Thursday 9 July 2020

Waziri Mkuu wa Ivory Coast afariki dunia ghafla

Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Amadou Gon Coulibaly, amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo Alhamisi akiwa na umri wa miaka 61.

Shirika la habari la IRIB limeripoti habari hiyo na kumnukuu Rais Alassane Ouattara wa Kodivaa akitangaza jana usiku kwamba Ivory Coast imeingia kwenye msiba wa kuondokewa ghafla na Coulibaly.

Aidha amesema, Waziri Mkuu Coulibaly alishiriki kwenye kikao cha kila wiki cha Baraza la Mawaziri la serikali ya Kodivaa, hali yake ikawa mbaya na amefariki dunia hospitalini.

Mwezi Machi mwaka huu, Coulibaly aliteuliwa na chama tawala wa Ivory Coast kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho ili kumrithi Rais Alassane Ouattara.
 
Waziri Mkuu huyo alirejea nchini Kodivaa tarehe pili mwezi huu wa Julai baada ya kupitisha muda mrefu wa matibabu nchini Ufaransa. Aliwahi kufanyiwa operesheni ya moyo mwaka 2012.

Ouattara amemtaja Colibaly kwamba alikuwa mtu wake wake wa karibu mno katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Haikuweza kujulikana haraka ni nani atateuliwa kushika nafasi yake ya kugombea urais wa tiketi ya chama tawala katika nchi hiyo ambayo ni mzalishaji mkubwa wa cocoa duniani.


Share:

Watiania Ubunge Wa CCM Mkoa Wa Iringa Waonywa Kuzingatia Sheria Na Kanuni Za Chama

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
KAMATI ya siasa ya chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Iringa imewata watiania na wanachama kuheshimu kanuni na sheria za uchaguzi zilizowekwa ndani ya chama ili kuepuka panga linaloweza kujitokeza pindi watakapo kiuka taratibu za chama.

Mwenyekiti wa kamati ya siasa Mkoa wa Iringa Abel Nyamahanga ameyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa ccm mkoa wa Iringa na kusema kuwa watia nia wanatakiwa kupita ofisi za wasimamizi wa uchaguzi ili kupewa taratibu za uchaguzi.

Nyamahanga alisema chama hakitasita kumchukulia hatua mwanachama na mtia nia ambaye atakiuka sheria na taratibu za uchaguzi.

Alisema kuwa kila kitu kinachofanywa na chama cha mapinduzi kipo kwenye kanuni za uchaguzi za chama hicho hivyo watia nia kwenye ngazi za udiwani na ubunge wanatakiwa kufuata kanuni hizo ili waweze kutia nia bila kuwa na kashfa.

“Tunacho kizungumza hapa kila kitu kipo kwenye miongozo na kanuni za chama chetu cha mapinduzi (CCM) ndio maana tunawataka watia nia wote kufuta kanuni na taratibu za chama wakati wa nia yake ya kutafuta nafasi ya kuwatumiakia wananchi” alisema Nyamahanga

Nyamahanga aliwataka wanachama na watia nia wote kuheshimu kanuni za uchaguzi ndani ya chama cha mapinduzi ili kuondokana na tatizo la rushwa ambalo miaka mingi kipindi cha uchaguzi ndio huaribu taswiara ya chama cha mapinduzi.

Aidha Nyamahanga aliwataka watia nia waache mara moja kupita kwenye kata na matawi kwa lengo la kukutana au kuwasalimia wapiga kura badala yake wanatakiwa kupita katika ofis za wasimamizi wa uchaguzi ili wapate taratibu na mwenendo wa uchaguzi unaokubarika ndani wa chama hicho.

 Alisema wapo baadhi ya watia nia wamekuwa wakiwakusanya  wapiga kura kutoa maeneo mbalimbali kwa kisingio cha kuwasalimia,kujitambulisha  na kuwapa nauli ikithibitika kwa mgombea yoyote yule ataondolewa kwenye orodha ya wagombea kwa mujibu wa ibara ya 35 kifungu kidogo cha kumi na sita.

Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu (CCM) Taifa Salim Asas alisema kuwa serikali ya chama cha mapinduzi imeleta maendeleo kwa wananchi hivyo wanauhakika wa ushindi katika uchaguzi mkuu.

Alisema kuwa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa kitashinda kwa kishindo majimbo yote hata jimbo la Iringa mjini ambalo lipo upinzani nalo watashinda kwa kuwa chama hicho kimejipanga vilivyo kuhakikisha hakuna makundi ili kuhakikisha kwenye uchaguzi mkuu wanaenda kwenye uchaguzi wakiwa wamoja.

Aliongeza kuwa wananchi wa manispaa ya Iringa wamekuwa na imani na utendaji wa kazi wa chama cha mapinduzi hivyo itakuwa kazi nyepesi kushinda kwa kuwa wanauhakika wa kumpata mgombea mwenye uwezo wa kupeperusha pendera ya chama hicho.


Share:

Waziri Kairuki Ahamasisha Kilimo Cha Pamoja Same

Na Dixon Busagaga ,Same.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki,ameutaka uongozi  wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, kuhamasisha wananchi kulima kilimo cha pamoja,hususani yale mazao yenye uhitaji mkubwa katika viwanda, ili kuwezesha kilimo chenye tija na upatikanaji wa masoko ya uhakika.

Kairuki ametoa Rai hiyo jana, wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani humo, ambapo alisema kilimo cha pamoja kina manufaa makubwa kwa wakulima kwa kuwa wawekezaji wataweza kukununua mazao mengi kwa pamoja, na hivyo kuinua uchumi.

Kairuki alisema, yapo mazao yenye uhitaji mkubwa katika viwanda mbalimbali nchini, akitolea mfano wa  zao la Mtama, ambapo alisema kampuni ya Kilimanjaro Biochem (KBL) iliyopo wilayani Mwanga, ina mahitaji ya zaidi ya Tani 6,000 hivyo ni dhahiri , kuwa soko la uhakika litapatikana, endapo wakulima watalima kilimo cha pamoja na kuzalisha zao hilo kwa wingi.

“Wilaya ya Same ina fursa nyingi za Kilimo, kutokana na ardhi yake kuweza kustawisha mazao ya aina nyingi tofauti na maeneo mengine, kwani yapo maeneo ya umwagiliaji ambapo wanaweza kulima kilimo cha umwagiliaji na maeneo mengine makubwa ya kilimo kingine, hivyo hamasisheni kilimo cha pamoja chenye tija”alisema Kairuki

Mbali na hilo,  Kairuki  alitaka pia Wilaya hiyo,  kujenga makumbusho ya Madini, ambayo watalii pamoja na wananchi watatembelea na kujionea madini mbalimbali ambayo yanapatikana wilayani humo.

“Fursa ya madini ni kubwa katika Wilaya hii, sasa wekeni mkazo kwenye utafiti ikiwezekana iwe kijiji kwa kijiji na kuwepo na maduka ya kuuzia vifaa vya uchimbaji ikiwemo baruti”

Aidha katika kupanua wigo wa uwekezaji, Katika wilaya hiyo,Kairuki alisema ipo haja ya kuangaliwa uwezekano wa kuanzishwa kwa machinjio ya kisasa, katika Wilaya hiyo,akieleza kuwa ipo mifugo mingi na endapo itaanzishwa machinjio, itakuwa fursa nzuri ya uwekezaji katika Halmashauri hiyo.

“Suala la kuanzisha machinjio, liende sambamba na upatikanaji wa mbegu bora za mifugo, pamoja na kutoa elimu kwa wafugaji juu ya umuhimu wa machinjio ili kuwawezesha kuitumia na kuleta tija kwa Wilaya”alisema Kairuki.

Katika hatua nyingine,Kairuki aliutaka pia uongizi wa Wilaya hiyo, kushughulikia migogoro ya Ardhi hususani ile inayohusu wananchi na wawekezaji kwa haraka, ili kuweza kutoa muafaka na kuwezesha uwekezaji kuendelea kwa tija.

“Mwekezaji anapofika mahali akakutana na migogoro, inamchelewesha kuanza kazi zake, lakini pia inakwamisha kasi ya uwekezaji, hivyo hakikisheni mnashughulikia migogoro kwa haraka iwezekanavyo, ili kupanua wigo wa uwekezaji”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule,alisema wakulima kulima zao moja katika eneo moja, itawarahisishia wanunuzi kupata mazao wanayohitaji kwa wingi, na hivyo kuwa na masoko ya uhakika.

“Wakulima wanapolima mmojamoja  au mazao ya aina tofauti katika eneo moja,hayana tija kwao wenyewe na pia kwa serikali, pindi inapotarajia kuuza zao moja kwa Wingi kwa wakati mmoja, lakini inapotokea tukasema kata fulani ni ya zao fulani, wanaweza kukusanya mazao yakauzwa kwa pamoja na kuleta Tija”alisema Senyamule.


Share:

Nafasi za Ajira katika Shirika la Kazi Duniani




Share:

SERIKALI KUJENGA KITUO KIKUBWA CHA UKUZAJI VIUMBE MAJI CHATO


Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Charles Kabeho akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na taasisi ya ujenzi ya Corporation sol uliofika ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuelekea kijiji cha Rubambangwe ambako kitajengwa kituo kikubwa cha kukuzia viumbe Maji.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dokta Rashid Tamatamah (Kulia) akionesha mipaka ya eneo kinapotarajiwa kujengwa kituo cha kukuzia viumbe hai katika kijiji cha Rubambangwe wilayani Chato muda mfupi kabla ya kukabidhi eneo hilo kwa mkandarasi (Corporation Sol) ili aweze kuanza ujenzi wa kituo hicho.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dokta Rashid Tamatamah (kulia) akikabidhi mkataba na michoro ya majengo ya kituo cha kukuzia viumbe maji kwa Meneja wa Kampuni ya Corporation Sol Bw. Simeo Machibya Wilayani Chato (Geita).


Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia sekta ya Uvuvi imeikabidhi kampuni ya ukandarasi ya Serikali ya Corporation Sol eneo naf mkataba wa Ujenzi wa Kituo kikubwa cha Ukuzaji wa Viumbe Maji ili kazi hiyo ianze mara moja.

Makabidhiano hayo yaliyofanyika leo (08.07.2020) katika kijiji cha Rubambangwe kilichopo Wilaya ya Chato mkoani Geita yalifanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dokta Rashid Tamatamah ambaye mbali na kubainisha kuwa mradi huo utakuwa ni mkubwa kuliko yote hapa nchini, pia alielezea maeneo kadhaa yatakayohusiana na mradi huo.

Dokta Tamatamah alisema kuwa mradi huo utajumuisha ujenzi wa mabwawa yatakayokuwa na uwezo wa kutoa zaidi ya tani 10 kwa mwaka, jengo la vitotoleshi vya samaki ambalo litakuwa na uwezo wa kutoa vifaranga zaidi ya milioni mbili kwa mwaka, jengo dogo la kutengeneza chakula cha samaki na eneo la kuhifadhia samaki hao.

Aliongezea kuwa mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.8 mpaka kukamilika kwake na tayari Wizara ilishalipa fidia ya shilingi milioni 42 kwa wakazi waliokuwa wakifanya shughuli zao za kiuchumi katika maeneo hayo yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 28.

“Lakini pia hapa litajengwa darasa, bweni na ukumbi wa chakula kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakuzaji viumbe maji wanaohitaji kujifunza au kuongeza ujuzi wa taaluma hiyo kwa kozi fupi za wiki mbili au tatu” Alisistiza Dokta Tamatamah.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe Maji ambao ndio wasimamizi wakuu wa kituo hicho pindi kitakapoanza kufanya kazi, Bw. Nazaeli Madala alisema kuwa kituof hicho kitakuwa ni ufumbuzi wa changamoto ya uchache wa samaki wanaopatikana kwenye vyanzo vya asili.

“Kituo hiki kitahudumia mikoa yote inayozunguka kanda ya ziwa na maeneo jirani na ukanda huo na tutawafundisha wafugaji wa samaki, maafisa ugani wa fani ya ufugaji wa samaki na pia kitatumika kwa ajili ya mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaosoma katika ngazi mbalimbali huko vyuoni” Aliongeza Madala.

Madala alibainisha kuwa kituo hicho kitawasaidia kupata muongozo wa kujenga vituo vingine katika maeneo yanayozunguka Ziwa Tanganyika, Nyasa na maeneo ya Pwani lengo likiwa ni kuhakikisha viwanda vyote vya samaki vilivyopo nchini havikosi malighafi.

Naye Afisa Mtendaji wa kijiji cha Rubambangwe Bi. Restituta Majura alisema kuwa mradi huo utawanufaisha sana wakazi wa kijiji hicho kwani mbali na kutoa ajira kwa wananchi watakaoshiriki kwenye hatua ya ujenzi, pia wanatarajia kunufaika na uwepo wa barabara itakayoelekea eneo la mradi kwani pia itawasaidia kufika kwenye zahanati ya kijiji inayoendelea kujengwa hivi sasa.

Kabla ya kuelekea kwenye eneo la ujenzi wa kituo hicho, Dokta Tamatamah akiwa na timu yake ya wataalam kutoka Wizarani walifika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Charles Kabeho ambaye aliishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kupeleka mradi huo kwenye Wilaya yake na kuahidi kufuatilia kwa ukaribu hatua zote za ujenzi wa kituo hicho hadi kitakapokamilika mnamo mwezi Oktoba mwaka huu.

Share:

NHIF TANGA YAOKOA MILIONI 76, YATOA ONYO KWA VITUO


 Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga Ally Mwakababu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kulia ni Mkuu wa Idara wa Bima katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Melinas Kidogoma

 Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni Mkuu wa Idara ya Bima Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Melinas Kidogoma

 Mkuu wa Idara ya Bima Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Melinas Kidogoma akizungumza kulia ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu

Mgonjwa ambaye ni mwanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) akipimwa 
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua matukio


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umefanikiwa kuokoa kiasi cha milioni 76 kutoka vituo vya kutolea huduma ambavyo vilionekana kuwa na mapungufu wakati wa kaguzi ambayo ililenga kuviongezea uwezo wa uelewa ikiwemo kuona taratibu wa matibabu zinafuatwa kama zilivyo za wizara 

Hatua hiyo ni kutokana na kufanya kaguzi 125 kwenye vituo vya kutoa huduma ambavyo bado vilionekana kuwa na mapungufu huku wakitoa onyo kwao iwapo wataendelea na vitendo vya namna hiyo watachukuliwa hatua kali. 

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga Ally Mwakababu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari ambapo alisema kaguzi hizo walizifanya ikiwa ni kuona kama vituo hivyo zinafuatwa taratibu za wizara. 

Alisema kwamba kufuatia uwepo wa mapungufu hayo mfuko huo umetoa onyo kali na iwapo vituo hivyo vitarudia makosa hayo watavipeleka vyombo vya sheria au kuvifungia. 

“Lakini niwaambie kwamba nia yetu sio kuvikomoa vituo ila kuhakikisha huduma za msingi stahili stahiki zinatolewa kwa wananchi kwa sababu nhif imetoa ahadi kwa kwao ukiwa ndani ya mfuko unapata kila kitu hivyo anapokosa kwa sababu yako Lazima uwajibishwe”Alisema Meneja Mwakababu. 

Awali akizungumza katika mkutano huo, Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza alisema kwamba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo inakaribia kusajili duka dawa la ndani na ipo kwenye hatua za mwisho na hiyo itapunguza usumbufu kwa wanachama ambao lazima walikuwa watoke nje ya geti kuchukua vifaa na kurudi ndani kupata huduma.



Alisema kwamba hospitali wameanzisha mradi huo wanatarajia kuwa duka hilo litasaidia kuondoa usumbufu ambao walikuwa wakikumbana nao wanachama wao. 

Hata hivyo alisema suala la udanganyifu kwenye uwasilishwaji wa madai fedha zinazolipwa kwa kufauta miongozo na taraibu ambazo zimewekwa huku akieleza kwamba watoa huduma wa namna hiyo hawawezi kuwavumiliwa na watachukuliwa hatua. 

“Kwa kweli tunapobaini madai yana udanganifu hatuchelewi kuchukua hatua kwa watoa huduma na wanajua tunavamia vituo tujiridhishe anachodaia ni kweli”Alisema 

Daktari huyo alisema kwani wakiwapa nafasi watoa huduma ambao sio waaminifu wanachukua nafasi ya kujiongezea vitu ambyao wanachama wao hawajapata kwenye vituo vyao.

Share:

Majengo Ya Hospitali Ya Manispaa Yakamilike Katika Kipindi Husika- RC Tabora

NA TIGANYA VINCENT
UONGOZI wa Manispaa ya Tabora umetakiwa kuhakikisha Wakandarasi wanaojenga majengo ya  Hospitali ya Wilaya na yale ya Kituo cha Afya Tumbi wanakamilisha kwa ubora unatakiwa na ya  muda waliopewa katika mkataba ili wananchi waweze kupata huduma kwa karibu.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kukagua miradi ya maendeleo.

Alisema kiasi cha shilingi milioni 700 zilizotolewa na Serikali ni lazima zionekane katika miundo mbinu itakayojengwa na iwe msaada kwa wananchi kupata huduma bora kwa gharama nafuu.

Dkt. Sengati alisema hatasita kuwachukulia hatua watendaji wote watakaobainika kutumia fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo wananchi wayonge kwa maslahi binafsi.

Aliwataka watendaji wanaopewa majukumu ya kusimamia miradi kuwa wazalendo na waaminifu ili siku moja nao wawe sehemu ya mafanikio hayo.

Naye Katibu wa Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Tabora Joseph Kashushula alisema Mwezi Mei mwaka huu walipokea shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa majengo matatu ambapo yote yameanza.

Alisema majengo hayo ni Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD), Maabara na kichoma taka  na yote yanatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu kama ilivyo kwenye mkataba.

Kashushula alisema kiasi hicho ni sehemu ya fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo ndani ya mwaka wa fedha huu wanatarajia kupata kiasi cha shilingi bilioni 1 ili kukamilisha majengo ambayo yatakuwa yamebaki.

Kwa upande wa Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Tumbi Charles Ngussa alisema walipokea kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo wa Nje (OPD) na vyoo.

Alisema hadi hivi sasa wameshatumia shilingi milioni 113.1 na zimebaki shilingi milioni 86.8.

Ngussa alisema kati ya fedha zilizotumika wameweza kununua vifaa vyote vinatakiwa ikiwemo bati na rangi.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora mara baada ya kuwasili ofisini kwake jana alianza kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa dhana ya hapa kazi.

mwisho


Share:

TGNP YASHTUSHWA MATUKIO YA VIPIGO NA MAUAJI YA WANAWAKE NA WATOTO

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), tunasikitishwa na kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

 Hivi karibuni, kumekuwa kukiripotiwa kupitia mitandao ya kijamii juu ya matukio kadhaa yanayohusisha vipigo na mauaji ya wanawake na ukatili dhidi ya watoto ndani ya familia na jamii kwa ujumla.

 Uwepo wa vitendo hivyo ni ukiukwaji wa haki za wanawake na watoto kama inavyoainishwa katika Ibara ya 12 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) inayotaka haki ya kuheshimu na kuthamini Utu wa Mtu. 

Licha ya kuwa vitendo hivi ni aibu kwa Taifa kwa ujumla, lakini pia vinakosesha Amani na kusababisha madhara kimwili, kisaikolojia na kiuchumi kwa wahusika na jamii.

TGNP tunakemea vitendo hivyo na kutoa rai kwa mamlaka husika za serikali hususan jeshi la polisi kufuatilia na kuchukua hatua stahiki kisheria. 

Vile vile, tunawataka viongozi wa dini kusimama katika nafasi zao na kukemea vitendo hivi; Jamii kutokaa kimya pale ambapo matukio kama haya yanapojitokeza kwa kutoa taarifa kwa mamlaka na vyombo husika.

 Pia, tunawataka watu binafsi kujitokeza na kupaza sauti pale wanapoona viashiria au vitendo ya ukatili vikifanyika ndani ya familia na jamii kwa ujumla.

TGNP itaendelea kufuatilia na kupaza sauti dhidi ya matendo haya ya kikatili yanayodhalilisha, na kuondoa Utu na Heshima kwa wanawake na watoto.

TGNP
Share:

BALOZI MONGELLA: ZAMA ZA ADUI WA MWANAMKE NI MWANAMKE MWENZAKE ZIMEPITWA NA WAKATI


Wanawake nchini wametakiwa kuondoa dhana potofu iliyojengeka katika jamii ya kuamini kuwa mwanamke hawezi kusonga mbele bila kumkwamisha mwanamke mwenzake.

Rai hiyo imetolewa na Balozi Gertrude Mongella wakati akizungumza na wanawake kutoka viunga mbalimbali vya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza ambapo amewataka kupendana, kusaidiana na kuungana pamoja ili kufikia malengo ya kuwa na nafasi sawa katika vyombo vya maamuzi ili waweze kujikomboa katika ukandamizaji wa kijinsia na kujiletea maendeleo.

"Mwanamke unapoona mwanamke wenzako amesimama mlangoni anataka kuingia ndani, Usimvute nje, Unachotakiwa kufanya ni kumsukuma ndani ili wote muingie, Ukimvuta nje wote mtadondoka wa nyuma yenu watawakanyaga", alisema.

Aidha Balozi Mongella amewapongeza wanawake viongozi wanaoshika nafasi mbalimbali nchini akiwemo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe Ummy Mwalimu kwa kusimama kidete katika vita dhidi ya janga la Covid-19 na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kusimamia vizuri sekta ya Ardhi nchini.

Akimkaribisha mgeni rasmi wa kongamano hilo, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amewaasa wanawake walioshiriki kuhakikisha wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kushiriki katika zoezi la kupiga kura ili kufikia lengo la kuwa na usawa katika maamuzi maarufu kama hamsini kwa hamsini pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli kwa kujadili wanawake na kuwaamini kwa Kuwateua katika nafasi mbalimbali za uongozi sanjari na kutatua changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wake Mjumbe wa baraza la wadhamini wa CCM na Mwenyekiti mstaafu wa Umoja wa wanawake wa CCM Mhe Anna Abdallah mbali na kuelezea historia ya viongozi wanawake waliowahi kuwepo nchini, amewataka wanawake wanaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuzingatia maadili, kuwa waadilifu na kuzitendea haki nafasi wanazowania ili kuleta taswira chanya kwa jamii juu ya kuondoa dhana mbovu ya kutoamini wanawake kwa kuwaona hawawezi kufanya lolote bila ya uwepo wa mwanaume.

Akihitimisha Mkurugenzi wa shirika lisilo la KiSerikali la Kivulini lililopo jijini Mwanza Ndugu Yassin Ally amesema kuwa kongamano la kujadili nafasi ya mwanamke katika uongozi wa kisasa nchini limeandaliwa na wanawake wa wilaya ya Ilemela kwa kushirikiana na taasisi ya Kivulini likiwa na lengo la kuhamasisha mshikamano wa kuunga mkono wanawake wanaogombea, kuweka mikakati ya kuongeza nafasi za wanawake wagombea kuelekea uchaguzi mkuu na kushirikishana fursa na changamoto za uongozi wa kisasa nchini huku likipambwa na Kauli Mbiu ya MSHIKAMANO WETU, USHINDI WETU, CHUKUA HATUA

Kongamano hilo pia lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wanawake kutoka maeneo tofauti ya mkoa wa Mwanza akiwemo akiwemo mwenyekiti wa UWT mkoani humo Mhe Hellen Bogohe na mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ilemela Mhe Salome Kipondya na mada mbalimbali zikiwasilishwa na mchambuzi wa masuala ya kijinsia Dr Geoffrey Chambua.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JULAI 9,2020





















 

Share:

Wednesday 8 July 2020

ARTISAN GRADE II (FITTER MECHANICS) – 3 POST at  SHIRIKA LA MZINGA

ARTISAN GRADE II (FITTER MECHANICS) – 3 POST at  SHIRIKA LA MZINGA POST DETAILS POST ARTISAN GRADE II (FITTER MECHANICS) – 3 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER SHIRIKA LA MZINGA APPLICATION TIMELINE: 2020-07-08 2020-07-21 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES   i.  To undertake repair works or fabricate equipment, plants and parts scheduled […]

The post ARTISAN GRADE II (FITTER MECHANICS) – 3 POST at  SHIRIKA LA MZINGA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

SUPPLIES ASSISTANT – 1 POST at SHIRIKA LA MZINGA

SUPPLIES ASSISTANT – 1 POST at SHIRIKA LA MZINGA POST DETAILS POST SUPPLIES ASSISTANT – 1 POST POST CATEGORY(S) PROCUREMENT & LOGISTIC MANAGEMENT EMPLOYER SHIRIKA LA MZINGA APPLICATION TIMELINE: 2020-07-08 2020-07-21 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.  To Maintain stock records; ii.  To Assist in establishing  claims for lost or shorthanded goods with relevant […]

The post SUPPLIES ASSISTANT – 1 POST at SHIRIKA LA MZINGA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

TECHNICIAN GRADE II – 1 POST at SHIRIKA LA MZINGA

TECHNICIAN GRADE II – 1 POST at SHIRIKA LA MZINGA POST DETAILS POST TECHNICIAN GRADE II – 1 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER SHIRIKA LA MZINGA APPLICATION TIMELINE: 2020-07-08 2020-07-21 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES     i.  To operate, maintain  and assist to repair  production machines; ii.  To assist to design […]

The post TECHNICIAN GRADE II – 1 POST at SHIRIKA LA MZINGA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wizara Ya Mifugo Na Uvuvi Yadhamiria Kufikia Malengo Ya Kisekta Katika Uchumi Wa Kati.

Na. Edward Kondela
Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendeleza jitihada za kuhakikisha inafikia malengo ya kisekta baada ya Tanzania kuorodhesha na Benki ya Dunia hivi karibuni kuwa moja ya nchi zilizoingia katika uchumi wakati ulioainishwa katika dira ya taifa ya mwaka 2020-2025.

Akizungumza leo (08.07.2020) wakati wa mafunzo rejea yanayotolewa na Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) iliyo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa wafugaji katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde, ameipongeza LITA kwa kutoa mafunzo hayo yenye lengo la kuifanya wilaya hiyo kuwa na shughuli nyingi za kiuchumi ukiwemo ufugaji wa kuku kibiashara.

“Sisi siyo wafugaji, sasa katika kupanua wigo wa shughuli za kiuchumi mwisho wa siku tunakuwa na shughuli nyingi za kiuchumi kikiwemo kilimo na uvuvi ambavyo tumeshavizoea sasa tunataka kwenda kwenye ufugaji, ufugaji wa wanyama na ndege wafugwao kwa maana ya kuku, wengi wenu mnafuga kuku wa kienyeji ambao siyo wa kibiashara tunapoongelea uchumi tunataka chakula lakini pia kupata kipato kwa ajili ya matumizi mengine.”  Amesema Mhandisi Munde

Mhandisi Munde amefafanua kuwa kupitia mafunzo hayo wanafunzi pia watajifunza kwa vitendo ufugaji wa kuku na hatimaye kufundisha jamii inayowazunguka, kutokana na mafunzo hayo kujumuisha walimu kutoka shule tano za msingi zilizopo Wilayani Mkuranga ambazo pia zitapatiwa vifaranga vya kuku aina ya kroiler vikiwa na umri wa wiki tatu.

Aidha ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia kwa naibu waziri wa wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega kwa kuhamasisha ufugaji wa kuku kibiashara katika maeneo mbalimbali nchini ili wananchi wajikwamue kiuchumi ikiwemo Wilaya ya Mkuranga, ambapo Oktoba 4, Mwaka 2019 Mhe. Ulega aliahidi kutoa vifaranga vya kuku aina ya kroiler kwa vikundi 25 vya wilaya hiyo vilivyohudhuria mafunzo kipindi hicho.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Angello Mwilawa akizungumza kwenye mafunzo rejea kwa wafugaji Wilayani Mkuranga, amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikifanya mapinduzi makubwa katika sekta za mifugo na uvuvi kwa kuhamaisha ufugaji endelevu na ufugaji bora kote nchini.

Dkt. Mwilawa amesema wizara imekuwa ikifanya mkakati wa kuboresha uzalishaji na biashara ya ndege wafugwao wakiwemo kuku, kwa kuwa kaya nyingi nchini zimekuwa zikitegemea ufugaji wa kuku ambao umekuwa na faida kwa pato la taifa kwa jumla na ngazi ya kaya kwa kuboresha lishe na hivyo wizara kuhimiza ufugaji wa kuku kwa kuwa mtaji wake ni mdogo.

 “Sisi kama wizara tunahimiza wafugaji wetu wajikite katika ufugaji wa kuku kwa kuwa wanahitaji mtaji mdogo, lakini kadri wanavyojipanua hao kuku wanaweza kumuongezea mtaji kuwa mkubwa zaidi hasa kwa kumuongezea kipato na kuleta faida katika ngazi ya kaya na ukubwa wake katika ngazi ya taifa, sisi kama wizara kuku ana mchango mkubwa katika ngazi ya taifa na kaya endapo shughuli ya ufugaji ikifanyika katika ubora.”

Naye Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utafiti kutoka Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) Bw. Silaju Kapembe akitoa mafunzo kwa wafugaji hao amewataka kabla ya kuanza kufuga kuku ni muhimu kuandaa mazingira bora ili kuhakikisha vifaranga vinamudu mazingira ya awali huku mmoja wa wafugaji hao Bw. Nyanza Mwinshehe akiishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuandaa mafunzo ya ufugaji bora wa kuku na kuiomba wizara hiyo kuweka mkazo zaidi wa shughuli za ufugaji katika Wilaya ya Mkuranga ili kuongeza wigo wa vyanzo vya kiuchumi.

LITA imekuwa na malengo makuu ya kutoa mafunzo kwa wafugaji wakiwemo wa kuku katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani ili kuondokana na ufugaji wa mazoea na kwenda kwenye ufugaji wenye tija na endelevu

Pia kuyaongezea thamani mazao yanayotokana na mifugo ili kuwa na kipato kikubwa zaidi pamoja na kuongeza lishe katika familia.

Wafugaji hao ambao wanapatiwa mafunzo na LITA ambayo iko chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanatokana na ahadi waliyopatiwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega Oktoba 4, Mwaka 2019 wakati wa mafunzo rejea Wilayani Mkuranga ambapo wanatarajia kesho (09.07.2020) kukabidhiwa vifaranga vya kuku aina ya kroiler vyenye umri wa wiki tatu kupitia katika vikundi 25.

Mwisho.


Share:

Mfumuko wa Bei Mwezi Juni Waendelea kuwa Asilimia 3.2

Na   Mwandishi Wetu- MAELEZO
Mfumuko wa bei wa Taifa kwa  mwezi Juni 2020 umeendelea kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa mwezi  Mei, 2020. 
 
Akizungumza leo Julai 8, 2020 Jijini Dodoma,  Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bi. Ruth Minja amesema kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka unaoishia mwezi Juni umebaki kuwa sawa na iliyokuwepo kwa mwezi Mei. 
 
Akifafanua, Bi Minja amesema kuwa baadhi ya bidhaa za vyakula zilipungua bei kwa mwezi Juni 2020 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2019, baadhi ya bidhaa hizo ni pamoja unga wa mahindi kwa asilimia 1.6, matunda kwa asilimia 2.1, viazi mviringo asilimia 0.5 na mihogo asilimia 13.3. 
 
Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula amesema kuwa ziliongezeka bei kwa mwezi Juni, 2020 ikilinganishwa na bei za mwezi Juni 2019, bidhaa hizo ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.7, gesi ya kupikia kwa asilimia 7.8 , mkaa asilimia 11.2, samani asilimia 2.7 na vitabu vya shule kwa asilimia 1.5. 
 
Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2020 umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka unaoishia mwezi Mei, 2020. 
 
Kwa upande wa nchi ya Kenya Bi Minja amesema kuwa Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2020 umepungua hadi kufikia asilimia 4.59 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2020. Kwa upande wa Uganda, Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 2.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2020. 
 
…Mwisho…


Share:

DAWA ZA CORONA ZAUZWA KWA MAGENDO KWA BEI YA JUU


Uchunguzi wa BBC umebaini kuwa aina mbili za dawa ambazo zilitumika kutibu wagonjwa wa corona nchini India - remdesivir na tocilizumab - zimekuwa zikiuzwa katika soko la magendo kwa bei ya juu ndiyo maana kuna upungufu mkubwa sana wa dawa hizo.

Mwandishi wa BBC, Pandey anaripoti kutoka mji mkuu wa India Delhi.
Mjomba wake Abhinav Sharma alikuwa na homa kali na alikuwa anapata tabu kupumua wakati alipolazwa hospitalini huko Delhi.

Alikutwa na virusi vya corona na madaktari waliiambia familia yake itafute dawa aina ya remdesivir - dawa ambayo imeruhusiwa kwa ajili ya matibabu ya corona wakati wa dharura nchini India ",hii ikiwa ina maana kuwa madaktari wanaweza kutoa ruhusa ya matumizi ya dawa hizo kwa kutokana na sababu maalum.

Lakini upatikanaji wa dawa hiyo umeonekana kuwa jambo ambalo haliwezekani - dawa ya 'remdesivir' imeadimika na haipatikani kokote.

Bwana Sharma alihangaika kuwapigia watu kumsaidia kupata dawa ya kumsaidia mjomba wake ambaye hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya kila saa.

"Nilikuwa na machozi machoni mwangu. Mjomba wangu alikuwa anapambana na maisha yake na nilikuwa nahangaika kupata dawa ambayo ingeweza kuokoa maisha yake," alisema.

"Baada ya kupiga simu kadhaa, nililipa mara saba ya gharama halisi ya dawa nilikuwa radhi kulipia gharama yoyote ile kwa kweli, lakini nawaonea huruma watu wale ambao hawana uwezo wa kununua kwa gharama hiyo," alisema.

Changamoto aliyokabiliana nayo Bwana Sharma, inazikabili familia nyingi sana mjini Delhi, ambapo watu wengi huwa wanahangaika na kufanya lolote ili kuokoa maisha ya wapendwa wao.

Baadhi wanasema huwa wanalazimika kulipa gharama kubwa sana kwa ajili ya dawa hiyo - wengi huwa wanaishia kwenye soko la zamani la dawa la mjini Delhi.

Via BBC SWAHILI
Share:

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MWAKA 2020 KUFANYIKA VIWANJA VYA NYAKABINDI MKOANI SIMIYU


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Serikali imetangaza kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kutafanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima NANENANE ambapo kitaifa yatafanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.

Akizunguzma na waandishi wa habari akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa Maonesho hayo yataambatana na uhamasishaji wa matumizi ya teknolojia bora za kilimo, ufugaji na uvuvi. Pia, maonesho hayo yatashirikisha Wadau mbalimbali zikiwemo Wizara, Taasisi za Umma na Binafsi, Wabia wa maendeleo, wakulima na Vyama vya wakulima, wafugaji na wavuvi.

Waziri Hasunga amesema kuwa Maonesho hayo ya Ishirini na Nane (28) tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 yatafanyika kwenye Kanda nane (8) za Maonesho ambazo ni Kanda ya Mashariki (Morogoro), Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Magharibi (Tabora), Kanda ya Kusini (Lindi), Kanda ya Kati (Dodoma), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Kanda ya Ziwa Mashariki (Simiyu) na Kanda ya Ziwa Magharibi (Mwanza).

Mhe Hasunga amesema kuwa Kupitia Maonesho hayo, Viongozi mbalimbali wa Kitaifa watatembelea viwanja vya Maonesho na kuhamasisha masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta za kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na Ushirika.

Amewataja baadhi ya Viongozi wanaotarajiwa kushiriki katika Maonesho hayo ngazi ya Taifa ni Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kadhalika amelitaja Lengo la Maonesho ya Nanenane katika kanda hizo kuwa ni pamoja na kutoa fursa kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wanaushirika kuona na kujifunza matumizi ya teknolojia bora za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa ajili ya kuongeza tija na uzalishaji kwa uhakika wa chakula, kukidhi mahitaji ya viwanda na masoko ya ndani na nje ya nchi.

Kaulimbiu ya Maonesho hayo kwa Mwaka 2020 ymaepambwa na kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020“.

Waziri Hasunga amebainisha kuwa Mwaka 2020 ni Mwaka wa Uchaguzi Mkuu, Kaulimbiu hiyo inatoa hamasa kwa wananchi kuchagua viongozi bora watakaokuwa chachu ya kuleta mapinduzi kwa ajili ya maendeleo ya sekta za kilimo ili kuinua ustawi wa maisha ya wakulima, wafugaji na wavuvi.

Aidha, Mhe Hasunga ametoa mwito kwa wadau wote wa sekta ya umma na binafsi kukamilisha maandalizi ya kushiriki katika viwanja vyote vya maonesho vilivyopo kwenye Kanda Nane (8) kama nilivyoeleza hapo juu. Aidha, Kamati za Maandalizi ya Nanenane ngazi ya Kanda zinazoongozwa na Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa zihakikishe zinakamilisha maandalizi yote muhimu na kuwashirikisha wadau wote.

Katika kuhakikisha Maonesho ya Kilimo yanakuwa na tija, Wizara ya Kilimo iliandaa na kusambaza katika mikoa yote Mwongozo wa Maonesho na Mashindano ya Kilimo, Mifugo Na Uvuvi. Mwongozo huo, pamoja na mambo mengine unaeleza Utaratibu wa Kusimamia na Kuratibu Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ikiwemo majukumu ya kila mdau; Matumizi Endelevu ya Viwanja Vya Maonesho; Mapato na Matumizi kwa ajili ya Maonesho; na Ufuatiliaji na Tathmini. Hivyo, nisisitize Uongozi wa Mikoa katika Kanda zote uhakikishe kuwa Maonesho ya Nanenane yanafanyika kwa kuzingatia Mwongozo huo.

Kadhalika, amesema kuwa ni lazima mikoa ihakikishe viwanja vya Maonesho vinatumika muda wote kabla, wakati na baada ya maonesho kama mashamba darasa na vitovu vya kutoa elimu ya matumizi bora ya teknolojia bora za uzalishaji na masoko.

MWISHO


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger