Wednesday 29 April 2020

DAKTARI WA WAGONJWA WA CORONA AJIUA


Dr. Lorna M. Breen ambaye aliamua kujiua, picha kubwa ni hospitali aliyokuwa anafanya kazi.

VIRGINIA, Daktari Mkuu katika chumba cha dharura katika Hospitali ya Manhattan nchini Marekani ambaye aliwatibu wagonjwa wengi wa virusi vya corona (COVID-19), Dkt.Lorna M. Breen amejiua kwa kujinyonga.

Kwa mujibu wa The New York Times, baba yake mzazi na Jeshi la Polisi mjini Charlottesville, Virginia wamethibithisha kifo hicho.

Dkt.Breen ambaye pia alikuwa ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Dharura katika Hospitali ya NewYork-Presbyterian Allen alijinyongea mjini Charlottesville, Virginia ambapo alikuwa anaishi na wazazi wake.

Msemaji wa Jeshi la Polisi mjini Charlottesville,Tyler Hawn ameeleza kupitia barua pepe kuwa, maafisa wa jeshi hilo siku ya Jumapili iliyopita walipokea simu ya dharura ikihitaji msaada wa kitabibu.

“Mgonjwa (Dkt.Lorna) alichukuliwa na kupelekwa Hospitali UVA kwa matibabu, lakini baadae aliamua kujijeruhi mwenyewe,”amesema Hawn.

Baba yake Dkt.Lorna Breen, Dkt.Philip C. Breen amesema, baada ya binti yake kubaini hali yake si njema aliamua kufanya uamuzi ambao si wa busara.

“Alijaribu kufanya kazi yake kwa kadri ya uwezo wake na ikamuua,”amesema Baba mzazi wa marehemu huyo.

Dkt.Philip Breen amesema, binti yake awali alikuwa ameambukizwa virusi vya corona, lakini alikuwa amerejea kazini baada ya kupona wiki moja na nusu iliyopita.
Share:

AKAMATWA KWA KUSAMBAZA UONGO MTANDAONI KUWA DAWA YA COVID 19 NI KUNYWA NA KUJIPAKA PILIPILI NA UPUPU

Na Amon Mtega - Songea 
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)Ibrahimu Bukuku (26)kwa tuhuma za kusambaza ujumbe unaodaiwa kuwa ni wa upotoshwaji kwenye mitandao ya kijamii uliohusu dawa ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona.
 

Akizungumza ofisini kwake jana Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Simon Maigwa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika kijiji anachoishi cha Lunyele (Darpori) kata ya Tingi Wilaya ya Nyasa mkoani humo.

 Kamanda Maigwa amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Chuo Kikuu cha Dodoma anayesomea shahada ya Sayansi fani ya Biolojia (Bachelor of Science in Biology) amesambaza ujumbe kupitia simu yake ya kiganjani usemao 'Dawa ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona ni kutumia upupu pamoja na pilipili.

Maigwa amefafanua kuwa ujumbe huo ambao umesambazwa kwenye makundi mbalimbali ya kijamii ya Whatsap kuwa "Dawa ya Covid 19 ni kuchukua pilipili kichaa sufuria moja iliyotwangwa halafu changanya na maji vikombe vitano kisha kunywa kutwa mara saba kwa muda wa siku tatu na siku ya nne chuma upupu na kujipaka mwili mzima" jambo ambalo linadaiwa kuwa upotoshwaji mbele za jamii na linachukuliwa mchezo kwenye gonjwa hili la Covid 19.

 Amesema kuwa jeshi la Polisi litaendelea kuwatafuta wale wote wanaofanya mchezo na ugonjwa huu wa Covid 19 unaosababishwa na Virusi vya Corona na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kujibu mashistaka yanayowakabili.
Share:

TULONGE AFYA YAZINDUA KIPINDI CHA 'WASHA KIDEO NA SITEREREKI' LIVE MTANDAONI KUELIMISHA VIJANA MASUALA YA AFYA 'COVID- 19'

Ili kukabiliana na changamoto za COVID-19 ambazo zimeathiri shughuli mbali mbali Nchini Tanzania, Programu ya USAID Tulonge Afya imezindua kipindi maalum cha TV cha moja kwa moja (yaani live) "Washa Kideo na Sitetereki" kipindi ambacho pia kitakuwa kikirushwa moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii. 


Malengo ya kipindi hiki cha Washa Kideo na SITETEREKI ni kushughulikia changamoto za kiafya zinazohusiana na vijana na jinsi wanavyoweza kukabiliana nazo katika kipindi hiki cha janga la COVID-19 ambapo mifumo yote ya kila siku imevurugika kwani watu wote wanahimizwa kukaa nyumbani.

Programu ya SITETEREKI ni jukwaa la kubadilisha tabia na mienendo ya kila siku (SBC) linalolenga vijana. Jukwaa hili linasaidia kukuza Muingiliano wa vijana nchini Tanzania ili kujua vyema, kuhamasisha, na kuwezesha vijana kuchukua tabia njema ambazo zitaboresha ustawi wao kwa jumla. SITETEREKI imeundwa kusaidia moja kwa moja vipaumbele vya kimkakati kwa vijana katika Serikali ya Tanzania na inafadhiliwa na serikali ya Marekani kupitia USAID.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Mkurugenzi wa USAID nchini Tanzania Andy Karas alisema kuwa kipindi cha Washa Kideo na SITETEREKI kimebuniwa kusaidia vipaumbele vyaSerikali ya Tanzania kwa Vijana.. 'Sote tunaelewa kuwa sasa vijana wetu hawawezi kwenda tena kwenye mikusanyiko ya kijamii, Luninga pamoja na mitandao ya kijamii sasa imekuwa ndio kimbilio la vijana wengi.

 Kwa sababu ya idadi kubwa ya watu wanaokaa nyumbani kwa sasa, utumiaji wa vyombo vya habari na hasa Luninga pia umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Vijana wetu wamekuwa wakivutiwa na mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na YouTube, Instagram, pamoja na vyombo vingine vya habari vinapokuwa vikirusha taarifa zao moja kwa moja. 

Kwa sababu hiyo, tumezindua kipindi "Washa Kideo na SITETEREKI" ili kutoa fursa ya kipekee ya kufikia mamilioni ya vijana wa kitanzania kwa njia ambayo huwashawishi wakati wa kutoa ujumbe muhimu wa afya ili kuwasaidia kuwalinda wao na familia zao, na nchi kwa ujumla kwa wakati wote na janga la COVID-19. "Karas alisema.

Aliongeza, ‘COVID-19 inajaribu kutikisa mienendo yetu ya maisha lakini kupitia muendelezo wa ufadhili wa serikali ya Marekani na uwekezaji wake katika afya ya Watanzania na taasisi za afya, na kuwa na mienendo mizuri ya kiafya ambayo tunashirikiana pamoja leo hii, vijana wa Kitanzania “hawata - tetereka”. 

Serikali ya Marekani inaendelea kusaidia kupambana na mlipuko wa COVID-19 kwa kuchukua hatua za haraka kupitia taasisi zake mbalimbali hapa nchini. Serikali ya Marekani inashirikiana na wafanyakazi wa Tanzania walio mstari wa mbele katika kupunguza maambukizi, kutoa huduma kwa waathirika, na kuandaa jamii kwa kutoa vifaa muhimu vinavyohitajika kupambana na COVID-19.

Akizungumza kuhusu kipindi cha Washa Kideo na SITETEREKI, Mkurugenzi wa Miradi Tulonge Afya Waziri Nyoni alisema kuwa Kipindi hicho Kina lenga kufikia vijana zaidi ya milioni 20 wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 25 hapa nchini.

Tamasha hilo litaunga mkono juhudi za kupambana na janga hatari la COVID-19, na VVU, afya ya uzazi na malengo ya mkakati wa uzazi pamoja na kukuza tabia chanya kwa vijana.

‘Tamasha la Washa Kideo na SITETEREKI litakuwa likirushwa kila Ijumaa kwa masaa mawili kuanzia saa tatu mpaka saa tano usiku huku wasanii wakitumbuiza moja kwa moja kupitia Clouds TV na Clouds Radio. Vile vile, litakuwa likirusha moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii ya Clouds Media. Wasanii, ma DJ pamoja na waendesha kipindi hicho pia watakuwa wakirusha moja kwa moja kwenye mitandao yao ya kijamii na hivyo kuweza kuwafikia zaidi ya wafuasi wao milioni 22.4 kwenye mtandao wa Instagram. Watazamaji wataweza kuwasiliana moja kwa moja na wasanii’ Nyoni alisema.

Tamasha la kipindi cha Washa Kideo na SITETEREKI litawaleta pamoja wasanii mbali mbali ikiwa ni pamoja na Maua Sama, jux na G-Nako, pia watakaoshiriki kwa njia ya mtandao watakuwa Harmonize, Nandy, Dogo Janja na Nikki wa Pili. Aliongeza kuwa watangazaji wa programu hiyo watakuwa Nickson George na Mina Ally wakati DJ’s watakuwa DJ D-Omy na DJ Sinyorita.

Mradi wa Tulonge Afya, ni mradi wa miaka 5 unaofadhiliwa na shirika la Marekani la USAID, miradi ya Tulonge afya ina lengo la kukuza shughuli chanya za afya katika kaya na jamii nchini Tanzania huku ikilenga wanawake na vijana. Mradi wa Tulonge Afya unatekelezwa na FHI 360 Wizara ya Afya , Maendeleo ya Kijamii, Wazee na Watoto pamoja na washirika wengine.
Share:

DOWNLOAD - PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ...TUKUTUMIE HABARI ZOTE BURE KWENYE SIMU YAKO

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.


Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

Serikali Itaendelea Kuwakinga Watumishi Wa Afya Ili Wasipate Maambukizi Ya Ugonjwa Wa Covid – 19

Na WAMJW – Dar es Salaam
Serikali itaendelea kuwalinda watumishi wa afya ili wasipate maambukizi wakati wakiwahudumia wagonjwa wenye Virusi vya Corona (COVID-19) kwa kuwapa vifaa kinga na mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa hao.

Hayo yamesemwa jana  jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJW) Ummy Mwalimu wakati wa kikao baina yake na wamiliki wa Hospitali binafsi na viongozi wa vyama vya kitaaluma vya afya.

Waziri Ummy alisema ni jukumu la Serikali kuhakikisha linawalinda watoa huduma za afya kwa kuwapa vifaa kinga ili wawahudumie wagonjwa waliopata  maambukizi ya ugonjwa wa COVID -19.

“Ninaomba mzifikishe shukrani zangu za dhati kwa wahudumu wa afya  ambao wako mstari wa mbele katika kuwahudumia  wagonjwa waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Corona ambao ni janga la kimataifa’’,alisema Waziri Ummy.

Waziri huyo pia aliwashukuru viongozi hao  kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kuhakikisha Hospitali zao zinatoa huduma kwa wagonjwa.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi alisema nguvu za pamoja zinahitajika ili wagonjwa wenye maambukizi ya ugonjwa wa Corona na wale ambao hawajapata maambuzi waweze kupata huduma za matibabu kwa wakati.

Prof. Makubi alisema jambo la muhimu kwa  watoa huduma za afya ni kujilinda wakati wanahudumia wagonjwa pia wamiliki wa Hospitali watoe elimu ya jinsi ya kujikinga na maambukizi ya COVID -19 kwa wafanyakazi wao.

 Naye Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dkt. Elisha Osati aliipongeza Serikali kwa hatua iliyochukuwa ya kupambana na ugonjwa wa Corona nchini.

“Mkutano huu ni wa muhimu kwetu kwani tumekaa kwa pamoja na kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19, ninaamini baada ya mkutano huu kila mmoja wetu ataenda kuyafanyia kazi”, alisema Dkt. Osati


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano April 29



















Share:

Tuesday 28 April 2020

KARIBU EKIE SHINYANGA CAR WASH CENTRE



Share:

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA 'POPOTE INATIKI' KUHAMASISHA WATEJA KUTUMIA MIFUMO YA KIDIJITALI

 Meneja Mwandamizi wa Masoko Benki ya CRDB, Joe Bendera (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Msanii Harmonize (katikati) wakati wa uzinduzi na kampeni ya “POPOTE INATIKI” inayolenga kuwahamasisha wateja kutumia mifumo ya kidijitali kufanya miamala yao ya kifedha. Uzinduzi huo ulienda sambamba na kumtambulisha msanii Harmonize kama balozi mpya wa Benki ya CRDB. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Benki ya CRDB na uongozi wa msanii Harmonize.
Benki ya CRDB imezindua kampeni maalumu ya mifumo ya kidijitali kwa wateja wake ijulikanayo kama ‘POPOTE INATIKI’, inayolenga katika kuwaelimisha wateja na watanzania kwa ujumla juu ya matumizi ya mifumo hiyo katika upatikanaji wa huduma za benki popote pale walipo masaa 24.

Akizungumza juu ya kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa alhamisi iliyopita huku ikienda sambamba na kumtambulisha msanii ‘Harmonize’ kama balozi wa Benki ya CRDB, Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts amesema hadi kufikia mwezi machi mwaka huu 2020 zaidi ya asilimia 80 ya miamala inayofanywa na wateja wa benki hiyo inafanywa kwa njia za kidijitali kupitia mifumo ya SimBanking, SimAccount, Internet BankingCRDB Wakala na TemboCard kupitia vifaaa vya manunuzi (PoS) na mtandaoni (e-commerce). 
“Mwaka jana 2019, tumefanikiwa kuboresha mifumo hii yote ya utoaji huduma kidijitali kwa kiasi kikubwa sana hii ikiwa ni pamoja na kuongeza baadhi ya huduma katika mifumo hii, hivyo basi tumeona ni vyema tukajikita pia katika kutoa elimu kwa wateja,” alisema Dkt. Witts.
Dkt. Witts alisema Benki ya CRDB kupitia mkakati wake wa biashara wa 2018-2022 umejikita zaidi katika kuleta mabadiliko ya kidijitali ilikuendana na mahitaji ya wateja ambayo yamekuwa yakibadilika kila uchwao. 

“Kupitia mifumo hii ya kidijitali hamlazimu mteja kufika katika tawi ili kupata huduma, popote pale Ulipo, uwe mjini, kijijini, nyumbani au mtaani, ndani ya nchi au nje ya nchi, muda wa kazi au muda ambao sio wa kazi, masaa 24 tunakuwezesha kufanya miamala yako ya kwa uharaka, unafuu na usalama, na ndio maana tunasema ‘POPOTE INATIKI’,” alisema Dkt. Witts.
Dkt. Witts alisema malengo ya kampeni hiyo ya ‘POPOTE INATIKI’ ni kuona wateja wengi zaidi wakitumia mifumo ya kidijitali jambo litakalo saidia kuongeza ufanisi katika sekta nyengine za maendeleo kwani muda ambao mteja angetumia kwenda benki sasa utatumika katika shughuli za uzalishaji. “Malengo yetu mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu ni kuona zaidi asilimia 90 ya miamala ya wateja inafanyika kupitia mifumo ya kidijitali,” alisema Dkt. Witts.

Dkt. Witts alisema Benki ya CRDB inajivunia mifumo hiyo ya kidijitali kwani imesaidia sana katika kutimiza azma ya Serikali ya kufikisha huduma kwa Watanzania wengi zaidi “Financial Inclusion” hususani wa vijijini ambapo uwekezaji kupitia mfumo wa matawi ungechukua muda mrefu kutokana na gharama za uwekezaji kuwa kubwa. 

“Ukitazama kwa upande wa mawakala sasa hivi tuna Zaidi ya CRDB Wakala 14,000 nchi nzima ambao wamefika katika kila kila kijiji, kila tarafa, kila kata,” aliongezea Dkt. Witts huku akibainisha kuwa mbali na kusogeza huduma karibu zaidi na wateja CRDB Wakala pia inasaidia kutoa ajira kwa Watanzania.
Akizungumza juu ya matumizi ya mifumo hii ya kidijitali katika kipindi hiki ambacho taifa linapambana na janga la ugonjwa wa corona, Dkt. Witts alisema Benki hiyo imekuwa ikiwasisitiza wateja wake kutumia mifumo hiyo ambayo hamhitaji mteja kufunga safari kwenda benki. 
“Tunashukuru changamoto hii imetukuta tukiwa na mifumo bora zaidi ya kidijitali, haikutulazimu kufanya mabadiliko au maboresho makubwa kwa tayari tuna mifumo imara ya SimBanking, SimAccount, Internet BankingCRDB Wakala na TemboCard, hivyo tunaendelea kuwasihi wateja kutumia mifumo hii kupata huduma katika kipindi hiki,” alisema Dkt. Witts.
Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa Masoko, Joe Bendera alisema benki hiyo inatambua vijana ndio wamekuwa mstari wa mbele zaidi katika kutumia mifumo ya kidijitali na hiyo ndiyo sababu kubwa benki hiyo imeamua kumtumia msanii kijana ‘Harmonize’ katika kuhamasisha na kueleimisha jamii juu ya matumizi ya mifumo ya upatikanaji huduma kwa njia ya kidijitali ya Benki ya CRDB. 
“Tukifanikiwa kuwafikia vijana tutakuwa tumeweza kuifikia jamii yote, Harmonize ni kijana anayejituma na ushawishi mkubwa kwa vijana na hata watu wenye umri mkubwa, ni imani yangu kwa kushirikiana naye tutakwenda kubadilisha mtazamo wa jamii juu ya matumizi ya mifumo ya kidijitali ya benki,” alisema Bendera.
Naye msanii Harmonize aliishikuru sana Benki ya CRDB kwa nafasi ya kuwa balozi wa benki hiyo huku akielezea ni ndoto ya kila msanii wa Tanzania. Harmonize alisema yeye binafsi amekuwa mteja wa Benki ya CRDB kwa muda mrefu na amekuwa akitumia njia mbadala za kupata huduma hususani SimBankingCRDB Wakala, ATMs na Internet Banking.
“Ni najua vilivyo faida ya kutumia njia hizi kupata huduma, ni njia rahisi, nafuu na salama zaidi kwa mteja. Nitumie fursa hii kuwahamasisha wateja wote kuwa hakuna haja ya kwenda tawini kufanya miamala kwani ukiwa na Benki ya CRDB ‘POPOTE INATIKI’ kupitia SimBanking, SimAccount, Internet BankingCRDB Wakala na TemboCard,” alisema Harmonize.
Share:

LHRC KUZINDUA RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA 2019 KWA NJIA YA MTANDAO


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wametangaza kupitia tovuti yao na mitandao ya kijamii kuzindua Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania 2019. 


Ripoti imepangwa kuzinduliwa Jumatano, Aprili 29, 2020 kupitia mtandao wa YouTube (Haki TV), mtandao wa Zoom na mitandao ya Twita, Facebook na Instagram. Kwa mujibu wa LHRC, hii ni mara ya kwanza kwa shirika hilo la utetezi wa haki za binadamu hapa nchini kuzindua ripoti kwa njia ya kidigitali tangu walipoanza kuchapisha ripoti hiyo mwaka 2002.

LHRC imetaja sababu kubwa ya kulazimika kufanya hivyo ni kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ambao umewalazimisha kufanya kazi kutoka nyumbani na kuepuka mikusanyiko ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo hatari.

 Kwa mujibu wa taarifa hiyo ripoti hiyo itaangazia hali ya haki za binadamu kwa mwaka 2019 sambamba na kufanya ulinganisho wa hali ilivyokuwa mwaka 2018. Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania inayoandaliwa na LHRC huangazia haki zote za binadamu ikiwemo haki za kiraia na kisiasa, haki za kiuchumi, haki za maendeleo na haki za makundi maalumu.

Ripoti hiyo pia huchambua ufanisi wa mamlaka za usimamizi wa haki na kutoa mapendekezo kwa lengo la maboresho.

Tumia link hizi Haki TV kufuatilia moja kwa moja uzinduzi huo kuanzia saa 4:00 asubuhi kupitia mtandao wa You Tube na mtandao wa Zoom.
Share:

Education Technical Experts at Palladium- Tanzania

Palladium is recruiting for Education experts for an upcoming flagship programme in Tanzania aimed at improving the quality of education for girls and boys in the country. Shule Bora will aim to reach all 11.5 million girls and boys in primary and pre-primary schools in Tanzania, working closely with the government of Tanzania to design and deliver reform and interventions across the country. Our education technical… Read More »

The post Education Technical Experts at Palladium- Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WALIOWEKWA KARANTINI WATISHIA KUJIUA


Chuo Kikuu cha Kenyatta
Baadhi ya raia waliowekwa Karantini eneo la Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya, wamezua tafrani baada ya kutishia kujiua kwa kujirusha kutoka ghorofani, wakidai kunyanyaswa na Serikali wakilazimishwa kulipa ada ya Karantini.

Raia hao wamesema hawana uwezo wa kulipa ada hiyo, kwani waliambiwa kuwa Serikali imesimamia kila kitu kuhusu wagonjwa watakaowekwa Karantini.

Kupitia video iliyoripotiwa na kituo cha televisheni cha NTV nchini humo, imewaonesha raia hao wakipiga kelele kuwa wanataka kujirusha kutoka ghorofani kutokana na kadhia hiyo, huku wahudumu wa afya wakiwasihi kuacha kufanya hivyo.

Baada ya kubadilisha uamuzi wao, mmoja wa watu waliotaka kufanya kitendo hicho amesimulia, "nilitolewa nyumbani nikiwa na shida ya kifua na kukohoa, nikapelekwa kupimwa kisha nikaletwa hapa Kenyatta, lakini siku nataka kutoka nikaambiwa huwezi kutoka mpaka ulipe, nikauliza nalipa nini wakati Serikali imesimamia kila kitu?".

Mgonjwa mwingine amesema kuwa aliletwa chuoni hapo akisumbuliwa na kifua na si Corona lakini hakupewa matibabu na amewekwa chuoni hapo kwa siku zaidi ya 21 kwa kuwa hana pesa za kulipa.

Kwa pamoja, wananchi hao wameiomba Serikali ya Kenya kuwaangalia upya kwa kuwa hawana pesa za kulipia, hivyo wanaombwa waachiwe kwa sababu wao si wahalifu.
Share:

TRUMP AITISHIA CHINA KULIPA FIDIA KISA CORONA


Rais wa Marekani Donald Trump amesema huenda nchi hiyo ikaitaka China kuilipa fidia kutokana na janga la maambukizi ya Corona kwa kile anachosema kuwa nchi hiyo ilishindwa kuzuia maambukizi ya Corona.

Trump amesema kwa sasa uchunguzi dhidi ya China unaendelea wakati huu nchi hiyo ikiwa imeshuhudia zaidi ya vifo vya watu zaidi ya elfu 56.

Hivi karibuni Rais Trump alililaumu shirika la Afya Duniani kwa kuegemea zaidi upande wa China.

Rais huyo wa Marekani alidai kwamba shirika hilo la kimataifa lilishirikiana na China katika miezi kadhaa iliyopita kupuuza hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Rais Trump alisema shirika hilo liliisifu China ingawa pana sababu ya kuwa na mashaka juu ya idadi rasmi  iliyotolewa na serikali ya China juu ya vifo vilivyotokana na mambukizi ya virusi vya Corona.

Tangu aingie madarakani Rais Trump amekuwa anayatilia mashaka mashirika ya kimataifa na mara kwa mara amekuwa analibeza shirika  hilo la afya. 

Katika bajeti ya mwezi Februari utawala wa Trump ulipendekeza kupunguza mchango wa fedha wa Marekani kwa shirika la WHO kutoka dola milioni 122.6 hadi dola milioni 59.9


Share:

HUU NDIO UVAAJI SAHIHI NA SALAMA WA BARAKOA (MASK)




Share:

Grants and Finance Officer – S&O-USAID Boresha Afya Merkle Tanzania

Consulting – Grants and Finance Officer – S&O-USAID Boresha Afya Merkle Tanzania Job Description Grants and Finance Officer The Grants & Finance Officer will be responsible for reviewing payment requests and making accountability on grants disbursed to sub grantees. This position reports directly to the Senior Grants & Finance Officer and Grants Manager. What You Will Do/Specialized Competencies… Read More »

The post Grants and Finance Officer – S&O-USAID Boresha Afya Merkle Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Engineers- CEMENT Industry- Process, Mechanical, Electrical, Production- Tanzania Achyutam International Dar es Salaam, Tanzania

Achyutam International has been mandated by a leading Cement producers to look for Engineers for their production unit There are three positions Process Engineer – 1 No Mechanical Engineer – 1 No Electrical Engineer -1 No Candidates need To be technically qualified and should posses minimum Bachelors degree and working experience with either Cement Manufuctring Plants or in… Read More »

The post Engineers- CEMENT Industry- Process, Mechanical, Electrical, Production- Tanzania Achyutam International Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Expressions of Interest – Technical Leads for Tanzania Education Development Trust Dodoma, Tanzania

Expressions of Interest – Technical Leads for Tanzania Education Development Trust Dodoma, Tanzania Education Development Trust is inviting expressions of interest from experienced technical experts to join the implementation team of an anticipated six-year programme, Shule Bora, to improve quality, inclusivity, and safety of learning for all 11.5 million children in government pre-primary and primary schools in Tanzania. In addition to providing support to… Read More »

The post Expressions of Interest – Technical Leads for Tanzania Education Development Trust Dodoma, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Atiwa Mbaroni Jijini Mbeya Kwa Kusambaza Taarifa za Uongo Kuhusu Corona

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia JOYCE KEPHAS AKYOO @ MANKA [31] Mfanyabiashara na Mkazi wa Stereo Jijini Mbeya kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu [COVID 19] katika Mtandao wa Kijamii.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 27.04.2020 majira ya saa 13:30 Mchana baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kufanya msako huko eneo la Stereo lililopo Kata ya Manga, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya.

Ni kwamba mnamo tarehe 30.03.2020 majira ya saa 14:09 Mchana mtuhumiwa alituma taarifa za uongo na zenye lengo la kupotosha kuhusiana na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu kwenye kundi “Fans of Mwailubi Car Wash” katika mtandao wa WhatsApp kwa kuweka picha za marobota ya nguo akieleza kwa maandishi na kwa sauti baada ya kujirekodi akisema “Mablanket ya Wagonjwa wa Corona ambao wamefariki nchini China na nguo hizo zinaletwa barani Afrika na ugonjwa wa Corona” Mtuhumiwa aliendelea kuongea na kuandika akitahadharisha watu wasikubali msaada huo.

Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Tangu kuanza kwa Janga la Homa Kali ya Mapafu [COVID 19] na kutangazwa kama Janga la Dunia, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Viongozi wakuu wa Nchi ndio wamekuwa wakitoa taarifa kuhusiana na ugonjwa huo pamoja na namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi yake, hata hivyo Serikali imekuwa ikitoa makatazo mbalimbali kwa wananchi kuacha kutoa taarifa za kupotosha umma na kusubiri kupata taarifa kutoka vyanzo sahihi.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mpaka wa Tanzania na Malawi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, maeneo ya Karantini na kudhibiti magari ya kubeba abiria kwa kuwataka kupakia abiria kulingana na siti zilizopo [level seat].

Pia elimu inaendelea kutolewa kwa Wananchi katika maeneo mbalimbali namna ya kujikinga na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona [COVID 19] na kuwataka wananchi kufuata maelekezo yanayotolewa na Viongozi Wakuu wa Nchi, Wataalamu na Wizara ya Afya ikiwemo kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono [Sanitizer].

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger