire na Manyara kujionea vivutio mbalimbali.
 
Afisa Michezo mkoa wa Manyara Charles Maguzu amesema kuwa wamepata heshima hiyo kutokana na ulingo wa kisasa ambao upo katika mkoa huo pekee na ule wa jeshi .
 
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya ngumi mkoa wa Manyara Bwana Nicolous Mwaibale amesema mpaka sasa maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba timu ipo vizuri na itaingia kambini Jumatatu Agosti 10 ikiwa na wana masumbwi takribani 20.


Share:

Naibu Waziri Dkt Angeline Mabula Amtembelea Mjane Wa Baba Wa Taifa Butiama

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amemtembelea Mjane wa Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Butiama mkoa wa Mara.

Dkt Mabula alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani Butiama kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi sambamba na kugawa hati za ardhi kwa wananchi wa Butiama mkoani Mara waliopimiwa na kumilikishwa maeneo yao.

Naibu Waziri mbali na kutembelea wilaya ya Butiama pia alitembelea wilaya za Musoma, Rorya na Tarime ambako alizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi, alikagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi na kufuatilia maelekezo aliyoyatoa kuhusiana na masuala ya ardhi. 


Share:

Bilioni 15 Zatumika Kukopesha Pembejeo Kwa Wakulima-Kusaya

Serikali ya Awamu ya Tano imetumia shilingi Bilioni 15 kwa ajili mikopo ya pembejeo kwa wakulima tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015.

Kauli hiyo imetolewa jana (08.08.2020) na Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Gerald Kusaya kwenye viwanja vya maonesho ya Nanenane Nyakabindi mkoani Simiyu wakati akikabidhi matrekta mawili kwa wakulima wa wilaya Meatu 


“ Rais Dkt.John Pombe Magufuli amekwisha toa zaidi ya shilingi Bilioni 15 kwa ajili ya mikopo ya pembejeo kwa wakulima tangu alipoingia madarakani iliyosaidia kukuza sekta ya kilimo kwa kuongeza matumizi ya zana bora za kilimo” alisema Kusaya


Kusaya aliongeza kusema kuwa Wizara ya Kilimo kupitia Mfuko wa Pembejeo (AGITF) umekwisha toa jumla ya mikopo 314 wakulima na kuchangia upatikanaji wa ajira 364 kwenye viwanda vitatu vya kuchakata mbegu za mafuta nchini.


Katika hafla hiyo, wakulima wawili Juma Mpina toka Kisesa Magu na Pius Machungwa toka Meatu walikabidhiwa matrekta mawili kila moja likiwa na thamani ya shilingi milioni 60 ikiwa ni mkopo toka AGITF.


“Leo nimekabidhi matrekta mawili kwa wakulima hawa, nitumie fursa hii kuwahamasisha wakulima kuja Wizara ya Kilimo kupata mikopo kwa mtu mmoja moja au kikundi kwa riba ya kati ya asilimia 6 hadi 7 katika kipindi cha miaka miwili” alisisitiza Katibu Mkuu.


Mfuko wa Pembejeo hutoa asilimia 90 ya fedha zinazohitajika  kwenye mkopo wa trekta na mkulima anatoa asilimia 10 inayotakiwa ambapo lengo la serikali ni kuwezesha wakulima wengi kupata pembejeo bora na zenye gharama nafuu ili kukuza uzalishaji wa mazao ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.


Mwisho


Share:

Logistics & Marketing Coordinator at Pyxus Agriculture Tanzania Limited

Pyxus Agriculture Tanzania Limited Logistics & Marketing Coordinator Company: Pyxus International, of which Pyxus Agriculture Tanzania Limited (PAT) is a subsidiary, is a global agricultural company united behind a common purpose – to transform people’s lives so that together we can grow a better world. With 145 years’ experience delivering value-added products and services to […]

The post Logistics & Marketing Coordinator at Pyxus Agriculture Tanzania Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

TCRA YANG'AA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA 'NANE NANE' 2020...YATWAA KOMBE



Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa Mshindi wa kwanza katika kundi la Mamlaka ya Udhibiti wa Bidhaa na Huduma kwenye Maonesho ya Wakulima Nane Nane 2020 kitaifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu ikiwa na Kauli mbiu ya 'Tumia Mawasiliano kwa maendeleo ya kilimo mifugo na uvuvi,Chagua viongozi bora 2020. Pichani kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akimkabidhi kombe la ushindi Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo. (Picha na TCRA).


Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akimkabidhi kombe la ushindi Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo.
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo akifurahia kombe la ushindi wa kwanza katika kundi la Mamlaka ya Udhibiti wa Bidhaa na Huduma kwenye Maonesho ya Wakulima Nane Nane 2020 kitaifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.
Maafisa kutoka TCRA Kanda ya Ziwa Mashariki wakifurahia kombe la ushindi wa kwanza katika kundi la Mamlaka ya Udhibiti wa Bidhaa na Huduma kwenye Maonesho ya Wakulima Nane Nane 2020 kitaifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.
Maafisa kutoka TCRA Kanda ya Ziwa Mashariki wakifurahia kombe la ushindi wa kwanza katika kundi la Mamlaka ya Udhibiti wa Bidhaa na Huduma kwenye Maonesho ya Wakulima Nane Nane 2020 kitaifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.
Maafisa kutoka TCRA Kanda ya Ziwa Mashariki wakifurahia kombe la ushindi  wa kwanza katika kundi la Mamlaka ya Udhibiti wa Bidhaa na Huduma kwenye Maonesho ya Wakulima Nane Nane 2020 kitaifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.

Mkuu wa TCRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Asajili John (kulia) akikabidhiwa Kombe la Ushindi wa Kwanza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson katika Maonyesho ya Nane Nane Nyanda za Juu Kusini

Maafisa kutoka TCRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakiwa na ngao na cheti cha ushindi kundi la Mamlaka ya Udhibiti wa Bidhaa na Huduma kwenye Maonesho ya Wakulima Nane Nane 2020 Nyanda za Juu Kusini.
Share:

Picha : MKURUGENZI MKUU WA TIGO KATIKA MAONESHO YA NANE NANE MKOANI SIMIYU


Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo, Bw. Simon Karikari akinawa mikono kama moja ya njia za kujikinga na Ugonjwa wa Corona mara alipotembelea katika maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu. 
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo, Bw. Simon Karikari akipata maelezo mbali mbali kutoka kwa maafisa wa Tigo kuhusu huduma na ofa mbalimbali Katika maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya nyakabindi Mkoa wa Simiyu. 
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo, Bw. Simon Karikari akizungumza na maofisa wa Tigo mara alipotembelea katika maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo, Bw. Simon Karikari akisikiliza maelekezo kutoka kwa ofisa kutoka Moja ya Mabanda ya bodi za kilimo mapema leo alipotembelea katika maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo, Bw. Simon Karikari akipata maelezo kuhusu Ofa mbali mbali zinazotolewa katika Banda la Tigo mara alipotembelea katika maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu.
Burudani zikiendelea katika jukwaa la Tigo wakati wa Maonesho ya Nane Nane yakiendelea katika vivanda via Nyakabindi Mkoani Simiyu 

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili August 9















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger