Saturday 22 February 2020
Serikali ya Mseto yaundwa Sudan Kusini
Miji mitatu ya Tanzania yatajwa kasi ya ongezeko la watu duniani
Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa (UN) ya mwaka 2017 ukuaji huo utatokea katika nchi tisa, kati ya nchi hizo, tano zinatoka barani Afrika ambazo ni Tanzania, Congo, Uganda, Nigeria, na Ethiopia.
Kwa mujibu wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) ifikapo mwaka 2035 miji 15 ambayo idadi ya watu inakuwa kwa kasi zaidi, ambayo yote inatokea Afrika, inatarajiwa kuwa na wastani wa watu mara mbili zaidi ya waliopo sasa, ambapo katika miji hiyo, Tanzania imefanikiwa kuingiza miji mitatu.
Nchi za Afrika zinakadiriwa kuwa zitakuwa zaidi kutokana na kuwa na vijana wengi zaidi duniani. Zaidi ya 75% ya watu wote barani Afrika wana umri chini ya miaka 35, kwa mujibu wa UN.
Hapa chini ni orodha kamili ya miji 15 duniani ambayo ongezeko la watu litakuwa kwa kasi zaidi hadi ifikapo mwaka 2035:
15. Lilongwe, Malawi: Hadi mwaka 2020 ina watu 1,122,000, na idadi hiyo inakadiriwa itakuwa kwa 97% hadi 2,210,000.
14. Ouagadougou, Burkina Faso: Hadi sasa kuna watu 2,780,000,na idadi itaongezeka kwa 97% kufikia 5,481,000.
13. Uige, Angola: Jumla ya watu sasa ni 511,000, makadirio ya ukuaji ni kwa 98% hadi kufikia 1,013,000.
12. Bobo-Dioulasso, Burkina Faso: Idadi ya watu mwaka sasa ni 972,000 ambapo itakuwa kwa 100% kufikia.
11. Dar es Salaam, Tanzania: Mji huu una jumla ya watu 6,702,000, kasi ya ukuaji ni 100% ambapo itafikia watu 13,383,000.
10. Tete, Mozambique: Jumla ya watu katika mji huu ni 371,000, ongezeko litakua kwa kasi ya 101%hadi kufikia 744,000.
9. Niamey, Niger: Jumla ya watu 1,292,000, kasi ya ukuaji ni 101% ambapo itafikia watu 2,600,000.
8. Bunia, Congo: Mji huu una jumla ya watu 679,000, ambapo idai ya watu itaongezeka kwa kasi 101% kufikia 1,368,000.
7. Gwagwalada, Nigeria: Mji wa Gwagwalada una jumla ya watu 410,000, ambapo ukuaji watu unatarajiwa kukua kwa kasi ya 102% kufikia 827,000.
6. Mwanza, Tanzania: Mji wa Mwanza una watu 1,120,000, ukuaji wake utakuwa kwa kasi ya 102% kufikia 2,267,000.
5. Songea, Tanzania: Mji huu uliopo mkoani Ruvuma una watu 353,000 na unakadiriwa kuwa utakua kwa 110% kufikia watu 740,000.
4. Kabinda, Congo: Mji unakadiriwa kuwa na watu 466,000, na ukuaji wake utakua kwa 110% kufikia watu 979,000.
3. Kampala, Uganda: Kampala ina makadirio ya watu 3,928,000, na kasi ya ukuaji inatarajiwa kuwa kasi 112% kufikia 7,004,000.
2. Zinder, Niger: Mji huu unakadiriwa kuwa na watu 489,000, ukuaji wake unakadiriwa kuongezeka kwa 118% kufikia 1,065,000.
1.Bujumbura, Burundi: Mji huu unaongoza kwa kasi ya ukuaji wa watu ambapo hadi mwaka 2020 unakadiriwa kuwa na watu 1,013,000, idadi hiyo itakua kwa 123% kufikia 2,263,000.
Serikali Kudhibiti Wahamiaji Haramu Wanaotumia Njia Za Treni
Serikali imeapa kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini kwa kutumia usafiri wa treni huku ikiwataka wananchi kuacha tabia ya kuwahifadhi na kuwasafirisha wahamiaji hao kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, mkoani Tabora wakati wa kikao na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani hapa baada ya kuwepo kwa taarifa za kiintelijinsia zinazohusisha baadhi ya wahamiaji haramu kutumia usafiri huo kuingia katika mikoa mbalimbali nchini
“Nchi yetu inaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu,hivyo ni vyema kudhibiti watu wanaoingia nchini pasina kufuata utaratibu rasmi,na tuna taarifa juu ya wahamiaji haramu sasa kuanza kutumia njia ya treni kuingia nchini tena wengine wakisaidiwa na raia sasa natao onyo wenye tabia hiyo kuacha mara moja na vyombo vya ulinzi na usalama viimarishe ulinzi katika maeneo husika” alisema Masauni
Akizungumza katika Kikao hicho,Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tabora,Kamishna Msaidizi,Amiru Sadiki aliiomba serikali kuweka maafisa uhamiaji katika vituo vyote vya reli nchini ili kuweza kukagua wasafiri wanaoingia katika mikoa mbalimbali kama ilivyo katika viwanja vya ndege.
Awali akitoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora,Kamishna Msaidizi wa Polisi,Barnabas Mwakalukwa alisema hali ni shwari huku kukiripotiwa matukio machache.
“Upungufu wa makosa ya mauaji ambayo hapo awali yalikuwa kero kubwa kwa wananchi umetokana na juhudi za polisi katika kufanya doria ya kukamata waganga wa kienyeji wanaojihusisha na ramli chonganishi na tayari jeshi tumeanza operesheni maalumu inayoendelea katika mikoa ya Shinyanga,Geita,Mwanza,Kagera,Simiyu na Tabora huku kukiwa na mafanikio makubwa na hali sasa inaendelea kutulia” alisema ACP Mwakalukwa.
YANGA YATOA MSAADA WODI YA AKINA MAMA KITUO CHA AFYA NGAMIANI JIJINI TANGA
Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz kulia akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ngamiani Jijini Tanga Anjelina Mahaka kushoto kwa ajili ya wakina mama wajawazito wanaojifungua kwenye kituo hicho leo katikati anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga Thabithy Kandoro
Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz kulia akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ngamiani Jijini Tanga Anjelina Mashaka kushoto kwa ajili ya wakina mama wajawazito wanaojifungua kwenye kituo hicho katikati anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga Thabithy Kandoro
Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz kulia akikabidhi msaada wa vitu mzazi aliyemkuta kwenye wodi ya wakina mama wajazito kwenye Kituo cha Afya cha Ngamiani Jijini Tanga kushoto ni kwa ajili ya wakina mama wajawazito wanaojifungua kwenye kituo hicho leo katikati anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga Thabithy Kandoro
Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo kulia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga Thabithy Kandoro
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ngamiani Jijini Tanga Anjelina Mashaka akizungumza huku akiishukuru Klabu ya Yanga kwa msaada huo
Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga Thabithy Kandoro akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo kushoto ni Afisa Mhamasishaji wa klabu hiyo Antonio Nugaz
Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaza kushoto akiwaongoza wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuingia kwenye kituo cha Afya Ngamiani Jijini Tanga kwa ajili ya kutoa msaada .
KLABU ya Yanga imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye wodi ya wakina mama wajawazito kwenye kituo cha Afya Ngamiani Jijini Tanga ikiwa ni mkakati wao kusaidia makundi mbalimbali kila wanapo kwenda kucheza mechi zao za ligi kuu ikiwa ni mpango wao wa kurudisha kwa jamii.
Msaada huo umekabidhiwa leo na Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz kwa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Anjelina Mashaka katika halfa iliyohudhuriwa mashabiki na wanachama wa timu hiyo mkoani Tanga.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Nugaz alisema wana mshukuru Mwenyezi Mungu amewawezesha kuwqa sehemu ambazo wazazi wao ambao walizaliwa kwenye vituo mbalimbali vya afy na wao wamefika kwenye kituo hicho kwa kile walichobarikiwa wakiotoe wodi ya wakina mama.
Alisema msaada ambao wameutoa pamoja na vitu vyengine lakini neti za kujikinga na mbu ambazo wamezikabidhi zitakuwa msaada mkubwa kwao ili kuepukana na kuumwa ugonjwa wa malaria.
“Wazazi ambao wamebahatika kupata watoto wanapaswa kujikinga na mbu ambao wanaeneza malaria hivyo katika kurudisha kwa jamii timu ya wananchi tumeona tuwasaidia neti na vitu vyengine ikiwemo sabuni na vifaa kwa ajili wa watoto wadogo”Alisema Mhamasishaji huyo.
Aidha alisema kwamba amefurahishwa na namna wanachama wa Yanga na mashabiki waliovyoonyesha mshikamano wa pamoja kwenye jambo hilo hivyo kwa niaba ya kamati ya utendaji chini ya Mwenyekiti wao Dkt Mshindo Msola na timu nzima.wanakwenda kuchukua pointi tatu ingawa mechi itakuwa ni ngumu.
Awali akizungumza katika halfa hiyo Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Anjelina Mashaka aliishukuru klabu hiyo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia msaada huo ambao umefika wakati muafaka.
“Nashukuru kupokea neema ambazo mmezileta Yanga kwa niana ya Jiji la Tanga natoa shukrani zangu za dhati kwa ajili ya zawadi na wagonjwa wetu ambao wanajiandaa kupata watoto”Alisema Mganga huyo
Alisema kwamba pia wanathamini mchango wao wa kutoa sadaka kwap ambao utawasaidia kutokana na hapo awali kuwa na uhitaji wa neti ambazo zitasaidia kwenye kituo hicho.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Mashindano wa timu ya Yanga Thabithy Kandoro alisema kwamba timu halisi ya Yanga lazima iende kwa vitendo ni jambo la msingi wao.
Alisema wao kama timu ya wananchi wana sababu ya kuijenga timu yao na kuwa wazalendo na kuhakikisha wananchi wanafaidi na kupata afadhali watu wengine wajitokeze kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali.
WIZARA YABARIKI MSAFARA WA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA
Waziri mkuu wa Lesotho anayekabiliwa na mashtaka ya kumuua mkewe wa zamani aondoka nchini
Bukoba DC Job opportunities, February 2020
Bukoba DC Job opportunities, February 2020
The post Bukoba DC Job opportunities, February 2020 appeared first on Udahiliportal.com.
Walimu Mkoani Tabora Watakiwa Kuwafundisha Wanafunzi Umuhimu Wa Uzalendo
WALIMU Mkoani Tabora wametakiwa kuwalea kimaadili wanafunzi na wanavyuo ili waweze kukua katika uadilifu na uzalendo ambao utakaowawezesha kushiriki ujenzi wa Tanzania mpya msingi mkuu ni viwanda.
Kauli hiyo imetolewa leo na katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa ufunguzi wa mafunzo na maelekezo kuhusiana na uendeshaji wa klabu za maadili kwa walimu wa shule za msingi ,sekondari na vyuo.
Alisema kuwa katika kukuza uchumi Tanzania mpya ipo haja ya kuwa na vijana ambao wamekuzwa katika msingi ya uadilifu na uzalendo ambao utaweka mbele maslahi ya Taifa na sio masalahi binafisi.
“Maslahi ya Taifa yatadumu daima …lakini maslahi ya mtu binafsi ni ya muda baada ya kufa basi nayo yamekwisha” alisema.
Makungu alisema mafunzo hayo ni muhimu sana katika kujenga jamii yenye maadili mema ambayo yatasaidia kuzalisha Viongozi wazalenda na waadilifu.
Aidha Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwapongeza walimu kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ya kukuza maadili mkoani Tabora na kuongeza kuwa uanzishwaji wa Klabu za Maadili utaleta mabadiliko chanya na kuongeza ufaulu kwa vijana mashuleni na vyuoni.
Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Kanda ya Magharibi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Gerald Mwaitebele alisema Ofisi hiyo imeamua kuanzishia Klabu hizo ili kuwajenga vijana tangu awali ili kuwajenga kukua kimaadili na uzalendo wakiwa wadogo.
Alisema ni kazi kubwa kufundisha umuhimu wa maadili kwa mtu mzima kuliko kufundisha akiwa mdogo kwa kuwa atajengeka katika hali ya uadilifu na kuipenda nchi yake.
Mafunzo hayo ya siku moja yameshirikisha walimu wa shule za Msingi, sekondari na Vyuo vya Elimu vilivyopo Manispaa ya Tabora na yalikuwa na mada za Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Mgongano wa Masilahi na Mwongozo wa Uanzishwaji na Uendeshaji wa Klabu za Maadili
mwisho
Waziri Mkuu: Uzalishaji Mbegu Za Michikichi Unaridhisha
Aliyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Frbruari 21, 2020) alipotembelea kituo cha utafiti wa zao la michikichi cha Tari Kihinga kilichopo wilayani Kigoma alipokuwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Kigoma.
Akiwa kituoni hapo, Waziri Mkuu alipokea taarifa ya utafiti juu ya uendelezaji wa zao la michikichi uliliyofanywa na TARI kuanzia mwaka 2018, ambapo hadi kufikia Februari 15, 2020 taasisi hiyo ilikuwa imezalisha mbegu 1,525,017 ambazo zinaweza kupandwa katika shamba lenye ukubwa wa ekari 30,500.
Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kulipa kipaumbele zao la michikichi kwa lengo la kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini, hivyo ufufuaji zao hilo utaliwezesha Taifa kuzalisha mafuta ya kutosha kwa ajili ya mahitaji ya ndani na ziada itakayobakia itauzwa nje ya nchi.
Kufuatia hatua hiyo, Waziri Mkuu amewataka wananchi hasa vijana kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo kwa wingi kwa kuwa upo uhakika wa kupata mbegu bora na pia zao hilo litawakwamua kiuchumi na kuwaondolea umasikini wa kipato.
Pia, amewaagiza Maofisa Ugani kuwafuata wakulima katika maeneo yao na kuwaelekeza namna ya kulima zao hilo kuanzia hatua za awali za utayarishaji mashamba, matumizi bora ya pembejeo ili waweze kulima kisasa na kujiongezea tija.
Baada kutembelea kituo hicho Waziri Mkuu alizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mwanga Community Centre uliopo Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka watumishi wa umma watenge muda ya kusikiliza kero za wananchi.
“Watumishi mnatakiwa kwenda kwa wananchi na kusikiliza kero zinazowakabili na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi. …hamuendi na kama mngekuwa mnaenda kusingekuwepo na mabango kwani kitendo cha kuwepo mabango ni ishara tosha kwamba hamuendi.”
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali imepeleka fedha nyingi mkoani Kigoma za kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo sh bilioni 4.6 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, ambapo Manispaa ya Kigoma Ujiji inapata sh milioni 50 kila mwezi hivyo hakuna sababu ya wananchi kukosa dawa.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha na kusogeza huduma za afya kwa kujenga vituo vya afya karibu na makazi ya wananchi zikiwemo za afya ili kuwapunguzia kutembea umbali mrefu hadi hospitali za wilaya au mkoa.
Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia Baraza lake la Madiwani wahakikishe wanasimamia vizuri matumizi ya fedha mbalimbali zinazotolewa na Serikali kwa lengo la kugharamia miradi ya maendeleo.
Waziri Mkuu alikemea tabia ya baadhi ya wananchi katika maeneo mengi ya mkoa wa Kigoma kudai fidia kwenye maeneo hata ya mapori na kukwamisha baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa hospitali ya kanda, aliwataka wabadilike.
Awali, Waziri Mkuu alishiriki swala ya Ijumaa katika msikiti wa Mujahidina uliopo eneo la Buzebazeba mijini Kigoma, ambapo alitumia fursa hiyo kuwaasa waumini wa dini ya kiislam na wananchi kwa ujumla kuendelea kushikama na kulinda amani.
Pia, Waziri Mkuu aliwahamasisha walime zao la michikichi kwani Serikali imeamua kulifufua zao hilo ili waweze kuondokana na umasikini. Wanaotamani kulima michikichi wajiandae wakati utakapofika watasambaziwa miche.
(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
Friday 21 February 2020
Picha : JAMBO YATOA MSAADA WA VINYWAJI KWA JESHI LA AKIBA SHINYANGA
Finance Officer at Norwegian Refugee Council (NRC)
Position: Finance Officer (Tanzania Nations only Tanzania, Norwegian Refugee Council NRC is looking for qualified candidate base at Kibondo,Kigoma The purpose of the Finance Coordinator is to Ensure accountability and accurate financial reporting in conformity to NRC’s accounting practices and standards and donor requirements. All NRC employees are expected to work in accordance with the organisation’s core values: dedication, innovation,… Read More »
The post Finance Officer at Norwegian Refugee Council (NRC) appeared first on Udahiliportal.com.
Program Officer at Kilimo Trust
Job Advert – Program Officer – Policy Advisor Job Grade: KT4 Unit of Service: KT Tanzania Reports To: Country Team Leader Tanzania Duty Station : Dar-es- Salaam -Tanzania Employment Category: One Year Renewal Contract Purpose of the Job ➢ To support Program Development through, Program implementation, Policy Development & Promotion ➢ To ensure that Private sector interests are reflected in… Read More »
The post Program Officer at Kilimo Trust appeared first on Udahiliportal.com.
Finance Manager at School of St. Jude
Finance Manager Job Summary To oversee all areas of finance related to the school including but not limited to; accounts receivable, accounts payable, capital spending, budgeting, financial reporting and purchasing. Job Description Reporting To – Founding Director. Working relationships – Accounts Team, all Business Teams, Purchasing Teams and Academic Departments. Key Responsibilities & Tasks Oversee all finance related… Read More »
The post Finance Manager at School of St. Jude appeared first on Udahiliportal.com.
Territory Manager at Vodacom
Territory Manager Description Maximises sales revenue by working through and with distributors, dealers and other partners within assigned territory. Works alongside distributors and staff to carry out all the activities required to achieve set targets. Monitors stock levels both at distributor level and in the trade; also identifies gaps in the distribution chain and brings them to management… Read More »
The post Territory Manager at Vodacom appeared first on Udahiliportal.com.